Bila Magufuli kushika utawala awamu hii ya 5 je nchi ingekuwaje kufikia mwisho wa mwaka huu na kipindi kama hiki?

shige2

JF-Expert Member
Oct 11, 2016
8,106
3,967
Hebu kidogo tuchemshe bongo. Nimeleta swali zuri tu tulijadili. Kama rais Magufuli asingeingia madarakani katikla awamu hii nchi ingekuwaje na hasa kwa watu MASKINI na wanyonge?
Sisemi he is flawless/mapungufu.

Maana ukweli kabisa nchi hii tulifikia kipindi cha mtu kulinga hata kukutisha kwa sababu ana hela na hela hiyo ni ya WIZI.
MNYONGE hakuwa na MTETEZI.
Sasa hivi hiyo TABIA HAIKO sote TUKO SAWA.

KODI zililiwa na wachache na kuiweka nchi hii katika hali MBAYA ya OMBA OMBA.
nIseme kuwa most of the elites and privileged kila WIKIENDI walikuwa wakienda DUBAI nk kula Bata. Wakati walala hoi wanahanahangaika hawakuwa na msaada wowote. Leo MACHINGA ANATAMBILIKA. Dah! Pongezi sana.Magufuli..

Sincerely speaking kama huyu mzee asingeingia madarakani awamu hii.
Basi nchi hii
iingemilikiwa na watu WACHACHE wenye hela..

Ni lazima nieleweke pia kuwa si kila jambo naweza kukubaliana naye. Kuna mengine natofautiana naye KIMITAZAMO, Bali anabaki kuwa ni rais wangu..
Kama ni Mapungufu hata mimi na wewe tunayo mengi tu.

Lakini KIUKWELI nchi hii Mh Dr.JPM AMAEIOKOA kabisa.
Angalia miundo mbinu yetu sasa.

Kununua Ndege mpya at least watalii WAJE MOJA KWA MOJA mpaka Tanzania ni jambo la KUJIVUNIA.

KABANA WEZI,

Makusanyo ya Kodi YANATUMIKA na TUNAONA.

Tanzanite yetu India hawana namna bali kufuata sheria.

ELIMU ya BURE NK. NK
Ni mengi sana.
Na yote haya ameyafanya within MIAKA 3


.
Ukweli ni kuwa hat
a ile hotuba aliyoitoa leo wakati akiweka jiwe la MSINGI la ujenzi wa barabara.

Ungeamwagalia body language yake, ikiwemo TONE yake na zaidi alIpotoa HISTORY yake ya MAONO aliyokuwa nayo tangu zamani ni ISHARA TOSHA kuwai alikuwa akiandaliwa na MOLA ILI ATUKOMBOE.

BODY language yake alionyesha as someone with a sincere heart kabisa/ Mwenye nia njema kwa ajili ya WATANZANIA.

Naamini mwaka 2019 tutakuwa mbali zaidi kisiasa na kiuchumi, Na nafikiri hata UHUSIANO kati ya UPINZANI na CCM utabaki wa kisiasa na wala si wa ugomvi.

Ahsante awamu ya 5
Ahsante Rais Magufuli na TEAM yako YOTE.

Kheri za Krismasi na mwaka mpya 2019. Maana naamini unakuja na MAPYA KABISA amabayo Watanzania wengi hata wale wasiokupenda watapiga about turn.

Uwe na mwaka mpya wa Kheri na baraka. Bila wewe nchi hii ilikuwa inaingia SHIMONI. Let the truth be told!

Swali langu KUU kama magufuli asingeingia utawalani awamu hii ya 5 nchi ingekuwaje KUFIKIA MUDA HUU?
 
Sote tungekuwa na pesa.
True we uoni nyumba za nyasi vijijini zilivokuwa zikifutika Kwa kasi ya 4G mazao yote yaliuzika,vifaa vya ujenzi kila mtu alimudu,miundombinu imejengwa nyakati zote, deni la taifa lilikualikipungua kila mwaka, ajira zilikuwa tele,biashara zililipa,ofisi ziliweza jiendesha, NHC nyumba zilikuwa zikijengwa kila kona ya nchi,watu walilipwa mafao yao cash,viwanda vilikuwa vikichupua kama uyoga Kwa kasi,maghorofa mijini yalikimbizana,vyote vimesimama
 
Vyuma vingekaza, Ngosha kasaidia sana kufanya pesa ipatikane mtaani.

Asingeingia nchi ingetumbukia katika udikteta, angalau sasa hivi bunge liko live, wapinzani wanapata fair ground kufanya siasa

Asingeingia watu wangepotea, kutekwa sana, Awamu hii hilo halijatokea kabisa, Kweli Ngosha anatisha!

Asingeingia, watu wangepiga pesa ndefu, yaani watu wangepiga hata Trillion 1.5, lakini alivyoongia hakuna wa kuthubutu kugusa hata senti.

Ninachoona pia, laiti asingeingia Wapinzani wangenyanyaswa sana, na wrngine wangeweza kupigwa hata risasi na uchunguzi usifanyike, lakini yeye alipoingia, yaani kila kitu shwari, Wapinzani wanapeta hakuna hata mmoja ambaye kapigwa kirungu achilia mbali risasi!
 
Hivi wana Lumumba Rais anachaguliwa ili afanyie nini nchi yake ?! Tunategemea aifanyie nchi hii waliohaidi ktk ilani ya uchaguzi . Lakini pia awe Rais wa wote waliomchagua na wasio.
Na nafikliri hata leo alirudia hilo hilo unalolizungumzia. Ni rais wa WOTE!
 
Back
Top Bottom