Biden asaini amri ya kulinda haki ya kutoa mimba

Biden asaini amri ya kulinda haki ya kutoa mimba

Miss Zomboko

JF-Expert Member
Joined
May 18, 2014
Posts
4,618
Reaction score
9,611
Rais Joe Biden wa Marekani amesaini amri inayolenga kulinda haki ya kutowa mimba. Uamuzi huo ni kujibu uamuzi wa hivi karibuni wa Mahakama ya Juu kufuta haki ya kikatiba ya kuavya mimba nchini humo. Amri hiyo inawataka maafisa wa afya kuzingatia kuruhusu fedha za umma kutumika kuwasaidia wanawake kusafiri kwenye kwenye majimbo wanakoweza kutowa mimba.

Hata hivyo, hatua hiyo inatazamiwa kuwa na mafanikio madogo, kwani wajumbe wa Republican wanapigania kuwepo kwa sheria za kuzuwia utoaji mimba kwenye majimbo kadhaa ya Marekani. Uamuzi wa Biden unafanyika siku moja tu baada ya wapigakura wa Kansas kukataa kuondowa ulinzi wa kutowa mimba kwenye katiba ya jimbo hilo.

Kura hiyo lilikuwa jaribio la kwanza tangu uamuzi wa Mahakama ya Juu. Biden ameiita kura hiyo kuwa ushindi na onyo la wazi kwa wanasiasa wanaoingilia haki za wanawake. Amesema Mahakama ya Juu na Republican hawajui chochote kuhusu nguvu ya wanawake wa Marekani.


DW Swahili
 
HIZI SHERIA ZITAKUJA KUWAHUKUMU BAADAE, yaani wanaona kutoa mimba fresh tu.. okay
 
mwenzio kawa rais marekan , ww umeweza hata kuwa mwenyekiti wa hapo kwenu Chitoholii
Huo urais wake unamsaidia nini katika uhalisia? kuishi kwenye mijumba mikubwa na kupepewa na vijakazi?

Ubatili mtupu.

Acheni kuua watu.
 
Dunia haiwezi kuanza moja sababu ya Malinda yako, umeamua yafumuliwe kivyako, pambana na hali yako.
Teh ushazitaja kabisa hadi na tabia zako haya simama na mtetezi wenu anaewapambania muendeleze hayo uliyo andika
 
Back
Top Bottom