Webabu
JF-Expert Member
- Apr 29, 2010
- 7,194
- 10,929
Kitendo cha jeshi la Israel kupiga magari ya wagonjwa na kambi za wakimbizi wanakoishi mafukara kumewashangaza mpaka viongozi wa UN na US.
Msafara wa magari ya wagonjwa na waliojeruhiwa vibaya uliokuwa ukiondoka hospitali kuu ya Alshifa umepigwa na makombora mazito kutoka angani na kusababisha vifo vya wagonjwa hao jumla 15.
Waliokuwa wakisafiishwa kwenye magari hayo ni wale waliojeruhiwa vibaya katika mashambuizi ya karibuni kwenye kambi za wakimbizi kama vile Jabaliya na Nusreita ambako asili yake wanaishi watu maskini zaidi katika eneo la Gaza.
Katika kujieleza,jeshi la nchi hiyo IDF limesema ni kweli wao ndio waliopiga magari hayo na kwamba walikuwa wanapiga kuwamaliza wapiganaji wa Hamas.Kinachoshganaza walijuwaje kuwa hao ni Hamas bila kuona vitambulisho vyao
Iwapo ni kuwapiga Hamas mpaka hapo si ilikuwa tayari wameshawapiga.Kulikuwa na haja gani kuwapiga tena ilhali hawana silaha.Na kwanini wasingeteremka hapo hospitali kwenda kuwakamata