Biashara za majeneza hospitalini zinawapa msongo wa mawazo wagonjwa

Analogia Malenga

JF-Expert Member
Feb 24, 2012
5,038
9,928
1578719480344.png

Wafanyabiashara ya kuuza majeneza karibu na hospitali wamepewa hadi Machi kuondoa bidhaa zao karibu na hospitali moja iliyopo mjini Lusaka, Zambia kulingana na gazeti la Daily Mail.

Meya wa mji wa Lusaka Miles Sampa amesema kwamba wauza majeneza watahamishwa hadi maneo ya makaburini iwapo hawataondoka.

Wafanyabiashara hao walikuwa wamefungua maduka yao nje ya Hospitali ya Chuo Kikuu, ambapo kuna chumba cha kuhifadhi maiti.

Inasemekana kwamba wagonjwa na jamaa zao waliwasilisha malalamishi yao katika mamlaka ya eneo, na kusababisha kuchukuliwa kwa hatua hiyo.

Meya Sampa alinukuliwa na gazeti la Daily Mail akisema kwamba wauzaji majeneza walikuwa wanawapa wagonjwa msongo wa mawazo, na kufanya iwe vigumu kwao kupata nafuu.

Meya huyo pia amesema kwamba wafanyabiashara hao wameombwa kutafuta eneo mbadala la kuuza majeneza yao au wahamishwe hadi maeneo ya makaburini kuendeleza biashara yao.

Kwa kipindi kirefu biashara hiyo imekuwa kama mkombozi na kuwa moja ya njia kuu ya kuwapa vijana kiapato na pia kuwekwa kwa majeneza hayo hospitalini, kulionekana kama eneo sahihi la kuendesha biashara hiyo.

Biashara hiyo ilionekana kuhudumia zaidi wale wanaotoka maeneo ya mbali.

Wafanyabiashara ya kuuza majeneza pia wamekuwa wakitoa huduma zengine kama kutayarisha mwili na kuusafirisha na kuonekana kupunguza mzigo kwa waombolezaji ambao mara nyingi huwa katika hali ya kukosa ujasiri wa kujifanyia shughuli za kumuaga mwendazake jamaa wao anapoaga dunia.

Hata hivyo, biashara hiyo imekuwa ikitekelezwa karibu sana na wadi za wagonjwa ambao wamelalamika kwamba tukio hilo huwakosesha imani ya kupona hasa pale waombelezaji wanapojitokeza mchana mzima husababisha wagonjwa kufikiria zaidi kuhusu kifo badala ya uponaji.

Katika eneo hilo kifo kimekuwa kikichukuliwa kama biashara nyengine yoyote mfano uuzaji wa dawa na kadhalika.

Wakazi wanaamini kwamba majeneza hayastahili kuuzwa kwenye hospitali hiyo kwasababu hilo ni eneo linalostahili kuwapa wagonjwa moyo na utulivu wa akili badala ya kuwatia hofu.
 
Kuna wale jamaa wa pale manzese Agentina kama unatoka Ubungo kwa kwenda mjini upande wa kulia kwa miaka mingi wamekuwa wakiyaanika wazi kabisa barabarani hawa nao serikali iingilie kati waache kuwapa watu msongo wa mawazo.

Wayatunze ndani .

Kwani biashara hadi uiweke wazi nje ndiyo watu waje kununua?

Mbona bidhaa nyingi tu zinafatwa zikiwa ndani ya maduka zimetunza


Sent using Jamii Forums mobile app
 
Kila nafsi itaonja mauti... watengeneza majeneza na wachimba makaburi, madaktari na manesi, mapadre na kasheshe, mimi na wewe.... hakuna atakayesalia.

Kila mtu atimize wajibu wake.

Namwomba Mungu anijalie kifo chama, nife kwa amani.
 
Kule muhimbili maeneo ya nje ya hospitali zamani walikuwa wanayaanika nje barabarani lakini baadae naona walisemwa wakajirekebisha wakaweka ndani ya ofisi kwa vioo.

Hata hivyo bado inahitajika maboresho.

Na hii siyo kwa Dar tu hata mikoani na wilayani na hatimae mitaani pia


Sent using Jamii Forums mobile app
 
Wazo la RC Makonda la biashara na maduka ya bidhaa kuwa na mpangilio lilikuwa zuri sana, sijui kina nani wanakwamisha utekelezaji wake.

Ifike mahala ijulikane kuwa ukitaka huduma au bidhaa fulani ukienda maeneo fulani huko ndiko utakuta maduka ya bidhaa hizo na kuzipata kwa ushindani mzuri


Sent using Jamii Forums mobile app
 
sioni sababu ya kuwazuia, kifo hakiepukiki na pia hao kama wafanya biashara ni jukumu lao kuiweka bidhaa yao mahali sahihi ambapo wateja wao wataiona kirahisi.

na jambo jingine, mgonjwa anapokuwa na hofu ya kifo zaidi kuliko kuwa na tumaini la kupona zaidi inabidi kwanza tuhoji kuhusu ubora wa huduma zitolewazo huko kwenye vituo vyetu vya afya kabla hatujafanya maamuzi ya kuwaondoa wafanya biashara maeneo yaliyo sahihi kwa biashara zao.
 
Wazo la RC Makonda la biashara na maduka ya bidhaa kuwa na mpangilio lilikuwa zuri sana, sijui kina nani wanakwamisha utekelezaji wake.

Ifike mahala ijulikane kuwa ukitaka huduma au bidhaa fulani ukienda maeneo fulani huko ndiko utakuta maduka ya bidhaa hizo na kuzipata kwa ushindani mzuri


Sent using Jamii Forums mobile app
Mpangilio huo niliuona Kampala na Nairobi, lkn kwa Dar sijui kama itawezekana walishachelewa mno.
 
Back
Top Bottom