Bila kuitoa kafara CCM Taifa litaangamia | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Bila kuitoa kafara CCM Taifa litaangamia

Discussion in 'Jukwaa la Siasa' started by Kalumbesa, Jun 4, 2011.

 1. Kalumbesa

  Kalumbesa JF-Expert Member

  #1
  Jun 4, 2011
  Joined: Nov 24, 2010
  Messages: 1,009
  Likes Received: 6
  Trophy Points: 135
  Tanzania tumekuwa tukijivua amani kwa miaka mingi sana na hadi leo licha ya viongozi wetu kuonyesha dhahiri akili zao zimefika mwisho wa kufikiri yaliyo na amani na kuanza kutumia njia za utawala wa vitisho,ubabe mpaka kudiriki kuua wananchi au kutoa watu uhai ki rahisi tu, wengi wetu wanaona amani tuliyo nayo itaendelea kudumu tu..Mimi naona Taifa linaelekea kubaya.Serikali yoyote ile ikishindwa kuliongoza vema Taifa,hutaka kuendelea kubaki madarakani kwa njia zote hasa wizi wa kura na mtutu wa bunduki..Haya yameanza kujitokeza Tanzania na yana ishara mbaya sana huko tuendako...Binafsi naona hata huu mwaka tulio nao unaweza usiishe bila matukio makubwa ya kulitingisha Taifa...ili Taifa hili liweze kuondokana na balaa lililo mbele,inabidi tutoe kafara..na anayestahili kutolewa kafara ili kulinusuru Taifa ni CCM..Ni jukumu letu sote wananchi kulitambua hili mapema na kuwa tayari kulikamilisha wakati utakapokua muafaka...Nimalizie kwa kusema....Kama CCM angekuwa mtu tena mwanangu basi ningemtoa kafara fasta ili kulinusuru Taifa
   
 2. kweleakwelea

  kweleakwelea JF-Expert Member

  #2
  Jun 4, 2011
  Joined: Nov 29, 2010
  Messages: 2,422
  Likes Received: 437
  Trophy Points: 180
  kweli kaka...

  huku makazini wameanza kututazama kama wapinzani na sio working colleagues.....

  promortion kila kitu kimekuwa hivyo hivyo...

  viongozi wetu wanawaerka selo kila sehemu..


  wanatengeneza genocide ya ajabu sana...hata rwanda walianza vivyo hivyo!!!

  ina maana chadema tukichukua nchi tuanze kuwabalasa CCM maofisini? ni nini kitatokea??? mwenye akili na apime!
   
 3. rosemarie

  rosemarie JF-Expert Member

  #3
  Jun 4, 2011
  Joined: Mar 22, 2011
  Messages: 6,768
  Likes Received: 1,023
  Trophy Points: 280
  idea ni nzuri,lakini ningekuwa mimi ningesema bila kumwaga damu taifa linaangami,,naamini hakuna uhuru wa bure bila damu
   
 4. hashycool

  hashycool JF-Expert Member

  #4
  Jun 4, 2011
  Joined: Oct 2, 2010
  Messages: 5,899
  Likes Received: 442
  Trophy Points: 180
  I need me a long range sniper riffle
   
 5. Kalumbesa

  Kalumbesa JF-Expert Member

  #5
  Jun 8, 2011
  Joined: Nov 24, 2010
  Messages: 1,009
  Likes Received: 6
  Trophy Points: 135
  Ukiwa na Snipper utaanza kumdondosha nani? au main target atakuwa nani?
   
 6. Mikael P Aweda

  Mikael P Aweda JF Gold Member

  #6
  Jun 8, 2011
  Joined: Dec 17, 2010
  Messages: 2,934
  Likes Received: 33
  Trophy Points: 0
  kuna mstari katika biblia unasema, Mbegu ya haradali lazima ufe ili izaliwe mbegu nyingine mpya, nzuri na nyingi. Tafakari.
   
 7. Kalumbesa

  Kalumbesa JF-Expert Member

  #7
  Jun 8, 2011
  Joined: Nov 24, 2010
  Messages: 1,009
  Likes Received: 6
  Trophy Points: 135
  Ni kweli mkuu..tatizo hii mbegu(CCM) haikubali kufa hivi hivi inaonyesha dhahiri kwamba inataka kufa baada ya kunyonya damu za watanzania kama walivyokwisha anza kuua wananchi ki urahisi..Lakini mwisho wa siku tutawang'oa tu..nchi hujengwa na wananchi na lazima chama kipate baraka za wananchi,wananchi wakishasema basi,chama kimefikia kiama!
   
 8. T

  Taifa_Kwanza JF-Expert Member

  #8
  Jun 8, 2011
  Joined: Sep 3, 2010
  Messages: 443
  Likes Received: 2
  Trophy Points: 0
  Acha kabisa kufanya reference ya kwenye biblia kwenye siasa za ulimwengu huu.
  Hayo ni matumizi ya biblia for personal profit, huo ni upotoshaji wa neno la Mungu,
  never in the bible God has instructed anyone to kill, well even to fight
   
 9. Kalumbesa

  Kalumbesa JF-Expert Member

  #9
  Jun 8, 2011
  Joined: Nov 24, 2010
  Messages: 1,009
  Likes Received: 6
  Trophy Points: 135
  Sidhani kama amelitumia andiko hilo kwa ubaya....mimi nimemuelewa mbegu inayotoa mazao mabaya yapaswa kuachwa na mbegu mpya ipandwe...Ametumia huu kama mfano sidhani kama ana nia mbaya...CCM sasa inatoa mazao mabaya na anatusihi tupande mbegu nyingine na kwa sasa bila shaka mbegu hiyo ni CHADEMA...hata viongozi wa siasa hutumia baadhi ya mistari ya dini kuelimisha jamii..mbaya ni kuitumia vibaya kama alivyokuwa anafanya MA ROPE...Mwalimu Nyerere alikuwa anaitumia vizuri sana BIBLIA katika hotuba zake..hili si jambo baya,si katika siasa tu mafundisho ya BIBLIA ni muhimu sana katika maisha yetu ya kila siku, hasa kwa wale wanaoiamini BIBLIA..vibaya tu kuitumia kama kitabu cha hadithi na kutoa tafsiri za kidunia au unavyojisikia..
   
 10. ELNIN0

  ELNIN0 JF-Expert Member

  #10
  Jun 8, 2011
  Joined: Nov 26, 2009
  Messages: 3,771
  Likes Received: 221
  Trophy Points: 160
  Ni kweli na baya zaidi CCM hawana mtu mwenye mvuto ambaye akisimama mbele za wananchi na akaongea hoja watu wakashangilia. Ni nani ndani ya CCM ya sasa ambaye ni masafi mwenye mvuto na nguvu ya hoja!!

  Wanataka kuwatoa kafara mapacha watatu ili kurudisha imani kwa wananchi, lakini kazi hiyo ni ngumu sana, na hata wakiwatimua hao mapacha bado wananchi wana hoja nyingi sana za kifisadi ambazo haziwezi pata majibu kamwe aka kagoda and the likes...
   
 11. WISDOM SEEDS

  WISDOM SEEDS JF-Expert Member

  #11
  Jun 8, 2011
  Joined: Jun 1, 2011
  Messages: 782
  Likes Received: 14
  Trophy Points: 35
  Kuitoa CCM kwa aina hii ya wananchi kuwachagua viongozi kwa kununuliwa

  hati zao za kupigia kura kwa kilo mbili za sukari na upande wa khanga kutokana

  na hali zao kimaisha kuwa duni kiasi kwamba hawawezi hata kukumbuka ni lini

  ilikuwa mara ya mwisho kwao kunywa chai yenye sukari!


  Labda ya Tunisia yahamie hapa.
   
 12. Kalumbesa

  Kalumbesa JF-Expert Member

  #12
  Jun 8, 2011
  Joined: Nov 24, 2010
  Messages: 1,009
  Likes Received: 6
  Trophy Points: 135
  Wananchi hao hao ndio wengi wao wameamka sasa..watang'oka tu, wakichakachua kwenye sanduku la kura ya Tunisia,Egypt,Ivory Coast yatajitokeza...Waelewe Watanzania wanazidi kufunguka,kuelimika zaidi..Tanzania ya leo sio ya jana na tumechoshwa na upupu wao!!
   
 13. Kalumbesa

  Kalumbesa JF-Expert Member

  #13
  Jun 8, 2011
  Joined: Nov 24, 2010
  Messages: 1,009
  Likes Received: 6
  Trophy Points: 135
  Wanayoyafanya CCM siku baada ya siku mimi naona ni kama wanagongelea msumari katika Jeneza lao tarajiwa ili watakapotumbukizwa wazima wazima washindwe kufurukuta...Tunawashukuru sana Vilaza CCM kwa kutusaidia kuharakisha kifo chenu..KAMA KUMSUKUMA MLEVI VILE!!
   
 14. DOUGLAS SALLU

  DOUGLAS SALLU JF-Expert Member

  #14
  Jun 8, 2011
  Joined: Nov 13, 2009
  Messages: 11,659
  Likes Received: 4,755
  Trophy Points: 280
  Hivi mkuu unamjua Mfalme Daudi wa kwenye Biblia? Huyu alikuwa mpakwa mafuta na umaarufu wake ulianzia kwa kumuua Goliathi adui wa Israel? Inapobidi kuuwa basi ni ruksa kufanya hivyo. Hivi yale mabomu yanayomaliza watu kule Mbagala na Gongo la Mboto yalinunuliwa kama kalamu za kuandikia au kwa ajili ya kuuwa?
   
Loading...