- kuku wanapatikana kwa wingi masokoni au majumbani kwa wanaofuga.
- kuku wanauzwa kuanzia 6,500 hadi 8,000
- kuku mmoja anaweza kukatwa mara nne kwa kuuza ( mapaja mawili na vidali viwili). Ingawapia anaweza kukatwa hadi mara nane. Pia kuna viungo vingine kama shingo, kichwa, miguu, utumbo, firigisi utapata baada ya mikato hiyo.
- mtaji sio mkubwa. Andaa gharama ya meza nzuri ya kuuzia, jiko la mkaa, makarai ya kukaangia, mkaa, viungo, taa au koroboi kuweka mwanga unapouzia, kiti cha kukalia, vifungashio na vibebeo vya wateja wako mfano magazeti, au mifuko ya karatasi.
- Bei hutofautiana sehemu na sehemu lakini zinaweza kuwa kama mfano; TSH 200 hdi 500 kwa shingo, vichwa, miguu, na utumbo. Firigisi 500 hadi 700. Mapaja na vidali vinaweza kuwa 2,000 hadi 2,500.
- Maeneo mazuri ni karibu na vituo vya daladala vyenye abiria wengi wanaoshuka na wanaopanda, na karibu na makazi ya watu maana hivyo ni vitoweo vya mboga majumbani.
- Changamoto ni kama ushindani uliopo kwa wauza chips, kuuziwa kuku vibudu, chuma ulete, ushirikina wa wasiopenda maendeleo ya watu, mazoea ya baadhi ya wateja wa karibu wa kula siku mwishowe wanaanza kukopa, nk