Bila CCM Kunyang'anywa Viwanja, Michezo Itazidi Kufa

Chakaza

JF-Expert Member
Mar 10, 2007
40,319
72,748
Nchi hii inavyo viwanja vingi vya michezo vilivyo jengwa na wananchi kwa nguvu na fedha zao lakini viliporwa na kumilikishwa kwa CCM kiujanja ujanja.

Viwanja hivyo ni pamoja na Kirumba, Jamhuri, Mkwakwani, Maji maji, Ali H. Mwinyi nk nk karibu kila mkoa.

CCM haivitunzi na kuviendekeza hivyo kudumaza michezo. Sasa hivi hata ligi kuu ambayo ndio inatoa Timu ya taifa iko kiwango cha chini kutokana na ubovu wa viwanja hivyo jee tutapataje timu bora kwa hali hiyo?

Nini kifanyike kisheria kuinyang'anya CCM viwanja hivyo ili virudi kwa wenyewe wananchi chini ya Halnashauri zao?
 
Hakuna kitu ccm wanaweza, kinachotakiwa ni wananchi tuamue kuitoa madarakani kwa njia zinazofaa
 
Hakuna kitu ccm wanaweza, kinachotakiwa ni wananchi tuamue kuitoa madarakani kwa njia zinazofaa
 
Kama hao mnawaona wanafaa kuongoza nchi wanadaiwa kodi kidogo tu ya pango la ofisi je ukiwapa kiwanja name nchi wataweza suala la kiwanja inausiano gani na timu ya taifa kufanyavibaya kwanI ccm wanacheza
 
kuna siku wabunge wa ccm waliingiza magari yao ya kifahari uwanja wa jamhuri dodoma ili yaoshwe, na wakayaoshea humohumo uwanjani kwenye pichi

juzi silaha haramu zimechomewa uwanja wa lake tanganyika kigoma...seriously
uwanja wa mpira na michezo mingine unatumika kama furnace

halafu mnataka eti tushiriki AFCON, au eti tuandae...seriously
 
Kama hao mnawaona wanafaa kuongoza nchi wanadaiwa kodi kidogo tu ya pango la ofisi je ukiwapa kiwanja name nchi wataweza suala la kiwanja inausiano gani na timu ya taifa kufanyavibaya kwanI ccm wanacheza
Hujitambui, wachezaji wanaocheza kwenye viwanja vibovu kiwango chao kinaweza kupanda na kufikia cha wenzetu wenye viwanja vizuri? Na kwa nini wakomae na viwanja sio vyao?
 
Naungana nawe mkuu chakaza, viwanja vinatakiwa virudishwe kwenye halmashauri za wilaya,miji na majiji ili viweze kuhudumjwa vizuri
 
Naungana nawe mkuu chakaza, viwanja vinatakiwa virudishwe kwenye halmashauri za wilaya,miji na majiji ili viweze kuhudumjwa vizuri
Ndio maana nauliza tufanyeje? Jee ifunguliwe kesi ya aina gani na nani mshtaki na mshtakiwa?
 
Kama hao mnawaona wanafaa kuongoza nchi wanadaiwa kodi kidogo tu ya pango la ofisi je ukiwapa kiwanja name nchi wataweza suala la kiwanja inausiano gani na timu ya taifa kufanyavibaya kwanI ccm wanacheza

Mbona umetoka nje ya mada?
 
Back
Top Bottom