Biashara ya kuuza kuku wa kukaanga

She Quoted you

JF-Expert Member
Oct 19, 2020
687
1,162
Habari wana Jf.

Mim ni mkazi wa Dar es salaam, ninataka kufanya hii biashara ya kuuza kuku wa kukaanga
Naomba kufahamishwa kuhusu.

1.Bei ya kuku wa kisasa + Maeneo wanayopatikana kwa wingi
2.Kuku mmoja anatoa vipande vingapi
3.Vipande vinauzwa sh. ngapi ngapi
4.Mtaji mzuri wa kuanzia hii biashara
5.Changamoto

Bonus:
Maeneo mazuri ya kufanyia hii biashara eg.Buguruni,Kimara,Gongo la mboto,Mbagala etc.
 
Wasubiri wa DSM sisi wa mikoani ngoja tuzibe midomo labda ikitokea uhitaji tutatoa tuu ushauri.
 
- kuku wanapatikana kwa wingi masokoni au majumbani kwa wanaofuga.
- kuku wanauzwa kuanzia 6,500 hadi 8,000
- kuku mmoja anaweza kukatwa mara nne kwa kuuza ( mapaja mawili na vidali viwili). Ingawapia anaweza kukatwa hadi mara nane. Pia kuna viungo vingine kama shingo, kichwa, miguu, utumbo, firigisi utapata baada ya mikato hiyo.

- mtaji sio mkubwa. Andaa gharama ya meza nzuri ya kuuzia, jiko la mkaa, makarai ya kukaangia, mkaa, viungo, taa au koroboi kuweka mwanga unapouzia, kiti cha kukalia, vifungashio na vibebeo vya wateja wako mfano magazeti, au mifuko ya karatasi.

- Bei hutofautiana sehemu na sehemu lakini zinaweza kuwa kama mfano; TSH 200 hdi 500 kwa shingo, vichwa, miguu, na utumbo. Firigisi 500 hadi 700. Mapaja na vidali vinaweza kuwa 2,000 hadi 2,500.

- Maeneo mazuri ni karibu na vituo vya daladala vyenye abiria wengi wanaoshuka na wanaopanda, na karibu na makazi ya watu maana hivyo ni vitoweo vya mboga majumbani.

- Changamoto ni kama ushindani uliopo kwa wauza chips, kuuziwa kuku vibudu, chuma ulete, ushirikina wa wasiopenda maendeleo ya watu, mazoea ya baadhi ya wateja wa karibu wa kula siku mwishowe wanaanza kukopa, nk
 
Habari wana Jf
Mim ni mkazi wa Dar es salaam
Ninataka kufanya hii biashara ya kuuza kuku wa kukaanga
Naomba kufahamishwa kuhusu
1.Bei ya kuku wa kisasa + Maeneo wanayopatikana kwa wingi
2.Kuku mmoja anatoa vipande vingapi
3.Vipande vinauzwa sh. ngapi ngapi
4.Mtaji mzuri wa kuanzia hii biashara
5.Changamoto

Bonus:
Maeneo mazuri ya kufanyia hii biashara eg.Buguruni,Kimara,Gongo la mboto,mbagala etc.
Tuwasiliane kuna location moja nzuri sana
 
Swali tu la kawaida kwanza kwako.
Kwani ww hujawahi hata siku moja kununua kuku wa kukaanga!?
 
- kuku wanapatikana kwa wingi masokoni au majumbani kwa wanaofuga.
  • kuku wanauzwa kuanzia 6,500 hadi 8,000
  • kuku mmoja anaweza kukatwa mara nne kwa kuuza ( mapaja mawili na vidali viwili). Ingawapia anaweza kukatwa hadi mara nane. Pia kuna viungo vingine kama shingo, kichwa, miguu, utumbo, firigisi utapata baada ya mikato hiyo.

- mtaji sio mkubwa. Andaa gharama ya meza nzuri ya kuuzia, jiko la mkaa, makarai ya kukaangia, mkaa, viungo, taa au koroboi kuweka mwanga unapouzia, kiti cha kukalia, vifungashio na vibebeo vya wateja wako mfano magazeti, au mifuko ya karatasi.

- Bei hutofautiana sehemu na sehemu lakini zinaweza kuwa kama mfano; TSH 200 hdi 500 kwa shingo, vichwa, miguu, na utumbo. Firigisi 500 hadi 700. Mapaja na vidali vinaweza kuwa 2,000 hadi 2,500.

- Maeneo mazuri ni karibu na vituo vya daladala vyenye abiria wengi wanaoshuka na wanaopanda, na karibu na makazi ya watu maana hivyo ni vitoweo vya mboga majumbani.

- Changamoto ni kama ushindani uliopo kwa wauza chips, kuuziwa kuku vibudu, chuma ulete, ushirikina wa wasiopenda maendeleo ya watu, mazoea ya baadhi ya wateja wa karibu wa kula siku mwishowe wanaanza kukopa, nk
Jibu zuri sana
 
3 Reactions
Reply
Back
Top Bottom