wadzelino
JF-Expert Member
- Sep 16, 2019
- 231
- 391
Dunia imebeba mengi sana na Ukistaajabu ya Musa Hujayaona ya Firauni.
Hii imetokea Kijijini kwetu huku. Baada ya Utambulisho na maridhiano ya pande mbili. Mahari ikatolewa, Mil 2.5 hivi, na mipango ya harusi ikaanza.
Ee bwana ee siku zimesonga, hatimaye siku ya harusi ikawadia, mapema kabisa bibi Harusi akapelekwa saluni ili apambwe, kumbe alikuwa na yake, ni kwamba watu walisubiri bibi harusi hakurejea, almost wiki, taharuki imetanda.
Wazazi wa pande zote hawaelewi, wale wa binti ndo kabisa, kwa kuwa fedha walopokea kama Mahari ilishatumika, na Hawana kipato cha kuweza kurejesha, baada ya wiki.
Binti kaja kuonekana, akapangwa fasta baada ya manung'uniko ya Wazazi hapa na pale akakubali kukaa nao chini kuwaeleza ukweli, heee. Hawakuamini walichosikia!
Nanukuu "Kwa kweli mimi wakati nakutana na huyu (bwana aliyetaka kufunga ndoa) nilikuwa na bwana mwingine ninaempenda sana, ila huyu nilimpendea fedha tu, alikuwa akinihudumia, sasa ukweli ni kwamba Sikuwa tayari animiliki moja kwa moja, ndiyo maana nilifanya vile"
Mama yake alianguka ghafla.
Itaendelea...