BiBi Bombaaaaa Mawingu TVi

Lovebird

JF-Expert Member
Sep 27, 2012
5,786
7,750
FYI

"Mimi sio mtazamaji mzuri wa Clouds TV kwa kuwa vipindi vyake vingi ni vya ovyo–havina mvuto wala mafundisho ya maana. Jana, kwa bahati mbaya, nilitazama kipindi cha ‘BIBI BOMBA’ kinachorushwa na TV hiyo. Nimehuzunishwa sana kuona jinsi bibi na mama zetu wanavyodhalilishwa hadharani. Bibi zetu huulizwa maswali ya kidhalilishaji.

Bibi mmoja aliulizwa kama aliwahi kula mboga inayoitwa ‘Biology’, akajibu ‘ndiyo’. Hili ni swali linalohusu ufahamu na kwa wabibi wale ambao hawakwenda shule, hawajui biology ni nini. Si hivyo tu, hata wale walioishia la saba hawajui biology ni kitu gani. Kuwauliza mabibi swali kama hili ni kuwadhalilisha kitaaluma kwa kuwa tu hawakwenda shule.

Bibi mwingine aliombwa amtongoze kijana yule anayewauliza maswali hadi amkubali. Bibi akatekeleza agizo hilo laivu mbele ya skrini ya TV! Huu ni udhalilishaji wa hali ya juu.
Kama kweli kinachofanyika katika kipindi kile ni kuwajali bibi wale kwa maana ya kuwapatia pesa wakishinda hebu wanaoendesha kipindi kile siku moja wawalete bibi zao na wawahoji maswali yale ya kishenzi tuone kama itakuwa sawa kwao, kwanini pesa iwe kigezo cha kudhalilisha watu wazima? Tena wanadhalilishwa na vijana wadogo wasio na chembe ya maadili? Hivi kweli kumwambia bibi mtu mzima amtongoze kijana mdogo halafu mbele ya skrini kila watu wa rika tofauti wanatazama wakiwemo watoto hapo tunafundisha maadili gani kwa jamii?
Wizara ya jinsia inapaswa kukataza udhalilishaji huu wa kijinsia. Nasi wananchi tuache kushabikia upumbavu huu–tukatae kuwapigia kura bibi wanaoshiriki"
 
Back
Top Bottom