‘Big results now’ ni kioja au faraja

Tumake

Member
Mar 27, 2013
56
10
Hali ya elimu nchini inaonekana kuendelea kuwa mbaya licha ya ahadi nyingi za Serikali kuiboresha.
Mojawapo ya sababu za kuwepo kwa hali hiyo mbaya, inaelezwa ni mazingira duni ya kufundishia, uhaba wa vifaa na walimu kutoridhishwa na malipo kwa kazi wanazofanya.


Agosti 15, mwaka huu Serikali ilizindua utekelezaji wa mkakati wa ‘Matokeo Makubwa Sasa’ katika elimu nchini, huku sekta hiyo ikionekana kudidimia.


Elimu ni miongoni mwa sekta sita zilizochaguliwa katika Mpango wa Serikali hivi karibuni wa kuleta Matokeo Makubwa Sasa. Sekta nyingine ni Nishati, Maji, Miundombinu, Kilimo na Fedha. Sekta hizi sita zimechaguliwa ziwe za mwanzo katika kutekeleza Mpango huu wa Serikali ili kuiletea nchi matokeo makubwa kwa haraka.


Sekta hizi zinabeba msingi wa kufungulia fursa za ukuaji uchumi wa nchi kwa ujumla na kuchochea ustawi wa maisha bora kwa Watanzania wote.


Waziri wa Elimu na Mafunzo ya Ufundi, Dk Shukuru Kawambwa aliyezindua utekelezaji huo, Jijini Dar es Salaam, anasema katika sekta ya elimu, washiriki 34 kutoka taasisi 31 zikiwemo za Serikali na zisizo za Serikali, washirika na wadau wa maendeleo ya elimu walikutana kati ya 25 Februari hadi 05 Aprili, 2013, kutafakari kwa kina changamoto zinazoathiri sekta ya elimu.


Changamoto kubwa iliyoainishwa ni kiwango cha uandikishaji wa wanafunzi kimeongezeka, ubora wa elimu umeshuka, hususan kuporomoka kwa kiwango cha ufaulu katika Elimu ya Msingi na Sekondari. Kuboresha elimu ni kichocheo muhimu katika kuleta maendeleo nchini. Ingawa ufaulu siyo kiashiria pekee cha ubora wa elimu, kwa sasa ni muhimu kutumika kupima ubora wa elimu nchini kwetu.


Matokeo ya mitihani ya kidato cha nne yalivyokuwa


Asilimia 60 ya watahiniwa walipata alama sifuri yaani walifeli.


Mchanganuo ni kama hivi;


Matokeo ya kidato cha nne 2012: Alama 1 (0.4%) Alama 2 (1.6%) Alama 3 (3.9%) Alama 4 (26.0%) Alama 0 (60.1%).


Baadhi ya wananchi wanasema huenda ikawa ni mipango mizuri, cha msingi ni itekelezwe kwa vitendo. Hata hivyo baadhi wana hofu kwamba hakuna chochote cha maana kinaweza kutokea kwa sababu kwa staili ya sasa walimu hupatikana kutokana na waliofeli.


“Wengi wanaokwenda kusomea ualimu ni wale waliofeli. Kwa maana hiyo hawana uwezo wa elimu na ndiyo sababu wanashindwa kufaulisha,” anasema Mwandi Kimbwe, mkazi wa Arusha.


Mfano wa hali ya Geita


Kuna maelfu ya watoto wasiopata elimu stahiki katika vitongoji viwili vya Kijiji cha Namalandula, Bukombe mkoani Geita. Hali hiyo imesababisha wananchi kuamua kujenga shule mbili katika vitongoji vya Ilyamchele na Mtukula.


Wanaotoa taarifa za kweli hunyanyaswa na wakubwa


Agosti 15, mwaka huu, gazeti hili liliripoti kuhusu suala hili la kutokuwepo kwa shule.

Hata hivyo ilibanika baadae kuwa uongozi wa Halmashauri ya Wilaya ya Bukombe umeanza kuwafuatilia watu waliotoa taarifa za kuwapo kwa shule hizo huku zisizo na hadhi ukihoji “aliyetoa ruhusa kwa waandishi wa habari kuingia katika maeneo hayo na kuandika taarifa za shule husika”.


Wanafunzi zaidi wanufaika

Shule ya Ilyamchele ambayo sasa ina wanafunzi 600 ilianzishwa 2004 wakati shule ya Mutukula yenye wanafunzi 354 ilianzishwa 2008, zikiwa ni jitihada za kuwawezesha watoto zaidi ya 3000 waliopo katika vitongoji hivyo kupata mahali pa kusoma. Licha ya kwamba mazingira ya shule hizo siyo mazuri, lakini wananchi wa vitongoji hiyo wanasema walau malengo yao ya kuwawezesha watoto kujua kusoma, kuandika na kuhesabu yanafanikiwa.

Mkazi wa Kitongoji cha Mutukula, Suzy William anasema watoto wake wawili; Isaya William anayesoma darasa la tano na Eliza William anayesoma darasa la tatu katika shule waliyoianzisha wana uwezo wa kusoma, kuandika na kuhesabu tofauti na walipokuwa hawasomi.


Mkazi mwingine Elizabeth Leonard anasema kwa kutambua umuhimu wa elimu, wamekuwa wakichanga kiasi cha Sh20,000 kwa ajili ya kuwezesha ujenzi wa madarasa mapya tofauti na vibanda vilivyopo sasa.


Kwa mujibu wa Ofisa Mtendaji wa Kijiji cha Namalandula, Jackson Bwire shule iliyopo katika kijiji hicho ina wananfunzi 1,300 lakini ina upungufu wa vyumba vya madarasa 19 na walimu 11.


Kimsingi wananchi katika vitongoji hivyo wanailalamikia Serikali kwamba imeshindwa kuwasaidia kukamilisha majengo wealiyoanza na badala yake imekuwa ikikimbilia kufunga shule hizo ambazo kimsingi haikuzianzisha.


Msimamo wa uongozi wa Halmashauri ya Wilaya ya Bukombe ni kwamba shule hiyo ifungwe kwani haistahili kutoa elimu kutokana na kutokuwa na vigezo husika, lakini uongozi huo hautaki kueleza hatma ya kielimu kwa maelfu ya watoto wa shule hizi. Ofisa Elimu wa shule za msingi katika wilaya hiyo, Shadrack Kabanga kwa upande mmoja na Mkurugenzi Mtendaji wa Halmashauri ya Bukombe, Liliani Matinga kwa upande mwingine ni kama wanajivua wajibu kuhusu suala hilo kwa kuwa tu hakuna shule zilizosajiliwa katika vitongoji hivi.

SOURCE: Gazeti la Mwananchi


Kwa mfumo huo na hali ilivyo Big Results now inaweza kufanikiwa kweli?
 

Attachments

  • shule kioja.jpg
    shule kioja.jpg
    45 KB · Views: 80
I dont thik kama huo mpango utafanikiwa kwa mwaka huu kwa sababu ya maandalizi hafifu,may be two years ago kama mpango utaengelezwa ipasavyo
 
Kimsingi mpango wa Big result now si mbaya na unaweza kuleta matokeo makubwa japo si kwa kiwango kile kilichokusudiwa.
tatizo kubwa la mpango huu ni kutowahusisha wadau muhimu wa elimu ambao ni wanafunzi, wazazi na walimu. hawa ni kama utatu mtakatifu katika elimu. mpango unawabana zaidi walimu na maafisa wao na kuwasahau wazazi na wanafunzi. hauelezi kinaga naga jukumu la wazazi/walezi; hauelezi nafasi ya mwanafunzi na utayari wake. niliangalia kipindi cha EATV cha skonga ambapo mwanafunzi aliulizwa swali rahisi tu aaseme mahitaji 3 ya msingi ya mwanadamu. alitaja pumzi, maji, na vingine vya ajabu. sasa nikweli kuwa mwanafunzi aishie Dar ambapo kila kitu kipo anshindwa swali kama hili? mwanafunzi huyo huyo mwulize habari ya ligi za ulaya uone atakavyozichambua! je, ni kwa nini wanafuzi wanashindwa vitu rahisi vya darasani lakini wanaweza kukariri vitu vigumu kama movies za kiingereza, wachezaji, nyimbo, miziki n.k kwa usahihi? labda ni kwa sababu hawajui hatima ya elimu, hawaoni future iliyo dhahiri ndani yake?
ni kwa nini waazi wengi wana mtizamo hasi katika kuchangia elimu kuliko hata starehe? ni kweli kuwa hawana hata uwezo wa kulipa 20,000 ya ada sawa na bei ya kuku wawili ambao mtoto mwenyewe anaweza kufugiwa akawatunza na hao wakamlipia ada? mzazi anaweza kumpa fundi wa simu sh 20,000 kwa kumtengenezea simu kwa nusu saa tu lakini akagoma kulipa mchango wa jengo wa shs 5,000 kwa mwaka! mwalimu akimfundisha mtoto wake kwa mwezi kwa shs 10,000 kwa mwezi mzazi atalalamika kama katoa milioni. kimsingi elimu kwa walio wengi ni kama bidhaa ya second hand
Sasa mpango wa big result now umezingatiaje haya? kazi ya kufundisha si kama ya kusomba matofali ambayo unaweza kuiona na kuipima kirahisi bali ni kazi ambayo ni lazima iwe ya makubaliano yasiyo dhahiri kati ya msomi na msomaji kwa mpande mmoja na mfundishaji na aliyemwajiri yaani mwajiri na mzazi/mlezi kwa upande mwingine.
je, mpango wa big result umezingatia haya? ninayesema haya nimefanya utafiti katika maswala ya elimu niseme tu kwamba nina matumaini kwa mpango huu bali kuna mswali mengi yanahitaji majibu!
 
Back
Top Bottom