7) (A) ISSA A.S YEYE HAJAWAHI KUSULUBIWA WALA KUUWAWA Qurani Suratul An- Nisaa (Wanawake) 4:157-158 Na kwa (ajili ya ) kusema kwao sisi tumemuua masihi Isa mwana wa Maryamu, mtume wa Mungu. Hali hawakumuua wala hawakumsulubu bali walibabaishiwa (mtu mwingine wakamdhani nabii Isa.) Na kwa hakika wale waliokhitalifiana katika (hakika)hiyo (ya kumuua nabii Isa) wamo katika shaka nalo (jambo hilo kusema kauwawa]. Wao (kabisa) hawana yakini juu ya (jambo) hili (la kuwa kweli wamemuua nabii isa) isipokuwa wanafuata dhana tu.Na kwa yakini hawakumuua. Bali mwenyenzi Mungu alimnyanyua kwake. Na mwenyenzi Mungu ni mwenye nguvu (na) mwenye hikima. (B)YESU KRISTO: YEYE ALISULUBIWA MSALABANI Yohana 19:18,31,33 Wakamsulibisha huko,na wengine wawili pamoja,mmoja huku na mmoja huku, na Yesu katikati.Basi Wayahudi, kwa sababu ni Maandalio, miili isikae juu ya misalaba siku ya sabato(maana sabato ile ilikuwa siku kubwa), walimwomba Pilato miguu yao ivunjwe,wakaondolewe. Lakini walipomjia Yesu na kuona ya kuwa amekwisha kufa,hawakumvunja miguu. 8) (A) ISSA A.S HANA HADHI YA KUABUDIWA NA BINADAMU YEYOTE. Quran, Suratul Al- Maidah, 5:116 Na (kumbukeni) Mwnyezi Mungu atakaposema: Ewe Isa bin Maryam! Je ,wewe uliwaambia watu: Nifanyeni mimi na mama yangu kuwa waungu badala ya Mwenyezi Mungu? Aseme (Nabii Isa): Wewe umetakasika na kuwa na mshirika, hainijuzii mimi kusema ambayo si haki yangu (kuyasema, kwa kuwa ni ya uongo), kama ningalisema bila shaka ungalijua ; unayajua yaliyomo nafsini mwangu, lakini mimi siyajui yaliyomo nafsini mwako; hakika Wewe ndiye ujuaye mambo ya ghaibu. B) YESU ANASTAHILI KUABUDIWA NA WANADAMU NA MALAIKA Math 2: 2 yuko wapi yeye aliyezaliwa mfalme wa Wayahudi? kwa maana tuliiona nyota yake mashariki nasi tumekuja kumsujudia. Yoh 9: 35 Yesu akasikia kwamba wamemtoa nje; naye alipomwona alisema, Wewe wamwamini Mwana wa Mungu? Naye akajibu akasema, Ni nani, Bwana, nipate kumwamini? Yesu akamwambia Umemwona, naye anayesema nawe ndiye. Akasema, naamini, Bwana, akamsujudia. Filipi 2:10-11 ili kwa Jina la Yesu kila goti lipigwe, la vitu vya mbinguni, na vya duniani, na vya chini ya nchi; na kila ulimi ukiri ya kuwa YESU KRISTO NI BWANA, kwa utukufu wa Mungu Baba. Ebr 1:6 Hata tena amletapo mzaliwa wa kwanza ulimwenguni, asema, Na wamsujudu Malaika wote wa Mungu. 9) (A) ISA HASTAHILI KUWA MWOMBEZI WA WATU KWA MUNGU Sahih Al-Bukhari, vol.6 ,Hadithi no 3, The Noble Quran, English Translation uk. 8
.Nenda kwa Musa, mtumishi wa Allah ambaye Allah alizungumza naye uso kwa uso na alimpa Torati. Hivyo watakwenda kwake naye atasema Mimi sistahili kwa jukumu hilo la uombezi, na atataja mauaji aliyoyafanya kwa mtu ambaye si muuaji, na hivyo atajisikia aibu mbele ya Mola wake, naye atasema nendeni kwa Isa, mtumishi wa Allah, Mjumbe wake neno lake na roho iliyotoka kwake. Isa atasema sistahili mimi kubeba jukumu la uombezi
. B) YESU ANASTAHILI KUWA MWOMBEZI WA WANADAMU KWA MUNGU 1 Tim 2:5 Kwa sababu Mungu ni mmoja, na mpatanishi kati ya Mungu na wanadamu ni mmoja, Mwanadamu Kristo Yesu; Ebr 7:24-25 bali yeye, kwa kuwa akaa milele, anao ukuhani wake usioondoka.Naye, kwa sababu hii , aweza kuwaokoa kabisa wao wamjiao Mungu kwa yeye; maana yu Hai siku zote ili awaombee. 10) (a) ISA NI NABII MWINGINE TU ASIYE TOFAUTI NA WENGINE Quran Suratul Baqarah, (ngombe) 2:136 Semeni nyinyi (Waislamu waambiwe Mayahudi na Manasara; waambieni): Tumemwamini Mwenyezi Mungu na yale tuliyoteremshiwa, na yale yaliyoteremshwa kwa Ibrahimu na Ismail na Is-haqa na Yaaqubu na kizazi (chake Yaaqubu); na waliyopewa Musa na Isa na pia yale waliyopewa Manabii (wengine) kutoka kwa Mola wao; hatutofautishi baina ya yoyote katika hao. (Wote tunawaamini); na sisi tumenyenyekea Kwake. b) YESU YEYE YU JUU KULIKO VITU VYOTE Efeso 1:20-23 aliotenda katika Kristo alipomfufua katika wafu, akamweka mkono wake wa kuume katika ulimwengu wa roho; juu sana kuliko ufalme wote, na malaika, na nguvu, na usultani, na kila jina litajwalo, wala si ulimwenguni humu tu, bali katika ule ujao pia; akavitia vitu vyote chini ya miguu yake akamweka awe kichwa juu ya vitu vyote kwa ajili ya Kanisa; ambalo ndilo mwili wake, ukamilifu wake anayekamilika kwa vyote katika vyote. 11) (a) ISA ATAKAPORUDI, ATAOA NA KUZAA WATOTO Mishkat Al- Masabih, vol 2 uk.1159, Sahih Muslim, vol. 1 uk 92 Isa atakaporudi ataishi miaka arobaini (40), muda ambao atakuwa ameoa na kuzaa watoto, na atafanya ibada ya hija. b) YESU ATAKAPORUDI ATAKUJA KULINYAKUA KANISA, YAANI BIBI ARUSI Efeso 5:25-26, 32-33 Enyi waume, wapendeni wake zenu, kama Kristo naye alivyolipenda Kanisa, Uf 19:7 Na tufurahi, tukashangilie, tukampe utukufu wake; kwa kuwa arusi ya Mwana Kondoo imekuja na mkewe amejiweka tayari.akajitoa kwa ajili yake, ili makusudi alitakase na kulisafisha kwa maji katika neno;
..Siri hiyo ni kubwa ila mimi nanena habari ya Kristo na Kanisa. Lakini kila mtu ampende mke wake kama nafsi yake mwenyewe; wala mke asikose kumstahi mmewe. 12)(a) ISA ATAKUFA BAADA YA KUISHI MIAKA AROBAINI (40) Mishkat Al- Masabih, vol 2 uk. 1159,Sunan Abu Dawud, Hadithi 4310, Sahih Muslim, vol.1, uk.92 , Isa atakaporudi ataondosha dini zote zisiwepo isipokuwa Uislamu. Atamharibu Masih Dajjal, na ataishi duniani miaka arobaini (40) na kisha atakufa. Na baada ya kufa atazikwa pembeni mwa kaburi la Muhammad. B) YESU BAADA YA KUFUFUKA YU HAI SIKU ZOTE HAFI TENA Rum 6:9 tukijua ya kuwa Kristo akiisha kufufuka katika wafu hafi tena, wala mauti haimtawali tena. Ebr 7:24-25 bali yeye, kwa kuwa akaa milele, anao ukuhani wake usioondoka.Naye, kwa sababu hii , aweza kuwaokoa kabisa wao wamjiao Mungu kwa yeye; maana yu Hai siku zote ili awaombee. Uf 1:17-18 Nami nilipomwona nalianguka miguuni pake kama mtu aliyekufa. Akaweka mkono wake wa kuume juu yangu, akisema, Usiogope, mimi ni wa kwanza na wa mwisho, aliye hai; nami nalikuwa nimekufa, na tazama , ni hai hata milele na milele nami ninazo funguo za mauti na za kuzimu. 13)(a) ISA ALIPOZALIWA SAUTI YA FARAJA ILITOKA CHINI YA ARDHI Quran Suratul Maryam,19:23-24 Kisha uchungu ukampeleka katika shina la mtende, (akawa anazaa na huku) anasema: Laiti ningekufa kabla ya haya, na ningekuwa niliyesahaulika kabisa. Mara ikamfikia sauti kutoka chini yake (inamwambia): usihuzunike. Hakika Mola wako amejaalia (ameweka) kijito cha maji chini yako; Mafundisho ya Kiislamu yanaeleza kuwa huko chini ya ardhi kuna mnyama. Na huyo mnyama anazijua aya za Quran. Quran katika Suratul Al-Naml, 27:82 Na kauli (ya kuja kiyama) itakapowathibitikia Tutawatolea mnyama katika ardhi atakayewasemeza kwa sababu watu walikuwa hawaziyakinishi Aya Zetu b) ALIPOZALIWA YESU SAUTI ZA MALAIKA ZILITOKA JUU Luka 2:13-16 Mara walikuwapo pamoja na huyo malaika, wingi wa jeshi la mbinguni, wakimsifu Mungu na kusema, Atukuzwe Mungu juu mbinguni na duniani iwe amani kwa watu aliowaridhia. Ikawa malaika hao walipoondoka kwenda zao mbinguni, wale wachungaji waliambiana, Haya na twendeni mpaka Bethlehemu, tukalione hilo lililofanyika alilotujulisha Bwana. Wakaenda kwa haraka wakamkuta Mariamu na Yusufu, na yule mtoto mchanga amelala horini (14)(a) ISA HANA UFAHAMU WA MAMBO MBALIMBALI