USSR
JF-Expert Member
- Jul 15, 2015
- 11,718
- 27,812
BIHARAMULO KITOVU CHA KAMPENI ZA CCM KAGERA
Hapa Balozi Dkt Emanueli John Nchimbi anasubiliwa kwa hamu kubwa
Biharamulo ndio kitakuwa kituo kikuu cha kampeni cha Chama Cha Mapinduzi katika kampeni za mgombea mwenza wa urais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Balozi Dkt. Emanueli John Nchimbi, kwa Mkoa mzima wa Kagera.
Ni hapa Biharamulo ambapo Ilani ya utekelezaji wa miradi ya kimkoa itajadiliwa, na sauti ya wananchi kusikika moja kwa moja mbele ya mtu atakayekuja kuwa Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania iwapo CCM itashinda uchaguzi wa mwaka 2025–2030.
Kwa ukubwa wa kijiografia na wingi wa watu kulingana na Sensa ya Taifa ya mwaka 2022, Biharamulo imekuwa kiungo muhimu cha maendeleo ya Kagera. Aidha, Mkoa huu umeweka historia kwa kuwapitisha wabunge watatu bila kupingwa:
Innocent Bashungwa,
Dotto Bahemu,
Eng. Ezra John Chiwelesa, ambaye pia ni mwenyeji wa Biharamulo.
Kama ilivyokuwa katika ziara ya kikazi ya Mheshimiwa Rais Samia Suluhu Hassan, alipoitumia Biharamulo kama mlango wa kuingilia Mkoa wa Kagera, ndivyo ilivyo sasa kwa Balozi Dkt. Emanueli John Nchimbi. Safari yake kuelekea Kagera itaanza kwa kupokelewa na wananchi wa Nyakanazi, kisha kuingia Biharamulo Mjini kwa mkutano mkuu wa kampeni utakaobeba hamasa kubwa na matarajio ya wananchi wa Kagera.
Biharamulo, kwa mara nyingine tena, linathibitisha nafasi yake kama kitovu cha siasa, maendeleo na mshikamano wa wananchi wa Mkoa wa Kagera.