Biashara za bakery, nafaka na vinywaji

Hizi ndio product Kali kutoka Mirembe international school
Habari wakuu,

Kama unadhani biashara ni rahisi, basi jaribu kufanya. Hakuna sababu ya kujifunza kwa njia ngumu kama tayari kuna ambao walishajifunza na kusahihisha makosa.

Bila kupoteza muda, naomba kuleta kwenu fursa kadhaa.

1. BAKERY - Nimefanya shughuli hii kwa miaka mitano sasa. Na kwakuwa nimejiridhisha na nimemaliza kujifunza, sasa nahitaji mtu/watu serious waje tuilishe nchi.
Nahitaji kufunga Machine modern ambazo zitapunguza gharama za labour na kuongeza volume ya uzalishaji na hivyo faida. Uwekezaji huu unahitaji milioni 120 (Tsh. 120,000,000/=). Ukiwa serious ntashare business plan uipitie kabla hatujafanya makubaliano. Benki wako tayari kunipatia 80m lakini naona itafaa zaidi tukianza na 120m. Kama kuna namna nnayoweza kupata pesa hiyo ntafurahi zaidi na kama kuna mtu ana interest na industry ya Baking basi anaweza kusogea tuunge misuli pamoja.

2. NAFAKA - Mimi si mkulima na sina hobby na kilimo kabisa. Lakini niko kwenye mnyororo wa thamani wa kilimo. Ninazo godown kadhaa jijini Dar na soko la uhakika la nafaka hasa Mahindi. Tatizo langu kubwa ni kukosa mtaji wa kutosha kuleta mzigo mkubwa na kuuzungusha.
Again, kama kuna mtu ni mkulima mkubwa au supplier mwenye uhakika wa kushusha minimum ya tani 100 za mahindi kila wiki Dar, basi naomba tuwasiliane. Niko tayari kutoa godowns zangu na wateja wangu wote ili mzunguko uwe wa haraka. Hapa utachangua, unilipe senti kidogo kwa kila kilo tutayouza au uniuzie mimi kwa bei yako namim niuze kwa bei ya Dar. Soko ni la uhakika na niko tayari kukutoa wasiwasi kadiri utakavyohitaji.

3. VINYWAJI VYA JUMLA
- Nna "point" iliyoko barabarani, nimeshindwa kuweka vinywaji kama nlivyowaza mwanzoni (sikuwa na pesa). Hapa namkaribisha yoyote mwenye mapenzi na aina hii ya baishara aje tuuze vinywaji. Huku sina uzoefu napo sana lakin ni eneo zuri (Near Sinza -Dar) na hivyo ni rahisi kuuza pombe.

Kwa kumalizia, nlijipa muda kujifunza biashara mbalimbali na sasa nimeamua kuwekeza kwa nguvu kwenye biashara tajwa hapo juu. Kwa mwenye interest nawakaribisha Pm.

Kazi iendelee.
 
jamaa ana content, sema anaongea kama dalali, watu wa dar hizi lugha tumekutana NAZO sana 😂😂. anakupanga ukijaa, unakuta ni winga
 
Mkuu itoshe tu kusema "Bado hujui nini unakitaka kwenye haya maisha"
 
😁 Sasa si umtafte bahresa au manji chapchap au nikurlekeze majumbani mwao?
 
Similar Discussions

Back
Top Bottom