Bila kubebwa Kikwete hawezi kushinda U-rais | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Bila kubebwa Kikwete hawezi kushinda U-rais

Discussion in 'Uchaguzi Tanzania' started by Kachanchabuseta, Jul 7, 2010.

 1. Kachanchabuseta

  Kachanchabuseta JF-Expert Member

  #1
  Jul 7, 2010
  Joined: Mar 8, 2010
  Messages: 7,290
  Likes Received: 11
  Trophy Points: 135
  [​IMG]

  Na M. M. Mwanakijiji -

  NAWEZA kusema kitu ambacho watu wengi tayari wanakijua au kukikubali bila haja ya kufanya jitihada kubwa ya kuwashawishi.

  Kwamba, bila ya kubebwa na vyombo vya dola na Chama Cha Mapinduzi (CCM), Rais Jakaya Kikwete asingekuwa na nafasi ya kusimama tena kama mgombea na kwa hakika asingeweza kuwa mgombea wa CCM katika uchaguzi mkuu ujao.

  Sasa hili linaweza lisikubalike na baadhi ya watu, lakini mtu yeyote ambaye ataliangalia kwa ukaribu kwa ushahidi mdogo tu nitakouweka hapa utaona kuwa jitihada kubwa imefanyika ya kuhakikisha kuwa Rais Kikwete haanguki, ndani ya CCM na kwenye uchaguzi mkuu.
  Kufanya jitihada kuwa Kikwete asidondoke ni jukumu la shabiki wake yeyote yule na ni sehemu ya fani ya siasa. Kumpigia kampeni Kikwete siyo kosa hata chembe na watu (wawe wana CCM au vinginevyo) kujitokeza kumuunga mkono si jambo baya kwa kipimo chochote kile. Tatizo pekee ambalo ninaliona ni pale haya yote yanapofanyika kwa gharama ya kufuta demokrasia ndani ya CCM na ndani ya Taifa.

  Ninachokiona sasa hivi (na nimekuwa mfuatiliaji wa siasa za Tanzania kwa muda mrefu tangu 1995) ni kuwa kuna jaribio la hatari la kumbeba Kikwete “kwa gharama yoyote ile”.
  Inapofikia kuwa Rais wa Jamhuri ya Muungano anapigiwa kampeni na mtoto wake ambaye tayari ameshagubikwa na wingu la kusababisha mvurugano kwenye Jumuiya ya Vijana basi ni lazima mtu mwenye kufikiri ajiulize ni nini kinachoendelea.

  Kwa sisi wachunguzi tunaweza kuangalia kwa ukaribu na kuona dalili mbaya huko mbeleni. Niwe wa kwanza kusema kuwa sitashangaa kama Ridhiwani Kikwete atakuwa mgombea Ubunge mwaka huu na hata kupewa unaibu waziri! Mnafikiri haiwezekani? Fumbueni macho mtashuhudia!

  Lakini kubebwa kunakofanyika naamini kuna hatari zaidi kwa CCM kuliko kitu kingine. Wakati kwenye Ubunge na Urais wa Zanzibar wana CCM wanaruhusiwa kugombea jimbo lolote bila kujali kama kuna mbunge wa zamani au la kwa sababu ni “demokrasia” na pale ambapo kuna wabunge wamedai kuna njama za kuwahujumu kwenye “majimbo yao” wamekuwa wakipuuziwa na likija suala la Urais mtazamo ni tofauti.

  Wakati wabunge wanakebehiwa kuwa “hakuna mtu mwenye hodhi ya jimbo” kwa Urais inaonekana Rais Kikwete ndiye mmiliki “halali wa Urais”.
  Tangu mwishoni mwa mwaka jana na labda mapema zaidi viongozi kadhaa wa CCM wamekuwa wakituimbisha wimbo wa “Kikwete awe mgombea pekee” wimbo ambao hivi majuzi watoto wetu huko Dodoma (wenye kuitwa “wasomi”) wameurudia pasipo kufikiria wimbo huu wa Kikwete awe mgombea pekee.

  Mwenyekiti wa CCM mwenyewe hajamkemea mtu yeyote ambaye amekuwa akirudia wimbo huu mambo ambayo yamekuwa yakifanywa hata mbele yake (kama ilivyotokea kule Tanga). Uongozi wa CCM hauoni tatizo kuimba wimbo huu usio wa kidemokrasia wa kumtaka Kikwete awe mgombea pekee.

  Sababu ya wao kufanya hivyo ni rahisi kufahamika. Kikwete angepewa ushindani huru ndani ya CCM asingeweza kushinda.
  Maneno kuwa Kikwete ni “mtaji” hayana ukweli wowote kwa sababu ni mtaji kwa kadiri ya kwamba ni “mtaji pekee”. Kama Kikwete angekuwa anakubalika ama kwa wananchi au ndani ya CCM angekuwa wa kwanza kutetea haki ya kushindanishwa akiamini kuwa rekodi yake inamtosha kumshinda mgombea mwingine yeyote.

  Kama Kikwete angeweza kuchujwa kama wanavyochujwa marais wa Marekani nina uhakika wa asilimia 100 Kikwete angedondoshwa kiurahisi tu au kupata changamoto kubwa ambayo ingemfanya anoleke vizuri.

  Lakini kwa sasa, CCM haiwezi kuweka mtindo kama huo kwa sababu wanaogopa asije akaumbuka.
  Hii haina maana kuwa Kikwete siyo mtu mzuri, na wala haina maana kwamba Kikwete hajafanya “lolote”. Maana yake ni kwamba kiungozi Kikwete ni dhaifu kuliko marais wengine wote waliowahi kuwepo na kama angepata mshindani katika mazingira huru kabisa Kikwete asingepita.

  Na yeye mwenyewe amesema kweli hivi karibuni alipodai kuwa kama angeboronga CCM wangemtosa. Tatizo ni kuwa hawawezi kumtosa wakati yeye ndiye Mwenyekiti wa CCM na Rais ambaye amezungukwa na kila aina ya ujiko utishao.
  Matokeo yake Kikwete anasemwa pembeni, anakebehiwa pembeni, anadharauliwa pembeni na wakati mwingine na baadhi ya watu wa karibu yake kabia au ambao wanaonekana wako karibu yake. Laiti mambo ambayo yanasemwa juu yake na watendaji walio chini yake yangepata kuandikwa, nina uhakika kuna kundi la watu wangetimuliwa bila hata ya kusikilizwa kama Obama alivyomtimua Jenerali McChrystal wiki iliyopita.
  Lakini kubebwa anabebwa. Hii ndiyo siri ya kupinga wagombea binafsi! Kikwete asingekuwa na nafasi kama haki ya Watanzania kugombea nafasi yoyote bila kufungwa minyororo ya kitumwa ya vyama vya siasa isingefutwa na Mahakama ya Rufani.

  Kikwete angeweza kutumia mbinu kukihujumu chama cha upinzani au kukiwekea mizengwe, kwa mgombea binafsi angefanya nini? Ndio maana hata mara moja hajawahi kutetea haki hii ya msingi ya wananchi kwa sababu ingeweza kumgeuka.

  Nina uhakika kabisa kuwa tunapoelekea uchaguzi mkuu na baada ya wagombea wengine wa Urais kujulikana, Kikwete hatofanya mdahalo nao. Kikwete hawezi kujadiliana na kujenga hoja huku anabanwa katika jukwaa huru kujieleza kwa sababu rekodi yake ni tata.
  Si kwa sababu siyo mtu mzuri, si kwamba si mcheshi au hana mvuto, la hasha. Kwa kila kipimo cha umaarufu na uzuri yawezekana Kikwete anaongoza katika vingi.
  Lakini katika uongozi wa siasa mvuto wake ni wa kulazimisha. Pasipo kubebwa na kutengenezewa mazingira ya kuwa mshindi pekee Kikwete asingeweza kushinda. Sijui kama anastahili ngwe nyingine au la, sijui kama angeweza kushinda ndani ya CCM au la, lakini historia itakuja kutoa hukumu kali ya jaribio baya kabisa la kuminya demokrasia ndani ya CCM.

  Sitoshangaa hawa hawa wenye kuimba wimbo wa “awe mgombea pekee” na yeye mwenyewe kubariki (kwa ukimya wao) ndio watakaosimama mwaka 2014 wakianza kuimba wimbo wa “aongezewe muda” na hivyo kuweza kubadilisha Katiba yetu na kuondoa ukomo wa urais. Nina uhakika watakuwepo na hawataogopa.
  Hawataogopa kwa sababu Mahakama Yetu ya Rufaa imekubali kuwa CCM inaweza kubadili Katiba na kuweka kipengele chochote hata chenye kufuta haki za wananchi kwa sababu tu wamefuata “utaratibu” unaokubalika.

  Watabadili Katiba na kuondoa ukomo wa urais kwa sababu wanaweza na watoto wetu hawa hawa wa vyuo vikuu watakuwa wa kwanza wakiongozwa na “mtoto wa kwanza” kuanza kupita na kukusanya maoni ya kuunga mkono.

  Demokrasia imevunjwa ndani ya CCM, na kwa sababu hiyo ni kanuni kubwa imevunjwa, basi kanuni hiyo itatafuta namna ya kutuvunja. Nyerere alionya juu ya kuvunja kanuni.

  Wameivunja kanuni
  Hawaulizwi kwanini
  Wameficha kama mbuni
  Vichwa vyao mchangani
  Atawazindua nani
  Demokrasia kutetea?

  Source: Mwanahalisi
   
 2. Mzee Mwanakijiji

  Mzee Mwanakijiji Platinum Member

  #2
  Jul 7, 2010
  Joined: Mar 10, 2006
  Messages: 31,360
  Likes Received: 6,377
  Trophy Points: 280
  duh.. nadhani hii ilitoka wiki iliyopita..
   
 3. pcman

  pcman JF-Expert Member

  #3
  Jul 7, 2010
  Joined: Oct 9, 2008
  Messages: 743
  Likes Received: 32
  Trophy Points: 45
  Ningekuwa JK ninge mpa kazi ya kunishauri MM
   
 4. Kiby

  Kiby JF-Expert Member

  #4
  Jul 7, 2010
  Joined: Nov 16, 2009
  Messages: 5,202
  Likes Received: 1,007
  Trophy Points: 280
  Hata hivyo JK ni kiongozi wa usanii ndani ya awamu hii ya nne. Sii ajabu baada ya kuhakikisha kuwa tayari amepitishwa kama mgombea pekee atakuja na gear ya kutetea demokrasia ya raia yeyote mwenye sifa kugombea nafasi yeyote. Na hilo atalifanya akijua halimhuyu yeye ila watakaokuja baada yake. Pia akisahau kwa kutojua au kwa kujua kwamba ameishainyumbisha mahakama kuu ya rufaa kwa kuilazimisha ijivue mamlaka ya kuwa na uwezo wa kusikiliza shauri lililo la kisiasa ndani ya nchi hii. Jambo ambalo lina madhara makubwa huko mbeleni.
   
 5. Hassani

  Hassani JF-Expert Member

  #5
  Jul 7, 2010
  Joined: Jun 5, 2009
  Messages: 267
  Likes Received: 35
  Trophy Points: 45
  Niko osifisini namuona jk anapita kwa mbwembwe ya mapikipiki akitokea sabasaba.Kwa hizi mbwembwe zote hizi huyu mzee wa pwani atafanya lolote kubakia madarakani,lakini bob(pamoja na bangi zake) alishawahi sema you can't make all people fool all the time
   
 6. M

  Msengapavi JF-Expert Member

  #6
  Jul 7, 2010
  Joined: Oct 23, 2008
  Messages: 4,802
  Likes Received: 2,748
  Trophy Points: 280
  JK ni msanii abaye anabebeka tu kwa sababu wanaombeba wanajua wasipofanya hivyo cha moto kitawajia. Zimwi litujualo linataka awamu ya pili lipate fursa ya kutumaliza nasi tunaliangalia tu! Maskini watanzania sisi! Mungu aepushie mbali ballaa linalotujia, la awamu ya pili ya JK!
   
 7. Kachanchabuseta

  Kachanchabuseta JF-Expert Member

  #7
  Jul 8, 2010
  Joined: Mar 8, 2010
  Messages: 7,290
  Likes Received: 11
  Trophy Points: 135
  Ndo mana sasa hivi wanakuwa nampigia magoti ili akifanikiwa nyundu isiwaangukie
   
 8. Mzee Mwanakijiji

  Mzee Mwanakijiji Platinum Member

  #8
  Jul 8, 2010
  Joined: Mar 10, 2006
  Messages: 31,360
  Likes Received: 6,377
  Trophy Points: 280

  hahahah unakumbuka yaliyomkuta Daudi alipopewa kuwa msaidizi wa Mfalme Sauli?
   
 9. M

  Mkandara Verified User

  #9
  Jul 8, 2010
  Joined: Mar 3, 2006
  Messages: 15,443
  Likes Received: 132
  Trophy Points: 160
  Mengi yatazungumzwa kuhusu Kikwete lakini ukweli utabakia kwamba tatizo sio yeye isipokuwa sisi ambao tunapenda sana kuzungumzia pembeni kwa mabaya yake lakini tunapokuwa karibu naye tunampa kila sifa - UNAFIKI mtupu.
  Ni unafiki wetu ndio ulomweka Kikwete kitini na hakika anajaribu kila la kheri kukidhi Unafiki unaombeba kwani ndio hulka ya Watanzania. Siku zote Utavuna ulichopanda, huwezi panda mahindi ukategemea kuvuna Mpunga...

  Ifike wakati jamani jitazameni sisi wenyewe..Tulipomchagua Kikwete tulitegemea kitu gani haswa?..Ni sifa zipi za Uongozi alizokuja nazo ambazo ni tofauti na Kikwete huyu tuliyenaye leo. Tumepanda Mahindi tumchuje kwa kufikiria mapishi ya mahindi na sio kudai Pilau na Biriani leo hali sisi wenyewe hatukupanda Mpunga.

  Tuache tabia hizi za Unafiki wakuu zangu. Maelezo yote hapo juu yanaonyesha wazi UNAFIKI wa Watanzania ambao hawana walijualo isipokuwa akili ya kitumwa inayoambatana na UNYENYEKEVU wa bwana - Mungu Mtu. Kila apitako JK anapigiwa makofi na vigelegele, akiwa Bungeni, akitembea ofisi za serikali hakuna mtu hata mmoja anayethubutu kuhoji Uogozi wake kwa machafu tunayoyasoma..

  Hivyo basi, tukubali kwamba Kikwete atapita uchaguzi pasipo kubebwa na mtu yeyote kwani sisi wenyewe ndio Wanafiki..Na hakika kuongoza wanafiki ni lazima uwe kama Kikwete!
   
 10. Nyunyu

  Nyunyu JF-Expert Member

  #10
  Jul 8, 2010
  Joined: Mar 9, 2009
  Messages: 4,370
  Likes Received: 130
  Trophy Points: 160
  Mkuu Mkandara,

  Haya yote ni kweli, lakini nahisi ndo maana tuko hapa. Kwamba tujitahidi kuongeza wigo wa kutafakari mambo haya tuondeokane na utumwa huu. Kumbuka hakuna atakayeweza kum-confront JK ndani ya "system" hii. CCM imeshindwa kutofautisha chama na serikali. (i always believe this is one Nyerere's failures). Lakini CCM ya leo ilipaswa kuacha failures za Nyerere's regime na kuja na mapya kuendana na wakati. Wangelichukua mazuri yote yake wakayaboresha na kusonga mbele. Shida kubwa ni kuwa wameendeleza nidhamu ya woga ndani na nje ya chama. Namuunga mkono kaka yangu MMKJ katika article yake, lakini matokeo ya hali iliyojengeka ndani ya chama!! It is disgusting when they say "utaratibu wa chama ni kumuachia amalizie kipindi chake" Hii inakera sana, ina maanisha hata kama ameboronga kama JK alivyofanya still anaachiwa. Well for JK, it appears serious, hawakutaka hata kumshindanisha ndani ya chama, kwani ni boga lililooza!!!!

  Laiti, wangekubali kutengeneza fair system tusingelikuwa hapa leo. Imeniudhi sana kusikia leo asubuhi JK anasema "raisi Da Silva wa Brazil na serikali yake wanafikiria kuisamehe TZ deni la USD 225milion, kwamba hili ni jambo la kushangilia!!!". Nikajifikiria hivi JK, anajisikiaje kuendelea kuruhusu serikali yake kuwakumbatia wafanya biashara wanaokwepa mabilioni ya ushuru kwa kuwa wanakifadhili chama!!! EPA, MEREMETA, DEEP GOLD, RICHMOND, RADA..... etc. Serikali inapoteza mabilioni ya USD yanaachiwa kuingia mifukoni kwa watu!!!!

  Huwa nafikia hatua ya kukubali yaliyotokea ROMANIA, GHANA,....etc. Yanayoendeles Africa!!! Watu wakichoka inakuwa hatari!!!:mad:
   
 11. Mzee Mwanakijiji

  Mzee Mwanakijiji Platinum Member

  #11
  Jul 8, 2010
  Joined: Mar 10, 2006
  Messages: 31,360
  Likes Received: 6,377
  Trophy Points: 280
  Mkandara.. unachosema ndio ukweli wenyewe bila sisi wananchi kumbeba asingeweza kubebeka!
   
 12. Anko Sam

  Anko Sam JF-Expert Member

  #12
  Jul 9, 2010
  Joined: Jun 30, 2010
  Messages: 3,216
  Likes Received: 17
  Trophy Points: 135
  Lazima abebwe na vyombo vya dola na tume ya uchaguzi-hakuna demokrasia. Angekuwa anategemea kura ndo zimfikishe Ikulu asinge kataa kura za wafanyakazi. Kumbuka CCM ina alama ya jembe na nyundo kwenye bendera yake, lakini akawatosa wafanyakazi. Ina maana ameshashinda kabla ya uchaguzi. Kampeni na Uchaguzi wake ni usanii mtupu-hakuna jipya!:israel::yield:
   
Loading...