''BIG RESULTS NOW" Inaanza lini?; Picha zaeleza

''BIG RESULTS NOW" Inaanza lini?; Picha zaeleza

Noti mpya tz

JF-Expert Member
Joined
Mar 23, 2011
Posts
974
Reaction score
247
Mchawi wetu katuweza sana na hatuna hamu nae, misemo katupatia na maneno hakuacha kutupa.
Juzi tu tulikuwa na MMEM, MEMKWA, MKURABITA, MKUKUTA n.k. hatujafanya tathimini tukachomekea msemo wa kilimo kwanza hasa baada ya mtoto wa mkulima kuikamata ofisi ya waziri mkubwa iliyoachwa na mzee Lowasa.

Kilimo kwanza nayo hatujafanya majumuisho tumeibuka na ''BIG RESULTS NOW''!!!!!!!!!!!!!!. Sijajua nini maana ya msemo huu na nimekosa mtu wa kunieleza maana kila ninaemuuliza ananiambia nisubiri ikianza ndipo nitafahamu maana yake, sasa nimekuja hapa naomba mniambie... "BIG RESULTS NOW" inaanza lini?

Au nini maana ya ''NOW''..... Big results now ni results zipi? Positive au Negative? Au zote kwa pamoja?

Nategemea big results kwenye ELIMU, uwekezaji nyonyaji, mauaji kabla ya uchaguzi, wizi wa mali ya umma kabla ya kuondoka madarakani, big results kwenye unyanyasaji wa aina yoyote, hiyo now ni kwamba it starts now.

Hivi wewe unategemea positive big results haijalishi kama ni now au later katika uongozi huu wa dhaifu?

Nadhani tuko wengi hatuelewi hili...
 
Attachments

  • 942879_417928231639155_203917345_n.jpg
    942879_417928231639155_203917345_n.jpg
    9.5 KB · Views: 464
  • Darasa.jpg
    Darasa.jpg
    24.1 KB · Views: 368
WALIMU WANASEMA NO BIG RESULT WITHOUT BIG SALARY. Na tatizo ni kubwa la serikali yetu ni kukurupuka as if hatuna wataalamu wa kufanya investigation kabla. Mfano Amekwenda malaysia akaja na Big result pasipo kuangalia wawezeshaji [walimu] poor goverment
 
Tulieni mje muone. Mambo yanaenda sasa na matokeo utayaona punde. Acha kupiga mayowe
 
Mbona mpango wenyewe umeshakamilika na "ze bigi rezalts" zinaonekana? Wewe huoni sembe inapelekwa kila kona ya dunia mkulu akiwa kiranja wa hiyo "buziness"?
 
Ukisikia propaganda kama hii ujue kuna kitu kimepitishwa hapo. Kama si mamilioni fulani yameonekana kwenye anga basi ujue ni mpango baadaye kidogo. EPA ilitakaswaje? Power tillers, matrekta makubwa ya buluu. Big Results Now nayo ina yake. Acha kumchunguza bata wewe. Tulia uone results now.
 
Big result now ni propaganda mjamaa Kikwete kaenda malasia kacopy na kupaste sijui kama wana strategy za kuitekeleza nilimsikia mkubwa wake kasema eti mawaziri na makatibu wakuu watatoa ripoti kila mwezi ukiuliza baraza la mawaziri huwa wanacheza ndomboro labda
 
Mchawi wetu katuweza sana na hatuna hamu nae, misemo katupatia na maneno hakuacha kutupa.
Juzi tu tulikuwa na MMEM, MEMKWA, MKURABITA, MKUKUTA n.k. hatujafanya tathimini tukachomekea msemo wa kilimo kwanza hasa baada ya mtoto wa mkulima kuikamata ofisi ya waziri mkubwa iliyoachwa na mzee Lowasa.

Kilimo kwanza nayo hatujafanya majumuisho tumeibuka na ''BIG RESULTS NOW''!!!!!!!!!!!!!!. Sijajua nini maana ya msemo huu na nimekosa mtu wa kunieleza maana kila ninaemuuliza ananiambia nisubiri ikianza ndipo nitafahamu maana yake, sasa nimekuja hapa naomba mniambie... "BIG RESULTS NOW" inaanza lini?

Au nini maana ya ''NOW''..... Big results now ni results zipi? Positive au Negative? Au zote kwa pamoja?

Nategemea big results kwenye ELIMU, uwekezaji nyonyaji, mauaji kabla ya uchaguzi, wizi wa mali ya umma kabla ya kuondoka madarakani, big results kwenye unyanyasaji wa aina yoyote, hiyo now ni kwamba it starts now.

Hivi wewe unategemea positive big results haijalishi kama ni now au later katika uongozi huu wa dhaifu?

Nadhani tuko wengi hatuelewi hili...

Nadhani hii ni mipango tu ya kutafuna mikwanja ya walipa kodi na kuwapiga changa la macho wafadhiri kama ilivo mipango mingine iliotangulia; na tusistaajabu mwakani ukaibuka mpango mwingine wa maandalizi ya 2015.
 
Ukisikia propaganda kama hii ujue kuna kitu kimepitishwa hapo. Kama si mamilioni fulani yameonekana kwenye anga basi ujue ni mpango baadaye kidogo. EPA ilitakaswaje? Power tillers, matrekta makubwa ya buluu. Big Results Now nayo ina yake. Acha kumchunguza bata wewe. Tulia uone results now.

Lakini mkuu now si ndiyo sasa? where are the big results now? Mi nadhani labda wangetuandaa kwenye hiyo Project ili tujue tunafanyaje na sisi wananchi.
 
BIG RESULTS NOW walengwa wake siyo wananchi kwani kama mpango huu ungewalenga wananchi bila shaka hakuna ambaye angehoji maana na manufaa yake. Kwa mfano katika sekta ya elimu mpango huu umekuwa "implemented" mwezi Julai 2013 na wanataka hayo matokeo makubwa yaonekane kwa watahiniwa wa darasa la VII waliofanya mtihani mwezi huu wa 9. Huu kama siyo uzezeta ni nini? Unawezaje kufanikisha jambo kubwa kama hili kwa miezi miwili? Walimu ambao ndio wadau wakubwa wa mpango huu katika sekta ya elimu hawakuandaliwa kabisa bali walipewa tu maagizo kuwa ufaulu mwaka huu unatakiwa upande kutoka 31% (ufaulu wa mwaka jana) hadi 60%. SIJUI TUSUBIRI WAKATI UTATOA MAJIBU.
 
inauma kuona tusivyoiamini serikali yetu, hivi ina maana gani kama wote wanaochangia hakuna mwenye uelewa na haya matokeo makubwa inatuambia nini?

Hivi kwa wanaojua asilimia ya ufaulu inavyoweza kuyumbishwa kila mwaka mtu akikuambia hicho ndicho kitakuwa kipimo cha ukubwa wa matokeo unapata picha gani?

Mungu ibariki Tanzania!
 
haha..unanikumbusha enzi zile za JK-Lowasa Duo....jamaa walikuwa wanasema tunajipanga, tunanza ..karibu mwaka mzima sijui waenda kagua nini ili wapange mashambuli....
 
Wameshindwa big result after 50 years of freedom wataweza big results now akili zao zimechoka haziwezi kufikiri tena...!!...!!
 
Watawala wa Bongo wanaweza kupata Nobel Prize kwa ubunifu wa slogans za kupumbaza waBongo. Maana ya 'BIG RESULTS NOW' ni Maisha Bora kwa Kila Mbongo🙂 Ninasikia UVCCM na UWT vinapanga maandamano makubwa nchi nzima mwishoni mwa Septemba kuipongeza serikali sikivu kwa kuleta mpango wa BRN
 
Hujui kama tunatafuta kupiga pesa za uchaguzi 2015, tuulize walimu tumelipwa shillingi ngapi tutakuambia. Full usaniii
 
Ni usanii tu Mkuu kama ilivyokuwa ari mpya, nguvu mpya na kasi mpya, Maisha bora kwa kila Mtanzania yanawezekana, kilimo kwanza, Sasa tunalivua gamba, Tumethubutu tumeweza na sasa tunasonga mbele. Misemo chungu nzima kila kukicha lakini Watanzania hatuoni mabadiliko yoyote ya maana pamoja na utajiri mkubwa wa rasilimali uliokuwepo nchini. Na ule uchunguzi wa mabilioni ya Uswiss umeishia wapi!? Na wahusika mbona majina yao bado hayawekwi hadharani? Ni aje?
 
In other way ni mpango wa kuyapandisha matokeo hata kama watu hawatafaulu ili wawe na chakusema 2015. Ila kiukweli huo mpango hautekelezeki kwani umejaa ubabaishaji na kulazimisha yasiyo wezekana. PROBLEM CAN NOT BE SOLVED BY THE SAME OF THINKING THAT CREATE THEM.
 
Back
Top Bottom