Biashara zangu zimegeuzwa kuwa za ukoo

Tripp

JF-Expert Member
Feb 2, 2018
899
1,543
Habari wadau naombeni ushauri...

Mimi ni kijana ila Mungu alinijalia ajira ya muda mfupi nikapata pesa nyingi. Sasa nimefungua biashara 2 hapa Dar na zinanilipa, ila tatizo kubwa ni kwamba familia na wanandugu wamekuwa wakifanya kama mali za ukoo.

Kutwa kucha wana matatizo na wamekuwa wakienda hata kama sipo wanachukua pesa kwa waajiri kwa kigezo cha kaka, dada au mjomba n.k

Nifanyaje?
 
Mkuu hebu simama hapo ulipo. Toa amri hii haitaki mazungumzo wala makubaliano *Mtu yoyote asipewe pesa au bidhaa bila idhini yangu* hata kama ni mzazi mtoe hapo kwa ujanja weka mfanyakazi mwingine.
Mwanzoni watakuchukia ila baada ya miezi 2-6 watazoea tu.
Sawa nitafanya hivyo. Je wakitoa pesa mfano niwafanyaje
 
Sawa nitafanya hivyo. Je wakitoa pesa mfano niwafanyaje
Mtu akikiuka utaratibu chukua hatua na hakufai hapo dukani. Ama kila akiuza kusanya pesa usinunue mzigo hadi abaki na mashelfu tu ufungue kwingine. Kama ni mama unamwambia kuna madeni ya bank nalipa mkopo nilichukua.
Hata kiishe kitu cha elfu usinunue. Akibaki yeye na frem nyeupe arudi home asubiri hela ya matumizi utakayompa.
 
Fungua biashara nyingine kisiri halafu hizo mbili ziue kwa makusudi kisha anza kuwalaumu hao wanandugu

kama huwezi kuwalaumu nitakufundisha nipo njema kwa kulaumu
Asante
 
Fungua biashara nyingine kisiri halafu hizo mbili ziue kwa makusudi kisha anza kuwalaumu hao wanandugu

kama huwezi kuwalaumu nitakufundisha nipo njema kwa kulaumu
kama hiyo biashara mpya atayofungua itafeli na kufa je?

back to square 0
 
Back
Top Bottom