Bila CCM madhubuti upinzani imara nchi yetu itayumba...

Chama cha mapinduzi=KIDUMU!
Nadhani kwa sasa kinakaribia kuanza kuhifadhia mbege na ugoro!
 
rafiki yangu masopakyindi...
going forward, washauri ccm wenzio kuwa si vibaya wakiendelea kutumia majina dizaini ya id yako, lakini wakipata uongozi wakome ku-practise hicho id yako inachokisema!
 
Kidumu Chama Cha Mapinduzi. Nambari 1 kitaendelea kuwa Nambari 1 milele.

Ulidanganywa ukakaririshwa!,pole kijana.Wenzio hawapo kwenye hzo fikra ona akina nape wako magamba mwili tu but fikra na mawazo yote yako chadema.Kidumu ili iweje?.Hakuna chama au dola duniani iliyodumu milele hata moja unjidanyanya tu.Ccm hamna chenu na hamna jipya kwa watz na tena shule za kata ndo zitakazowang'oa 2015 kiulainii!,mtaji na muda wenu umekwsha na kama mnadhani kuwa mtatawala milele hamjui kusoma alama za nyakati na tena mnakuja kufilisiwa milele ninyi magamba,watoto wenu pamoja na wajukuu zenu.Kazi mnayo.
 
Jamani hii kauli ilikwisha potea zamani sana,sasa hivi wanapenda kusema ccm oyee! Naomba mufuatilie hili. Hawa jamaa kwisha,na wao wanajua vema hilo,ila tu kama inavyotuonyesha historia kuwa wenye kushika madaraka hawakubali kuachia kilahisi hivyo wanajitahidi kuwa wabishi.lakini ninaona muda unawatupa mkono kwa kasi kubwa. To be continued..
 
rafiki yangu masopakyindi...
going forward, washauri ccm wenzio kuwa si vibaya wakiendelea kutumia majina dizaini ya id yako, lakini wakipata uongozi wakome ku-practise hicho id yako inachokisema!
Thanks M-mbabe,mimi ni mnazi tu wa CCM katokana na historia yangu. Sipendezwi na mengi ndani ya CCM lakini zamani falsafa ya chama ni moto wa kuotea mbali.

Mi si kiongozi wala sigombei popote,lakini fuatilia kwa makini falsafa,sera na itikadi ya CCM Leo na utagundua kuwa hata msemo wa Kidumu chama cha Mapinduzi ni wa zamani sana na si dole Tupu la miaka ya karibuni.

Chombo kikienda mrama huzamishi chombo, unabadilisha muelekeo sawa Sawa na upepo unao vuma.
Hili ndio Somo CCM inbidi izingatie
 
Maumivu ya kichwa uanza pole pole. Jipeni matumaini na mtajutia kuanzisha shule za kata, ndizo zinaongeza wafuasi wa CDM

Hii kweli mtu wangu, mwezi wa sita narudi shule rasmi, nakumbuka mwaka 2010 niliongeza wapiga kura zaidi ya mia tatu wa CDM shuleni kwangu, sasa hii ya kuanzia 2012 hadi 2015, nitaongeza zaidi ya elfu kumi shuleni na kitaaa we acha tu, kama kipindi ni dakika themanini, arobaini kontenti ya kwenye silabasi, arobaini kontenti negatively ya ccm na kontenti positively ya CDM, hadi kieleweke, watajuta kuleta shule za sekondari kila mtaa.
 
IT`S TRUE! ''Mpaka sasa kuna watu wanatakiwa kutoka porini waje barabarani'' Hii haiitaji tution lakini kama tutaona kuna umuhimu itatumika. wamefanywa watumwa wa kifikra, Hawataki badirika wala kusikia harufu ya mabadiliko. Hawa ni baadhi ya watu wanaoishi kwa mazoea kama walivyo zoeshwa na chama chao cha kijani lakini siku zinapo zidi kusogea ''Hii kijani inazidi kuwa nyeusi (giza)" tuachane na sera za chama cha ''DUMU DUMU!'' na ili tufike tuendako wa Tanzania ni lazima tuanze upya! CHADEMA walikwisha ianza safari Tuwaunge mkono na harakati hizi ziendelee mpaka-2015.
 
Kwanini ujipe matumaini wakati hali unaoina
Ndugu yangu, kinacho nipa moyo ni ushindi wa Chadema umeweza kusema maneno mengi ya kukionya chama cha mapinduzi, ukilinganisha na kupuuzwa kwa ushauri uliokuwa unatolewa na wananchama wake kuwa CCM inakoelekea siko.

Ni jambo la kiungwana kuishukuru CDM kwa kuifundisha CCM katika yale ambayo imeonywa na imekaidi kusikiliza.
 
Ndugu yangu, kinacho nipa moyo ni ushindi wa Chadema umeweza kusema maneno mengi ya kukionya chama cha mapinduzi, ukilinganisha na kupuuzwa kwa ushauri uliokuwa unatolewa na wananchama wake kuwa CCM inakoelekea siko.

Ni jambo la kiungwana kuishukuru CDM kwa kuifundisha CCM katika yale ambayo imeonywa na imekaidi kusikiliza.

Mkuu nina uhakika ww u mwenzetu.. Sema umeanzisha hii thread ili ufurahie CCM kupondwa.. Maana magamba wote wameingia mitini toka washindwe.. Kumepwaya mno kwa kukosa upande wa pili..
 
Mkuu nina uhakika ww u mwenzetu.. Sema umeanzisha hii thread ili ufurahie CCM kupondwa.. Maana magamba wote wameingia mitini toka washindwe.. Kumepwaya mno kwa kukosa upande wa pili..
Mkuu mimi ni gambaz pyua!!!
Tena kadi yangu ni namba.......(wacha nisitaje kwa leo)
CDM si maadui zangu, ni watani zangu. Mtani wetu CUF tulimmaliza kitambo na kingi tumekula, bado CDM.

Hata hivyo vinara wetu tumeandika wee kwa uchungu ili wajisahihishe lakini imekuwa wapi!
Wakasema magamba wanayavua, ikawa kiini macho.
Magamba bado yapo na yanapeta na sisi tunaona.
Tumelia na rada, EPA,Kagoda na maskandali mengi ili watu wachukuliwe hatua feza irudi, sasa imekuwa wimbo uliochusha.

Sasa kanakuja kajamaa kanaitwa Chadema, kanafyeka miguu ya sapoti tunayosimamia,wananchi(wenyewe nasikia wanaita pipoz) hapo naona tuta amka.
CCM tusipoamka safari hii, kuondoa migongano ya viongozi, kujenga umoja na kuwaondoa wale wenye negative influence,
basi sijui tutegemee nini.
Lakini mimi nina matumaini bado ndio maana nasema:
KIDUMU CHAMA CHA MAPINDUZI!
Walioingia mitini hao ni tawi la vijana, si makada hao.
 
Back
Top Bottom