RuvulyDeFinisher
New Member
- Sep 4, 2019
- 2
- 3
__ BIKRA YANGU __
____ Sehemu ya Kwanza __
[emoji117] Tunaanza
Jina langu naitwa LIDYA nina miaka 17 ni mtoto wa mwisho wa kike katika familia ya mzee MUSSA, baba yangu ni HAKIMU na mama yangu ni MWALIMU mkuu katika shule ya GONGA, Mimi ni mwanafunzi wa chuo mwaka wa kwanza. Juzi majira ya saa mbili usiku nikiwa na marafiki zangu , HUSNA na MARY tulitoka chuo tukiwa tunakwenda kununua chakula cha usiku, Kutokana na umbali uliokuwepo kutoka chuo hadi sehemu wanapouzia chakula ilitugharimu kutumia muda mrefu kutembea barabarani. Kwa bahati nzuri mungu alitusaidia tukafika salama sehemu hiyo , Muuza chakula akatupatia chakula tulichokuwa tunahitaji wakati tunataka kuondoka kurudi chuo, Muuza chakula akatuambia hivi :
MUUZA [emoji117] Samahani dada zangu ninyi mnatoka wapi majira ya usiku kama huu alafu ni wasichana hamuogopi ?
Mimi na rafiki zangu tulipata mshangao kiasi rafiki yangu MARY akamuuliza Muuza chakula :
MARY [emoji117] Sisi ni wanafunzi wa chuo hicho karibu sio mbali sana na hapa kwako kwani kuna shida gani kaka ?
MUUZA [emoji117] Duuh inamaana ninyi hamjui chochote kuhusu mazingira ya karibu na chuo chenu ?
MARY [emoji117] Hapana sisi wageni leo hii tumefikisha mwezi mmoja katika chuo hicho kunanini kwani kaka yangu ?
MUUZA [emoji117] Dada zangu kwanza poleni sana, wanafunzi wa chuo hicho hawatakiwi kutoka usiku kama huu kwa sababu kuna mambo ya ajabu sana maeneo ya chuo chenu hususa kwa mabinti bikra, Maeneo haya kuna Ushirikina wa hali ya juu na kila siku mabinti bikra wanapotea na hatujui wanapelekwa wapi kwahiyo kama kuna bikra kati yenu mmmh sijui niseme nini lakini mungu awasaidie mrudi salama chuoni tena msipoteze muda rudini chuo sasa hivi sawa .
MARY [emoji117] Mungu wangu mbona unatutisha kaka yangu .
MUUZA [emoji117] Siwatishi nimewasaidia dada zangu hapa nimetoa uhai wangu kwa kuwasaidia ninyi, kwa kuwapa siri hii naomba kama mkifika salama chuo kesho msikose katika mazishi yangu ondokeni haraka na msigeuke nyuma hata mkisikia chochote yeyote ataegeuka nyuma atapoteza maisha yake .
Baada ya kusikia hivyo Mimi pamoja na wenzangu tuliondoka tukiwa na hofu kubwa sana iliyotanda mioyo yetu , Husna alikuwa analia sana kwa woga, tulitembea kwa kasi sana ili tufike chuo haraka, kipindi tunatembea ghafla tulisikia sauti ya muuza chakula ikituomba msaada, Nilisimama alafu......
_________ ITAENDELEA___________
#SHARE na wengine waisome hii
#LIKE_PAGE kwa mwendelezo wa simulizi hii na nyingine zaidi [emoji116][emoji116][emoji116][emoji116][emoji116][emoji116][emoji116]
https://www.facebook.com/RuvulyDeFinisher/