Centrehalf
JF-Expert Member
- Jun 9, 2013
- 509
- 145
Amani kwa wote,ni nimeshangazwa sana na kauli zinazotolewa na Arfi pamoja na shibuda kama utetezi wao juu ya ushiriki wao kwenye Bunge Maalum la katiba.
Nikianza na Arfi yeye anasema anaenda kuwakilisha wapiga kura wake maana yeye ni mbunge,kauli ambayo haitofautiani na ya Shibuda anaedai kuwa anaenda kuwakilisha wakulima wa pamba na wafugaji wa maswa kama mbunge wao.
Maswali ninalo jiuliza juu ya kauli za hawa watu ni
1.je ni lini hawa watu wamewahi kusanya maoni ya wapiga kura wao majimboni juu ya uandikaji wa katiba mpya?maana kwa mujibu wa sheria ya mabadiliko ya katiba aliyepewa mamlaka ya kukusanya maoni nchi nzima ni tume ya Rais iliyoongozwa na Mh Warioba tu, na wala hakuna chombo kingine kilicho ruhusiwa kisheria na kwa mujibu wa sheria ya mabadiliko ya katiba ni maoni yaliyokusanywa na hiyo tume ndiyo yanayotambulika kuwa rasmi kisheria.
2. Ni lini Arfi na Shibuda walichaguliwa na wananchi kwenda kuwawakilisha kwenye bunge maalum la katiba?maana kwa mujibu wa sheria ya mabadiliko ya katiba hakuna mbunge wa Bunge Maalum la katiba aliyeingia pale kwa kuchaguliwa wote wameteuliwa na Rais.
Rais pekee ndiye aliyepewa maamlaka ya kuteua wajumbe wa Bunge Maalum la Katiba hakuna mahala sheria ilipo wahusisha wananchi kuchagua wawakilishi wao ndani ya hilo bunge.
Hao mnaosema mnawawakilisha waliwatuma lini na kwa kutumia utaratibu gani?kusema ule ukweli kwa hili mumechemsha wala hamna hoja ya kujitetea bora mungeweka wazi ni nani mnaemtumikia ieleweke kuliko kusingizia wananchi.ni suala lilowazi kuwa nyie ni vibaraka wa CCM ndio maana Arfi wamekutenga usijihusishe na mambo ya kambi rasmi ya upinzani na leo umelithibtisha kwa kufanya hadharani ulichokuwa una kataa kumbuka duniani hamna siri ndio maana utakuta hata mchawi anayefanya mambo kwa kificho tena gizani kuna siku anakamatwa mchana kweupe .
Shibuda ni mmoja wa vibaraka wa CCM ndani ya upinzani kama unakumbuka Shibuda umewahi tajwa kuhusika kwenye mpango wa kukihusisha CHADEMA na ugaidi.
Umewahi tajwa kwamba ulikuwa miongoni mwa watu waliokuwa wanawashawishi vijana wawataje Mbowe na Slaa kuwa wanafadhili ugaidi kwa ahadi ya vijana kupewa pesa na vyeo, leo imedhihirika mchana kweupe nafuu ya Zitto yeye kwa unafiki mkubwa amejitenga nanyi japo lenu ni moja.ana maana yake kwa kuwa ana malengo fulani ndio maana ameweza hata kutamka wazi kuwa UKAWA wako sahihi je yeye kwa kutoingia bungeni hana wapiga kura munge kaa nae mumuulize kuliko kujichomeka.
Maana Shibuda mimi ninge kuelewa iwapo tu ungerudisha kadi ya CHADEMA na kuwaandikia barua ya kujivua uanachama hiyo ingekujengea heshima kubwa kwa mtu kjivua ubunge kupinga uonevu au mwenendo wa CHADEMA.
Unatangaza kujitoa CHADEMA kwa mdomo tu mbona taratibu za kujivua uanachama hujazitekeleza?kama sio usanii huo.
Mh Fred Mpendazoe alipo kiponda na kukipinga CCM aliandika barua ya kujivua uanachama na kurudisha kadi yao akawa amepoteza na ubunge wake ilikutimiza kauli yake na dhamira yake yakutetea wanyonge.
Arfi na Shibuda mmechemsha maelezo yenu hayana mashiko masikioni mwa watanzania.
Nawasilisha