Cyprian Majura Musiba ni nani na anatumwa na nani?

StingRay

JF-Expert Member
Jun 28, 2014
503
628
Unapata wapi nguvu ya kuutangazia umma wa Watanzania kwamba hawa ndugu zetu ni hatari??? Mamlaka unayatoa wapi Musiba???

Maana ya mtu hatari katika usalama wa taifa ni wewe wa kutoa hiyo hukumu na maamuzi ya kuwaita wenzetu Hatari???

Naombeni msaada ni nani huyu? Anapata wapi mamlaka na nani amemtuma?

Samahani JF niliiacha hii habari hewani bila kuiimarisha kwasababu huyu jamaa alinichefua sana, nasema ukweli nilifika hatua ya kufikiria kuukana utaifa wangu wa Tanzania. Polisi wanamuacha huyu? Vyombo vya habari mnaripoti mtu kama huyu really na mnaona ni taarifa ya kawaida tu....???

FullSizeRender_16.jpg
 
Unapata wapi nguvu ya kuutangazia umma wa Watanzania kwamba hawa ndugu zetu ni hatari??? Mamlaka unayatoa wapi Musiba.....??? Maana ya mtu hatari katika usalama wa taifa ni wewe wa kutoa hiyo hukumu na maamuzi ya kuwaita wenzetu Hatari???

Naombeni msaada ni nani huyu?? Anapata wapi mamlaka na nani amemtuma????
Unamzungumzia Willy Gamba au.....?!!
 
Umeleta habari kana kwamba kila mtu anajua kinachoendelea eeh huyo musiba kafanyaje
Ameitisha press conference na kutaka vikosi vya usalama viwashughulikie bila huruma Mange Lissu,Mbowe,Maria Sarungi,Zitto na wengine WANNE kwa madai ya kuhatarisha usalama wa nchi na kutumiwa na CIA na FBI
Hana kazi anatafuta huruma ya Magu na Bashite
 
Kila mkosoaji wa Chadema lazima muulizie wasifu wake..
mtaulizia wananchi wa nchi nzima sasa mkidhani wanatumiwa na CCM
Hamna ukosoaji wa maana ila ni pale mdaiwa wa haki. Anapo taka wadai wa haki waje hivi mara vile mara fanyeni hiki mara kile hamjafanya.
Wapeni haki yao muone kama hao watu ni wasumbufu au wakorofi.
Mtu yoyote ukimnyima haki yake lazima msumbuane.
Ndiyo maana upande mmoja unatuma polisi nk.
Jee hawa wa kijani wao huwa hawana makosa???
Au umewahi kufikiri kwamba tungekuwa na jeshi la polisi maalumu kwa Chadema. Nini kingetokea, maana hao wengine kwa mtazamo wako ni wa ccm.
Kuna watu wanatembea nchi nzima kukinadi chama. Na kufanya mikutano Wao halali.
Lakini kuna wengine hata wakikutana ndani ofisini kwao ni kosa. Wanakaa polisi siku tatu.
Kwa mtazamo huu hamtendi haki.
Tendeni haki. Kila mtu Atakuw huru. Hamna mkorofi.
 
WATU 10 AKIWEMO MANGE KIMAMBI WANAOTAJWA KUWA HATARI KWA USALAMA WA TAIFA
MTILAH BLOG / 42 minutes ago



MANGE KIMAMBI
Mkurugenzi wa Kampuni ya CZI, Cyprian Musiba leo Februari 25, 2018 amezungumza na waandishi wa habarina na kuwataja watu 10 hatari kwa usalama wa Taifa.

Musiba amesema serikali inatakiwa kuwa makini na watu wao kwani wanaweza kusababisha machafuko nchini .Musiba amewataja watu hao ni.

1.Mange Kimambi-Musiba amesema mange kimambi anatumiwa na FBI(Shirika la kijesusi la marekani)

2.Freeman Mbowe-Musiba amesema CHADEMA imepeleka vijan 500 ujerumani kwa ajiri ya kuratibu ajenda za kiarifu katika Taifa

3.Mari Sarungi-Musiba amesema maria sarungi kazi yake ni kuongea negative juu ya serikali

4.Zitto kabwe-Musiba amesema Zitto anahamasisha vyama vya siasa viungane viandamane tyarehe 26/04/2018 ili walete vurugu.

5.Lissu

6.John Heche
7.John Marwa (Alikuwa mlinzi wa Salum mwalim wakati wa kampeni Kinondoni)
8.Evarist Chahari-Mtanzania anaishiu Uingereza


9.Julius Mtatiro
10.Janja wind-Kikundi cha wafuasi wa CUF


Cyprian Musiba ameiomba serikali na vyombo vya ulinzi kuwafuatilia watu hao

Zaidi msikilize kwenye video hii hapa chini
 

Similar Discussions

Back
Top Bottom