Big up Shibuda, hapa umenena! | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Big up Shibuda, hapa umenena!

Discussion in 'Jukwaa la Siasa' started by Mag3, Sep 23, 2009.

 1. Mag3

  Mag3 JF-Expert Member

  #1
  Sep 23, 2009
  Joined: May 31, 2008
  Messages: 9,094
  Likes Received: 6,188
  Trophy Points: 280
  • Mimi simzuii mtu kuwa Mbunge wa Maswa kwa sababu kuwa na mtoto wa kike huzuii mtu kuleta posa, niliishatangaza na ninaomba mtu asijisumbue kuniambia Shibuda kuna watu watano wamekuja wanataka kugombea!!, ni haki yao, ohh ninaomba hela, sina hela, siwapi !
  • Tuwashughulikie wanaopitapita kupika majungu, acha wapige majungu sina hela ya kuwapa kwa ajili Shibuda niwe mbunge, sina pesa za kununua kadi za CCM kwa ajili niongeze wanachama wa CCM kunipigia kura za maoni sina!! Nasema sina wala sitatoa hata senti tano !
  Wakati mwingine nampenda Shibuda. Hapa alikuwa analikoromea Baraza la Madiwani wa Halmashauri ya wilaya ya Maswa ambapo aliwataka watu wanaomfuata kumweleza habari hizo kuacha mara moja na kwamba binafsi hatotoa fedha zozote zile kwa lengo la kusafisha hali ya hewa jimboni. Alisema binafsi yake hatamnunulia mtu yeyote kadi ya CCM ili aje ampigie kura wakati wa kipindi cha kura za maoni na kwamba ni bora wamnyime kura.
  Big up Shibuda.
   
Loading...