Sawa ila fahamu tu kuwa Biashara ya Genge haitaki Mtaji mdogo
Genge ni moja ya biashara zenye faida lakini ili uweze kudumu kweye biashara ya Genge,hautakiwi uwe na mtaji mdogo kama tunavyoaminishana,ni kweli vitu vya gengeni n vya sh.100,200 hadi 1000 vitu vinachezea humo lakini vitu hivi kumbuka unavinunua kwa jumla ili uviuze kwa reja reja.
ukisema genge linahitaji mtaji mdogo maana yake unasema mtu akienda kufungua genge, Basi anunue nyanya za 5000 anunue vitunguu vya 2000 karoti k za 5000,nk nk halafu aje auze apate faida..sidhan kama atatoboa.
hii biashara ili uone faida n lazima uingie ukiwa umejipanga,Uweze kununua vitunguu gunia,viazi gunia,na maviungo mengine pia,nk nk
Biashara ya Genge n biashara inayotaka kila siku uweke nyanya mpya,karoti mpya,hoho mpya ili hizi mpya ziweze kuuza zile za jana zilizosinyaa sinyaa,sasa utapata wapi hela ya kununua hoho mpya kama mtaji wako wa hoho uliishia jana kwa kuamini zingenunulika?
Biashara ya Genge ni nzuri lakni uzuri wa biashara hii ni kwa wale wenye mitaji,mtu sio una hela mawazo halafu unafungua genge (utakufa) katka biashara sishauri anaeanza ujasiriamali aanze nayo kama hana mtaji ni Biashara ya GENGE.
Ukiona muuza genge anasomesha,anajenga,anafanya maajabu halafu anakwambia Genge ndio kila kitu kwake Usifikiri alianza na mtaji Mdogo, hamna hiyo.