chamtemamoto
JF-Expert Member
- Jul 30, 2013
- 796
- 215
Hatuongozi na mavazi tunaongozwa na maandiko kama haya!
(b)yesu kristo alimtuma roho mtakatifu katika siku ya pentekoste. Yoh: 14:26 .lakini huyo msaidizi,huyo roho mtakatifu,ambaye baba atampeleka kwa jina langu,atawafundisha yote,na kuwakumbusha yote niliyowaambia. Katka kiyunani anaitwa paracletos yaani msaidizi au mfariji yoh 15:26 lakini ajapo huyo msaidizi, nitakayewapelekea kutoka kwa baba, huyo roho wa kweli atokaye kwa baba, yeye atanishuhudia yoh 16:7 lakini mimi ninawaambia iliyo kweli; yawafaa nyinyi mimi niondoke,kwa maana mimi nisipoondoka huyo msaidizi hatakuja kwenu; bali mimi nikienda zangu nitampeleka kwenu. 4) (a) issa a.s : Jina lake halina nguvu wala uwezo wa kuokoa bali ni rangi mbili katika al-luluwar- marjani, juzuu na1, hadithi na104 uk. 64 hadithi ya ibn abbas (r.a) kutoka kwa mtume (s.a.w) amesema, nilimuona musa (a.s) katika usiku wa al-isra, niliopelekwa,naye ni mtu mrefu, mwenye nywele za hudhurungi zimejikunjakunja kama mtu wa shanua.na nilimuona isa (a.s), naye ni mtu wa wastani wa umbo, unaelekea kwenye wekundu na weupe, ana nywele zilizonyooka (b) yesu kristo: Jina lake ni wokovu. Mdo 4:9-10,12 kama tukiulizwa leo habari ya jambo jema alilofanyiwa yule mtu dhaifu,jinsi alivyoponywa, jueni nyinyi nyote na watu wote wa israel ya kuwa kwa jina la yesu kristo wa nazareti, ambaye nyinyi mlimsulubisha, na mungu alimfufua katika wafu kwa jina hilo mtu huyu anasimama ali mzima mbele yenu .wala hakuna wokovu katika mwingine awaye yote, kwa maana hapana jina jingine chini ya mbingu walilopewa wanadamu litupasalo sisi kuokolewa kwalo baadhi ya aya ndani ya quran zinaeleza kuwa isa a.s aliwaponya wenye upofu. Ni akina nani hao tutajiwe angalau mmoja? Yesu alimponya kipofu batromayo. Aya zingine zinasema isa a.s alifufua wafu. Ni akina nani hao? Yesu alimfufua lazaro. Jina tulilopewa ni jina moja tu lenye wokovu la yesu kristo. Jina la isa a.s lisilo na wokovu limehusishwaje na jina la yesu kristo wa nazareth lenye wokovu? Mdo 16:31 wakamwambia , mwamini bwana yesu, nawe utaokoka wewe pamoja na nyumba yako. 5) (a) issa.a.s : Yeye siyo mwana wa mungu. Qurani suratul al an-am,6:101 yeye ndiye mwumba wa mbingu na ardhi. Inamkinikanaje awe na mwana, hali hana mke. Naye ndiye aliye umba kila kitu (sio baadhi yake kavizaa). Naye ni mjuzi wa kila kitu. Qurani suratul at- tawba (kutubu), 9:30 na mayahudi wanasema uzeri ni mwana wa mwenyezi mungu na wakristo wanasema masihi ni mwana wa mwenyezi mungu haya ndiyo wasemayo kwa vinywa vyao (pasi na kuyapima). Wanayaiga maneno ya wale waliokufuru kabla yao, mwenyezi mungu awaangamize. Wanageuzwa namna gani hawa! Fundisho la uwana wa mungu kama biblia inavyofundisha, halimo katika mafundisho na itikadi ya dini ya kiislamu kwa hiyo isa a.s siyo mwana wa mungu. (b) yesu kristo: Yeye ni mwana wa mungu. Luka 1:30-31,35 malaika akamwambia usiogope mariamu,kwa maana umepata neema kwa mungu.tazama utachukua mimba na kuzaa mtoto mwanamume; na jina lake utamwita yesu. Malaika akajibu akamwambia,roho mtakatifu atakujilia juu yako,na nguvu zake aliye juu zitakufunika kama kivuli;kwa sababu hiyo hicho kitakachozaliwa kitaitwa kitakatifu mwana wa mungu. Hivyo isa siyo mwana mungu lakini yesu ni mwana wa mungu. Kwa hivyo yesu siyo isa. 6) (a) issa a.s: Yeye siyo mungu aliyefanyika mwili. Suratul al- maidah, (meza), 5:72-73 bila ya shaka wamekufuru wale waliosema, mwenyezi mungu ni masih (issa)bin maryam.(na hali ya kuwa)masihi alisema enyi wana wa israel! Mwabuduni mwenyezi mungu, mola wenu. Kwani anayemshirikisha mwenyezi mungu, hakika mwenyezi mungu atamharimishia pepo, na mahali pake (patakuwa) ni motoni. Na madhalimu hawatakuwa na wasaidizi (wa kuwasaidia siku ya kiama) kwa hakika wamekufuru wale waliosema mwenyenzi mungu ni mmoja katika (wale waungu) watatu (yeye ndiye watatu wao ) hali hakuna mungu ila mwenyezi mungu mmoja ( tu peke yake) na kama hawataacha hayo wasemayo kwa yakini itawakamata wale wanaoendelea na ukafiri miongoni mwao adhabu iumizayo. (b)yesu yeye ni neno la mungu lililofanyika mwili: Yoh 1 : 1,14 hapo mwanzo kulikuwako neno, naye neno alikuwako kwa mungu naye neno alikuwa mungu ..naye neno alifanyika mwili akakaa kwetu . 7) (a) issa a.s yeye hajawahi kusulubiwa wala kuuwawa