Biashara ya vitu vya ndani

ankol

JF-Expert Member
Aug 21, 2012
2,110
3,481
Nawasalimu waungwana.

Nimetenga kiasi cha pesa 10m niweze jiajiri kwa kuuza vitu vya ndani kama ma carpet, ma duvet, mito, mapazia like kama unavyoyaona maduka ya home shopping center.

Nachoomba kutoka kwenu ni ABC ya biashara hii. Je nitatoboa? Location ni Sinza karibu ya Palestina.

Mwenye ufahamu wa biashara hii basi tujuzane.

Karibuni.

1623071277020.png

  • Thanks
Reactions: Doz
Kila mtu na bahati yake, ila kwa msimu hu mwezi wa sita kazi inakua ngumu ungeanza December ungepata boost kdgo, tena kubuka hayo ni luxury items mtu hununua baada ya kumaliza mahitaji muhimu, pia kila sehemu wamefungua hiyo aina ya maduka na bei zinafanana na huku kwetu tangi bomvu naona ni mengi kweli kweli.
 
Mwanangu jiachie tuu , nenda Kwa wauzaji wa jumla chukua mzigo Anza kupambana ,nothing to wait .... Ukipata exposure kdog unabypassy unakuwa unaagiza nje moja Kwa moja....!! Fresh Tu kibabe huku unasubir sku yako ya kufa....
 
Kuna competition ya vitu used toka nje, je unaiconsider vipi?
Vitu vipya bado vinathamani, ni biashara nzuri wewe jilipue ila jitahidi kuuza vya gharama nafuu vitatoka haraka maana wengi wanauzia bei za mall sasa wewe uzia bei za kimtaani.
 
vifaa kama vipo boss
Kuna hamira , vifungashio vya keki n.k

Kama una mtu mikoani mpe hiyo assignment akuangalizie soko kabla ya kufungua.

Nina mtu anafanya hiyo shughuli kila wiki lazima aagize mizigo.

Kuna kipindi baadhi ya vifaa vya keki katika Hilo eneo alipo huwa vinaisha kabisa Hadi Watu wanaenda mkoa ulio jirani nao kununua. Ambapo wakienda kwenye huo mkoa kununua gharama ni kubwa zaidi ya wewe ukiwaagizia. Au wakinunua kwako.

Pia nenda kariakoo kwenye maduka ya vifaa vya keki ukafanye uchunguzi wako zaidi na Zaid.

Assnte.
 
Nashukuru boss ubarikiwe
 
Amna ambacho hakiuziki mkuu learn how to sale kwanza ndio uingie sokoni, uhitaji bado upo tu. Tanzania ni miongoni mwa nchi ambazo hazijitoshelezi mahitaji ndio maana wanaagiza nje products, import rate is greater than export rate.
 
Back
Top Bottom