Bila CUF Imara Chadema Hatutashinda 2015

Bila CUF Imara Chadema Hatutashinda 2015

Naona huu wimbo wa UDINI....UDUNI....umeendelea kushika kasi .....tena naona kasi yake inazidi kuwa kubwa ziadi. CDM kinasemekana kuwa ni cha kikristo....CUF kinaonekana kuwa ni cha kiislamu....sijasikia TLP, NCCR, TADEA, UDP n.k. Lakini kikubwa sijasikia CCM ni chama cha mlengo gani....au chenyewe ndio hakina dini.....halafu kibaya zaidi aliyeanzisha wimbo wa UDINI ni KIKWETE....sasa mbona tunasahau kusema CCM ni chama cha dini gani....???

Baada ya kuona kuwa mtaji wa Kasi zaidi, Ari zaidi and Nguvu zaidi haimpi ushindi, Kikwete aliasisi UDINI ili kukinyima kura Chadema na Cuf. Mtu anayesema wenzake ni wadini, yeye ndiye MDINI MKUU, ndiyo maana amekuwa na upeo mkubwa wa kuwatambua wengine kuwa ni WADINI. Kwa maana nyingine kubwa na inayoeleweka, KIKWETE ndiyo MDINI KUU. Kama JK ni mdini, CCM inajinusuru vipi na udini? Na tunasemaje kama mwenyekiti wa chama ni mdini, tena MUISLAMU, Tunapata utata gani kusema kuwa CCM ni chama cha KIISLAMU? Au tuanze kuchambua team yake ya kampeni mwaka 2010? au tuanze kuangalia watu wa dini yake aliowapa madaraka kwa dini yake? au tuhesabu wakuu wa mikoa na wilaya, makatibu wa ccm mkoa na wilaya, wakurugenzi wa majiji, halmashari za mji na wilaya na vingine vingi? Si vema kuyafanya yote haya kwa sababu siku yakitokea ya kutokea, tutaathirika wote kwa kiwango sawa, hakutakuwa na mwanaCCM wala CUF au hata mwana CHADEMA ambaye atabaki salama, dhambi hii ya ubaguzi itatutafuna sote.

NINI FUFANYE......
Kikwete na CCM yake watapita....Mbowe na CDM yake watapita.....Lipumba na CUF watapita.....NCCR na mbatia itapita....TLP na Mrema watapita....LAKINI TANZANIA NA WATANZANIA wataendelea kuwepo hadi Mungu atakaposema ni mwisho wa kila kitu hapa duniani. Kufikiri mambo ya siasa kwa mtazamo wa dini fulani, ni kuishia kisera na maono ya kuongoza nchi...nafikiri wote mnaona CCM ilipotufikisha na Kikwete wake na udini anaousema. Nafikiri mnaona sera za CCM ya leo, juzi tumezisikia ARUMERU, hapo ndipo CCM ilipofika. Kuendelea na chama hiki kikiwa na viongozi aina ya akina Sitta, Lowasa, Vuai Nohodha, Hussein Mwinyi, Bernard Membe, Mwakyembe, na wengine wengi kutoka CCM mwaka 2015 ni kuliangamiza Taifa na kuzidi kuutambulisha UMBUMBUMBU WETU KTK anga za KIMATAIFA NA MAJIRANI ZETU. Wote tunanunua katika maduka yale yale, wote watoto wetu wanasoma Saint Kayumba, wote tunaishi nyumba zinazofanana, kifupi wote tunaishi maisha yanayofanana, ukiwatoa wachache ambao wanafaidi keki ya Taifa....sasa mtu maskini kama mimi anapata wapi ujasiri wa kushabikia CCM ilihali yote haya yamesababishwa na CCM?

TAIFA hil litajengwa na watanzania wote bila kujali itikadi zetu za dini na vyama. Tusipounganisha nguvu zetu kama watanzania, tutaendelea kuyasikia maendeleo kwenye nchi za wenzetu....Kama chama Tawala bado kinatoa ahadi hadi leo....maana yake hakuna ambacho wamefanya miaka yote ya uhuru....maana ya ahadi ni kupanga kufanya katika wakati ujao...CCM bado wanaahidi maji, bado wanaahidi umeme, bado waaahidi maisha bora, sasa wamefanya nini miaka yote ya uhuru....?
Kazi kweli, ndiyo maana wengine TUNAVUMILIA KUWA WATANZANIA na kamwe HATUJIVUNII KUWA WATANZNIA. Utajivunia nini katika nchi ya tatu kwa kukopa duniani ilihali kila siku wazungu wanaondoka na tani nyingi za dhahabu, almasi, gesi, magogo na sasa hadi wanyama.....KWELI KUSHABIKIA CCM LAZIME UWE NA MTINDIO WA UBONGO...






 
Kwa wale wanaochukulia mambo juujuu bila kuchambua kwa kina hawawezi kunielewa. Ni ukweli kwamaba CCM ina wafuasi sana katika mikoa fulani hasa ya tambarare na Pwani na pia Unguja. Mikoa kama Lindi, Mtwara, dodoma vijijini, tanga, unguja nk ni vigumu sana chadema kushinda huko. Lakini pia maeneo haya ndio CUF ina wafuasi. Sasa ili chadema ishinde lazima CUF iwe na nguvu ili katika maeneo hayo wagawane na CCM angalao CUF 40% CCM 60%. Kupanuka kwa CUF si tishio kwa Chadema bali CCM hivyo kwa maoni yangu ni vizuri tuisaidie CUF irudishe hadhi yake ili wapambane na CCM katika maeneo ambayo ni no fly zone kwa chadema. Nimebahatika kutembelea baadhi ya maeneo haya na nilikuwa Tanga last week baadhi ya watu wanaiona Chadema kama chama cha wakristo na ni ngumu kuwabadili mawazo. CUF wanaweza kuwabadili tukapunguza mtaji wa ccm! Tutafakari

Mkuu mtatiro, tatizo kubwa nnaloliona ndani ya kafu, mnatanguliza ubaguzi kama sera namba moja ili kufikia malengo yenu. Kwanini nasema hivi, mlianza kwa kufikiri mkiwapata waislamu wote wa Tz mtakuwa mmewin, mambo hayakwenda kama mlivyo tarajia. Mkajaribu ndoa na ccm ndani hakukukalika, ukatokea mpasuko mkubwa na hatimaye mnaelekea kaburin. Sasa mna taka chadema iwaimarishe ili mgawane kura na CCM, HILI NA SEMA NO,NO,NO. Nyie kufeni tu, ccm tutapambana nayo wenyewe, hadi sasa matokeo yanatarajiwa kuwa mazuri tu. Mbona Arumeru hamkuwepo lakini mabwana zenu walichambia *****!
 
Kwa taarifa yako mambo ya udini na ubaguzi wa rangi (uarabu) kwa kiwango kikubwa yamekuwa yakienezwa na CCM kuanzia enzi za Mkapa. Hii ilitokana na CCM kuiogopa CUF kuwa ingeshinda Zanzibar ambako ilionekana kuwa na nguvu kubwa kisiasa. Wakati huo CUF ilisingiziwa kueneza uislam na hata leo wafuasi wengi wa CUF ni waislam.

Ndani ya CCM kwenyewe Salim A. Salim alienguliwa kugombea urais kwa kuwa asili yake ni mwarabu!

Dr. Slaa alipoamua kugombea urais kupitia CHADEMA na kuonekana anaungwa mkono na wananchi wengi Kikwete na CCM yake waliamua kumpachika udini kwamba akishinda ataeneza ukatoliki kwa kuwa kabla ya kujiunga na mabo ya siasa alikuwa padre! Hivyo CHADEMA ikasingiziwa kuwa ni chama cha katoliki.

Uzushi wote huu umeanza kupuuzwa na wananchi na hasa vijana. Wazee wachache pia wamegudua kuwa hii ni propaganda ya CCM na kuanza kuwapuuza. Bila shaka watabaki watu wachache wenye fikra mgando ambao wataendelea kuukubali uzushi huu wa CCM.

Hivyo ni wajibu wa CHADEMA na CUF kui-prove wrong CCM kwa hoja na matendo ili vyama hivi viendelee kuaminika wakati CCM ikiendelea kujizika!
 
CUF inashika dola bila hata kutegemea chadema; kinachotakiwa ni tume huru na kusimamia kura period..

CUF haiwahitaji chadema kwasababu wameonyesha ubaguzi na dharau kwa CUF na upinzani wote kwa ujumla..

Mtakumbuka wakati CUF ilipokuwa chama kikuu cha upinzani kiliunganisha nguvu ya upinzani lakini baada ya chadema kupata nafasi hiyo tuliambulia matusi..

CUF must stands themselves and they can do better than any political party in Tanzania..

Kinachotakiwa ni ki-organize upya ikiwa ni pamoja na kuwaondoa na kuwastaafisha baashi ya wazee kwenye chama..
 
Udini,ukanda unaletwa na ccm nazani mme msikia Mkama alivyosema sasa hivi urais zamu ya nyanda za juu kusini.
 
ukiwaona watu wanashabikia udini muwaogope kama ukoma. mimi kwetu Mtwara hili tatizo lipo japo silipendi hata kulisikia na ccm wanalifanya kwa makusudi ili waendelee kutudumaza.hivi dini zetu zinatuletea nini zaidi ya kiroho? na wala si huu ufisadi na majizi na ukandamizaji kwa wenye haki.
 
Back
Top Bottom