- Hapa sawa sawa, tupo pamoja.
- Inawezekana maana yake hata wewe huna uhakika na unachosema, au?
- Ndiyo hasa tunachosubiri sasa hivi maelezo kamili toka kwake na CCM, sasa hivi nimemaliza kuongea na Lunyungu, inaonekana CCM na Oscar wana kila sababu ya kujibu hili swali.
Respect.
FMEs!
Sawa FME lakini tunasubili maelezo ya kwanini alibadili jina na uthibitisho kwamba ni raia wa Tz. hatusubili maelezo ya kama alivo eleza Lunyungu kwamba mkulu alimuita Ikulu kumshawishi saa nzima hivyo anabaraka zake, as if, baraka za mkuu ndo zinathibitisha uraia wa Mukasa aliye batizwa upya jina la Rwegasira!
Mkuu, imeshasemwa kuwa hajabadili jina, isipokuwa ameongeza la katikati ambalo alokuwa halitumii. Mchezo umekwisha, tusubiri kampeni na ushindi wa kishindoKwa hiyo swali la kujiuliza kwanini amebadilisha jina mara baada ya kuteuliwa kuwa mgombea wa CCM? Ana umri wa miaka 39 sasa, kwanini hakubadilisha alipokuwa O-Level, A-Level ama Mlimani au wakati akifanya graduate program?
Kwa upande wangu sijui lolote kuhusu Oscar zaidi ya kinachosemwa. Kabla ya kusikia juu ya pingamizi la Chadema jina la Mukasa tu lilinidokeza kwa namna fulani kuwa huyo ndugu ana uhusiano na Uganda. Siikuwa na matatizo ya uraia wake kwani Mtu wa Uganda anaweza kuhamia Tanzania na akawa raia wa Tanzania.
Kama vile watu waliotoka Nyasa na wako Tanzania na ambao majina yao tunayajua ni ya Kichewa kina (Banda, n.k) na wapo ambao wametoka Uarabuni au asili yao ni uarabuni na ukakuta majina yao mengi tu Zenji, Dar, Tanga n.k So, kuwa na jina la "Mukasa" siyo sababu ya kusema si raia wala sababu ya kushuku kuwa si raia.
Tatizo:
a. Kwamba kulikuwa na mjadala wa jina la "Mukasa" kunamfanya mtu aulize "kwanini" ukizingatia hayo niliyoyasema hapo juu. CCM au Oscar mwenyewe hakuwa na sababu yoyote ya kukana jina lake isipokuwa kama hakutaka watu wahusishe na "kitu fulani" yaani Uganda.
b. W/alipoamua kutumia jina la Rwegasira ambalo kwa Watanzania wengine linawakubusha ya kina "Paul Rwegasira" na wahaya waliowazoea Oscar amefanywa awe na jina la "kitanzania", it begs the question "why"? Ukifirikia sana hakuna jina la Kitanzania per se, kwani "Patel, Dewji, Nyoni/Nyuni, Simba, Tembo, n.k" ni majina ambayo unaweza kuyakuta nchi nyingine vile vile lakini yanatumiwa na watanzania. Kwanini hili la Oscar libadilishwe? Isipokuwa pale penye ishara ya matatizo?
Ninaamini waliovurunda hili siyo Chadema kwa kuchallenge uraia wa Oscar bali CCM kwa kuufanya uwe issue. Kama Chadema wana info zile zile ambazo CCM ziliwafanya waone kutumia "Mukasa" ni kukaribisha udadisi usio wa lazima kwanini wasihoji?
Hivyo utaona kuwa kama Oscar yuko (na inaonekeana hivyo) comfortable na jina lake kama Mtanzania na hakuna chochote cha kuficha asione haya aseme "Kutumia jina langu la Rwegasira naona kumezua maneno mengi, na nimeamua kutumia jina langu la kawaida la Mukasa, kwani mimi ni Mtanzania na sina hofu na asili yangu". Na kuanzia hapo hayo ya Rwegasira wayarudishe huko huko kwenye vikao vyao na Oscar aendelee kuwa Oscar Mukasa kama anavyo/alivyo fahamika kwa wengi.
Inasikitisha kuwa CCM kwa kuamua kumbadili Oscar Mukasa kuwa Oscar Rwegasira wamekaribisha wenyewe utafiti katika maisha ya kijana huyu na hivyo kututoa kwenye kuangalia ni nani anafaa kuwa mbunge wa Biharamulo.
Hata hivyo, kama kuna sababu ya msingi ya kuhoji uraia wake (kama ilivyodokezwa na CCM katika kubadilisha majina) ni haki ya kila Mtanzania kuona sheria inafuatwa. Kama tumeweza kuhoji uraia wa Rostam tuweze kutumia hilo hilo katika kuhoji uraia wa mtu mwingine yoyote pale inapotokea sababu ya msingi (kama mtu kutaka kuwa muwakilishi wa watu).
Tatizo kubwa ni kuwa bila kumaliza huu mjadala, itakuwa ni yale yale ya RA ambapo tangu alipoibuka 1994 akiwa kijana wa kama miaka 25 maswali yameendelea kuulizwa juu ya uraia wake na hayajakoma. Sitaki Oscar ajikute anahojiwa tena juu ya uraia 2010 au huko mbeleni endapo maswali ya msingi hayatojibiwa.
Tunaposema sheria ni kipofu maana yake ni hiyo. Haiangalii mtu ana utajiri kiasi gani, amesoma kiasi gani, amefanya vitu gani n.k swali ni JE AMEFUATA SHERIA? Wenzetu katika hili wanajitahidi sana ndio mwaana hapa in the "D" wamemfunga Meya wao jela, na sehemu nyingine wamewatia pingu wabunge wao (maseneta na wawakiilishi) bila kuwaonea haya.
Sawa FME lakini tunasubili maelezo ya kwanini alibadili jina na uthibitisho kwamba ni raia wa Tz.
- Are you sure kuhusu haya mkuu kwamba ndiyo the ishu at the table sasa hivi?
FMEs!
- Mkuu kama nimekupata vizuri ni kwamba ni haki ya kila mwananchi kuhoji ni sawa kabisa, lakini nimesikitishwa sana kwamba katika habari nzima umeshindwa hata mara moja ku-mention haki za Oscar kisheria pia kujitetea na attacts zisizokuwa na facts at hand,
- Sheria ni kweli inatakiwa kuwa kipofu, lakini only inapokuwa imeshiba yaani all facts at hand ambazo kwenye hi ishu ya Oscar, so far either hazipo au zipo ila hatujawekewa, sasa kwa mantiki ya kutokuwa na all the facts mezani bado sheria ianatkiwa kuwa kipofu.
Otherwise, baada ya kuisoma sana na betweeen the lines hii article yako, sasa I am convinced than ever before kwamba ushahidi wa ishu bado uko mbali sana na tuendelee kuusubiri.
1. Haki za Oscar hazitegemei mimi kuzitaja. Yeye kama msomi anajua haki zake na anajua ni wapi anatakiwa aziite kumtetea. Lakini zaidi ni kuwa Oscar hajanyang'wanya haki hizo.
2. Ili kuweza kushiba facts zote sheria inahitaji kuhoji maswali.
3. Kinachofanyika hapa na kwa muda tangu ianze post hii ni maswali ambayo yanalengo la kuchochea kutafuta facts.
4. Mahali pa uhakika pa kupata facts siyo JF bali mahakamani au kwenye chombo ambacho kinasimamia.
5. Sisi tunachofanya hapa ni kudodosa tu na kuchokoza lakini tusijifikirie kwa namna yoyote sisi ni sehemu ya utafutwaji haki au utoaji haki au hukumu.
6. Hili ni baraza la mijadala, maswali yanaulizwa, hoja zinatolewa na hupanguliwa, na mitazamo huundwa na fikra hubadilishwa au kudumishwa.
7. So, tuendelee kutafuta facts ndio maana hadi hivi sasa sijasema lolote kwa upande wangu kuhusu kama Oscar ni raia au si raia. Niko katika kuuliza maswali.
8. Haitoshi kusubiri tu bali pia kuchokonoa na kuuliza maswali, kuchokoza na kuibua hoja, ni katika kufanya hivyo ndivyo ambavyo tunaupekua ukweli na hatimaye kufikia mahali kusema kuwa "tunajua". Tuendelee kuuliza maswali na kutafuta majibu.
Mavi ya kale...????Lakini Oscar si alikuwa Chameda?...
Pingamizi la chadema lilikuwa na sehemu mbili. Kwanza, Oscar sio raia wa Tanzania na pili hana sifa za kugombea kwasababu hakuchaza fomu sawasawa. Kwenye fomu yake kipengele cha tatu kinauliza ulizaliwa wapi yeye akajibu "Bukoba". Kipengele cha nne kinauliza ni halmashauri/wilaya/mji/manispaa gani na yeye hakujaza kitu. Chadema wanadai "Bukoba" haitoshi kumtambulisha mtu amezaliwa wapi na vilevile unaporudisha fomu kila kipengele kinatakiwa kiwe kimejazwa tena kwa Herufi kubwa.
Oscar katika utetezi wake amewasilisha copy ya passport yake, copy ya birth certificate (ambayo tarakimu ya kwanza kwenye serial number haisomeki) pamoja barua ya mafao ya kustaafu kazi ya baba yake Biharamulo. Aidha, kwenye barua yake ya utetezi amesema bado anafuatilia vielelezo viwili, barua kutoka uhamiaji (hakusema itakuwa na nini) pamoja na cheti cha ndoa cha wazazi wake.
Mkurugenzi amesema vielelezo vilivyo kwisha wasilishwa vinatosha kuthibitisha kwamba Oscar ni raia wa Tanzania. Na kuhusu kujaza fomu sawasawa, Mkurugenzi pamoja na Oscar wamekiri kwamba fomu iliyobandikwa nje ya ofisi ilikuwa na makosa lakini fomu mbili ambazo mkurugenzi anazo zilikuwa zimejazwa kwamba anatoka mji wa bukoba. Hivyo kujazwa fomu moja kimakosa hakuwezi kumtengua Oscar kwenye kinyang'anyiro (ingawa hiyo fomu yenye makosa ndiyo ilikuwa available to the public for scrutiny).
Chadema wamekata rufaa leo mchana. Jaji makame na wenzake wanaingia Biharamulo kesho kuijadili rufaa ya chadema. Wana masaa 48 kuja na jibu.
Pingamizi la chadema lilikuwa na sehemu mbili. Kwanza, Oscar sio raia wa Tanzania na pili hana sifa za kugombea kwasababu hakuchaza fomu sawasawa. Kwenye fomu yake kipengele cha tatu kinauliza ulizaliwa wapi yeye akajibu "Bukoba". Kipengele cha nne kinauliza ni halmashauri/wilaya/mji/manispaa gani na yeye hakujaza kitu. Chadema wanadai "Bukoba" haitoshi kumtambulisha mtu amezaliwa wapi na vilevile unaporudisha fomu kila kipengele kinatakiwa kiwe kimejazwa tena kwa Herufi kubwa.
Oscar katika utetezi wake amewasilisha copy ya passport yake, copy ya birth certificate (ambayo tarakimu ya kwanza kwenye serial number haisomeki) pamoja barua ya mafao ya kustaafu kazi ya baba yake Biharamulo. Aidha, kwenye barua yake ya utetezi amesema bado anafuatilia vielelezo viwili, barua kutoka uhamiaji (hakusema itakuwa na nini) pamoja na cheti cha ndoa cha wazazi wake.
Mkurugenzi amesema vielelezo vilivyo kwisha wasilishwa vinatosha kuthibitisha kwamba Oscar ni raia wa Tanzania. Na kuhusu kujaza fomu sawasawa, Mkurugenzi pamoja na Oscar wamekiri kwamba fomu iliyobandikwa nje ya ofisi ilikuwa na makosa lakini fomu mbili ambazo mkurugenzi anazo zilikuwa zimejazwa kwamba anatoka mji wa bukoba. Hivyo kujazwa fomu moja kimakosa hakuwezi kumtengua Oscar kwenye kinyang'anyiro (ingawa hiyo fomu yenye makosa ndiyo ilikuwa available to the public for scrutiny).
Naam
Chadema wamekata rufaa leo mchana. Jaji makame na wenzake wanaingia Biharamulo kesho kuijadili rufaa ya chadema. Wana masaa 48 kuja na jibu.
Sasa hiyo kopi ya passport ni Mukasa ama Rwegasira?
gademu!! na kama hilo la Rwegasira halionekani katika jina la katikati.. ndio itakuwaje?
Naam!
Kwanini kuna suala la Uhamiaji wakati yeye ni Mtanzania?
naam!
....... Jamani miaka 29 una PHD bongo aahhh teh teh teh teh.
Sasa hiyo kopi ya passport ni Mukasa ama Rwegasira?
Umefulia kwenye huko ughaibuni, kwa taarifa yako wenye PhD kuanzia miaka 25 hadi 33 ni wa kumwaga siku hizi. Kuwa na PhD sio kitu cha ajabu bongo, kama huna master degree usirudi bongo mwanawane...
MkamaP,Harafu kingine nachotaka kufahamu kuna mdau hapo juu amesema Oscar ana PHD.Ni kweli??
Jamani kama anayo na pamoja mambo yote yanawezekana lakini kwa umri huo naanza kupatwa nawasisi wasiwasi hata kwa umri wake. Jamani miaka 29 una PHD bongo aahhh teh teh teh teh.
MkamaP,
Oscar ana miaka 39 na wala sio 29 kama ulivyoandika hapo juu. Taarifa zake zinasema alizaliwa 1970.
Kwa miaka ya nyuma ilikuwa ngumu sana kwa Mtanzania wa miaka 29 kuwa na Ph.D. Kwa siku hizi inawezekana. Kwa wale ambao hawajaenda JKT na pia hawakuhitaji kusubiri mwaka baada ya kumaliza A-level kwenda university inawezekana kabisa.