Tuseme za ukweli uji umekuwa common kwa sasa!....sijajua km kuna kipya!
Ningekuwa ndo mie Maathai ningeenda Katoro kuchukua vitenge vya bei chee!...kila kitenge sikosi 4000!.chukua kitenge kwa 18000uza kwa 25000
Habari za majukumu wanajamvi, matumaini yangu mnachukua taadhari dhidi ya janga hili la Corona.
Niende moja kwa moja kwenye mada. Mimi ni binti miaka 25 nimemaliza chuo mwaka wa tatu sasa sijabahatika kupata ajira rasmi ila nnajishughulisha na shughuli za hapa na pale mradi mkono uende kinywani.
Ninatamani kuanzisha biashara ya kuuza uji katika sehemu zenye watu wengi. Kwa sasa naishi Iringa. Malengo yangu ni kuwa na sehemu kama 10 za kuuza uji (sio ofisi bali vijana wa kutembeza katika maeneo hayo 10) asubuhi na jioni kwa mtaji wa sh 300,000.
Naomba kwa mwenye ujuzi au uzoefu au hata mawazo bunifu au ushauri wowote juu ya biashara hii.
Asante.
Uji sio common kijana nenda instagram mtafute mtu anaitwa habpap kaangalie biashara ya uji anavyofanya utaelewa
Sent from my iPhone using JamiiForums




Jutahidi ku manage hao vijana kwa uangalifu mkubwa unless watakuharibia kazi
Sent using Jamii Forums mobile app
Unatumia style gani kuuza huo uji?Nikutie moyo, mimi ni muajiriwa serikalini, Mshahara wangu kwa mwezi ni Tshs 2,800,000/=...Lakini naifanya hiyo biashara ya uji kwa mwezi napata Tshs 780,000/=. Gharama za uendeshaji ni Tshs 250,000/= kwa mwezi. Faida ya uji nayobakiwa nayo ni Tshs 530,000/=. Hivyo ada za watoto wangu Private school zinalipwa na hiyo biashara ya uji.
Pambana asikurudishe mtu nyuma
Unatumia style gani kuuza huo uji?
Unauza kwa kutembeza mtaan?
Au unauza kwenye banda?