Bibi kizee na kopo la castle

ARV

JF-Expert Member
Joined
Sep 6, 2011
Posts
5,554
Reaction score
7,993
Bibi kizee mmoja alikuwa anasafiri kwenye basi usiku na siti ya nyuma yake alikaa kijana mmoja. Wakati safari inaendelea akawa anainama chini ya siti yake anachukua kopo la castle na kulipeleka mdomoni(kama anakunywa kitu) sasa yule kijana wa nyuma yake akawa anashangaa huyo bibi anavyofaidi maisha kwa kunywa castle toka safari inaanza, akatamani amuibie angalao apige pafu moja halafu arudisha haraka lile kopo kabla bibi hajashtuka,Basi akamtaimu bibi wakati analitoa mdomoni na kuliweka chini kwa haraka akapitisha mkono chini ya seat akachukua lile kopo akanywa funda moja kuuubwa, baada ya hapo tukasikia mtu anapiga makelele na kutema mate kama mtu anayetaka kutapika, Kumbe yule bibi alikuwa anaumwa Kifua kikuu na alichukua kopo lile la castle kwa ajili ya kutemea makohozi...
 

nimekosea njia, samahani na kwaheli.
 
ebwanaee.wengine 2po mezani na jokx kama hivi zinakatiza apetaiti.he he.
 
hii sio joks bana, kwanza kitendo cha kutema mate na kunywa kitu haviendani, we unaweza kunywa kama unatema kweli?
 
Aaaaaagh...!shit! Umesababisha nimeshindwa kula kuku,maini,thupu,mayai,chipthi,ndizi,maembe,machungwa.....sasa nalala njaa,vyakula vyote hivi inabidi nivimwage tu..aaagh!
 
mmmhhh...mambo gani tena hayo ya kutapishana ndugu!next time toa tahadhari kabla mtu hajasoma.
 
Wizi ni nouma unaiba visivyoibika
 

wanitapisha!!!!
 

Similar Discussions

Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…