Bila CUF Imara Chadema Hatutashinda 2015

ibange

JF-Expert Member
Dec 31, 2010
1,543
550
Kwa wale wanaochukulia mambo juujuu bila kuchambua kwa kina hawawezi kunielewa. Ni ukweli kwamba CCM ina wafuasi sana katika mikoa fulani hasa ya tambarare na Pwani na pia Unguja. Mikoa kama Lindi, Mtwara, dodoma vijijini, tanga, unguja nk ni vigumu sana chadema kushinda huko. Lakini pia maeneo haya ndio CUF ina wafuasi. Sasa ili chadema ishinde lazima CUF iwe na nguvu ili katika maeneo hayo wagawane na CCM angalao CUF 40% CCM 60%. Kupanuka kwa CUF si tishio kwa Chadema bali CCM hivyo kwa maoni yangu ni vizuri tuisaidie CUF irudishe hadhi yake ili wapambane na CCM katika maeneo ambayo ni no fly zone kwa chadema. Nimebahatika kutembelea baadhi ya maeneo haya na nilikuwa Tanga last week baadhi ya watu wanaiona Chadema kama chama cha wakristo na ni ngumu kuwabadili mawazo. CUF wanaweza kuwabadili tukapunguza mtaji wa ccm! Tutafakari
 
HAYA MTATIRO. SASA UNATAKA CHADEMA WAKUSAIDIEJE?

wawafuate wananchi na kuwaambia jiungeni na CUF?
 
Kazi waliyonyo chadema ni kuwaelimisha watanzania wote wajue malengo, madhumuni, nia thabiti na wajibu wa chadema katika harakati za kumkomboa mtanzania wa kawaida bila kujari mkoa atokako, dini yake wala jinsia. Kazi ya chama makini ni kuhakikisha kinaelimisha watu mpaka wanelewa na kukiunga mkono na sio kuegemea nguvu ya vyama vingine hasa vinavyo amini katika misingi ya dini na mikoa kadhaa. Pole Mtatiro kwani nguvu ya chadema kwa sasa haizuiliwi popote na kwa lolote.
 
kifo cha ccm na cuf ni sawa na kifo cha mme na mkewe,operation m4c tunamaliza kabsa
 
Ni ukweli kwamba CCM ina wafuasi sana katika mikoa fulani hasa ya tambarare na Pwani na pia Unguja. Mikoa kama Lindi, Mtwara, dodoma vijijini, tanga, unguja nk ni vigumu sana chadema kushinda huko. Lakini pia maeneo haya ndio CUF ina wafuasi. Sasa ili chadema ishinde lazima CUF iwe na nguvu ili katika maeneo hayo wagawane na CCM angalao CUF 40% CCM 60%.

Maitario a.k.a Mtatiro,
Analysis yako haina mashiko kabisa Mkuu. Mbona CHADEMA imeweza kuongoza kambi ya rasmi ya upinzani bungeni CUF ikiwa dhaifu? Pia assume majimbo yote ya TANGA, LINDI, MTWARA, PWANI, DODOMA na UNGUJA wanashinda CCM. Je ndio tiketi ya CCM kushinda Uchaguzi Mkuu 2015? CHADEMA tunauwezo wa kushinda uchaguzi 2015 bila hata ya kushinda jimbo moja mikoa hiyo. Kura za kushinda Urais zipo Kanda ya Ziwa (Mwanza, Shinyanga, Simiyu, Geita, Bukoba na Mara) na Nyanda za Juu Kusini (Iringa, Njombe, Mbeya, Ruvuma, Rukwa na Katavi).
 
Kazi waliyonyo chadema ni kuwaelimisha watanzania wote wajue malengo, madhumuni, nia thabiti na wajibu wa chadema katika harakati za kumkomboa mtanzania wa kawaida bila kujari mkoa atokako, dini yake wala jinsia. Kazi ya chama makini ni kuhakikisha kinaelimisha watu mpaka wanelewa na kukiunga mkono na sio kuegemea nguvu ya vyama vingine hasa vinavyo amini katika misingi ya dini na mikoa kadhaa. Pole Mtatiro kwani nguvu ya chadema kwa sasa haizuiliwi popote na kwa lolote.

We wasema usilojua au inawezekana umekaririshwa! Chadema wadini na kwa sera hii magogoni CDM itaenda kwa kuomba kuonana na rais tu! fullstop.
 
Mkuu haina haja ya kulumbana kuwa ccm cjui imeshikilia mikoa flani kwani ukweli wa mambo ni miaka mi3 ijayo ndo itadhirisha anguko la ccm mfano mzuri ni igunga ambapo 2010 CDM hawakusimamisha mgombea yeyote ila baada ya fisadi papa kujivua gamba kwakutotaka siasa uchwara CDM walisimamisha mtu ambae japo ccm walishinda kijasho kiliwatoka ni mpishano wa kura ulikuwa kidogo sana piga hesabu na ufikirie kwa kina utaona tu kadiri siku zinavyokwenda ndo ccm wanazidi kuangamia japo na mbinu chafu wanazotumia hakuna wanachoambulia kwa huu mwamko wa sasa
 
Maitario a.k.a Mtatiro,
Analysis yako haina mashiko kabisa Mkuu. Mbona CHADEMA imeweza kuongoza kambi ya rasmi ya upinzani bungeni CUF ikiwa dhaifu? Pia assume majimbo yote ya TANGA, LINDI, MTWARA, PWANI, DODOMA na UNGUJA wanashinda CCM. Je ndio tiketi ya CCM kushinda Uchaguzi Mkuu 2015? CHADEMA tunauwezo wa kushinda uchaguzi 2015 bila hata ya kushinda jimbo moja mikoa hiyo.

ikulu akupeleken nan?labda muandike barua ya kuonana na rais mkanywe chai na juice
 
Pole sana ndugu, kwa hiyo unataka cdm wakusaidie nn,ela au? Hivi arumeru kafu ilikuwepo vile?
 
Mwishowe mtasema bila CCM CHADEMA haiwezi kuchukua nchi...

Hivi kwa nini baadhi ya waafrika hasa watanzania ni wavivu wa kufikiria kwa kiwango hiki?, mara bila CUF, ohhh Bila Zito, mara hili lile nyinyi wote lengo lenu moja tu.

Mnataka CCM iendelee kubakia madarakani hakuna jipya...

Kwa mwana mapinduzi yeyote anatakiwa kuelewa Arumeru tulikuwa wenyewe? mbona Uzini tulikuwa wenyewe, Mbona Karatu huu mwaka wa 12 tuko wenyewe..

Naomba thread hii ieleweke kama wanaiogopa sana CCM na sisi tushatoka huko.
 
Ni ukweli usiopingika kuwa fikra za udini ndizo zinazochelewesha ustawi wa siasa makini na demokrasia katika nchi yetu hasa ukizingatia wengi wetu elimu zetu ni za kujua kusoma na kuandika!Hili linachochewa pia na baadhi ya viongozi wa dini either kwa upeo wao mdogo au kwa makusudi simply kwakuwa wanachuki dhidi ya dini fulani (HILI LIPO PANDE ZOTE SI WAISLAMU WALA SI WAKRISTO mimi binafsi ni shahidi juu ya hili)!

Siasa za Tanzania zitaendelea kuwa za maeneo fulani hasa kulingana na waumini wa dini fulani kwa eneo husika na hili linaweza lisiangalie chama bali ni mtu husika mathalani Mh Zitto Kabwe alikiri hadharani kukumbana na changamoto toka kwa wakristo katika jimbo lake regardless kwamba chama chake kinatafsiriwa na watu baadhi kuwa ni cha kikristo!!Haya yote yanachochewa na chama tawala lakini hawajui madhara yake,ni kweli wanaweza kuwa watawala wa kudumu tz kwa kujengea vyama vya upinzani hoja za kuwa ni wadini lakini wakatengezeza matabaka baina ya wananchi wao mbaya zaidi kikinuka hapo nchi haitatawalika tena!!!
 
Kwa wale wanaochukulia mambo juujuu bila kuchambua kwa kina hawawezi kunielewa. Ni ukweli kwamba CCM ina wafuasi sana katika mikoa fulani hasa ya tambarare na Pwani na pia Unguja. Mikoa kama Lindi, Mtwara, dodoma vijijini, tanga, unguja nk ni vigumu sana chadema kushinda huko. Lakini pia maeneo haya ndio CUF ina wafuasi. Sasa ili chadema ishinde lazima CUF iwe na nguvu ili katika maeneo hayo wagawane na CCM angalao CUF 40% CCM 60%. Kupanuka kwa CUF si tishio kwa Chadema bali CCM hivyo kwa maoni yangu ni vizuri tuisaidie CUF irudishe hadhi yake ili wapambane na CCM katika maeneo ambayo ni no fly zone kwa chadema. Nimebahatika kutembelea baadhi ya maeneo haya na nilikuwa Tanga last week baadhi ya watu wanaiona Chadema kama chama cha wakristo na ni ngumu kuwabadili mawazo. CUF wanaweza kuwabadili tukapunguza mtaji wa ccm! Tutafakari
Nadhani wewe mwenyewe ndiye uliyelichukulia jambo hili juujuu. Chama cha saisa hakiwezi kuwa chenye nguvu iwapo kinategemea nguvu hizo kutoka katika chama kingine cha siasa. Ukiona unaanza kutafuta ushindiw a kimahesabu namna hivyo, basi fahamu kuwa chama chako si imara na hakina nguvu. Chama chenye nguvu kinasimama chneywe na kushinda hata kama kutakuwa na vyama vingine, kama ilivyotokea Arumeru Mashariki na sehemu nyingine.
 
ikulu akupeleken nan?labda muandike barua ya kuonana na rais mkanywe chai na juice

Haya. Sisi huwa hatupendi ubishi. Ni watu wa vitendo. Kumbuka kauli zenu za Arumeru na kilichotokea!
 
Kwa fikra hizi ukombozi wa nchi kwa mapinduzi ya kifikra umeshindwa, nahisi tutafute ukombozi kwa njia ya mtutu
 
HAYA MTATIRO. SASA UNATAKA CHADEMA WAKUSAIDIEJE?

wawafuate wananchi na kuwaambia jiungeni na CUF?

we omba tu ccm wasimamishe mkristo kwani wale wote wanaoishabikia sababu ya udini walioujaza watahama na kutafuta aliko muislamu mwenzao.
 
Back
Top Bottom