CONTROLA
JF-Expert Member
- Sep 15, 2019
- 7,087
- 23,868
👊sikupingi💪Biashara yoyote unayoifanya masaa 14 si mzuri
watakao elewa hii ni wachache sana ila huu n ukweli mchungu.
👊sikupingi💪Biashara yoyote unayoifanya masaa 14 si mzuri
Fafanua kidogo👊sikupingi💪
watakao elewa hii ni wachache sana ila huu n ukweli mchungu.
Haya mambo ndyo yanayo wafelisha watu washindwe kuthubutu.Kwanza lazima ufanye feasibility study, then uandae business, strategic na markerting plan.
Hapa umeandika kama anayeanza na 50K anapenda kumbe ndipo muscle yake ilipoishia.Viazi JE + Viungo vya chai na Pilau!? Akiba JE?! na pia Laki 3 unaanza sijakataa na
hata ukitaka genge la mtaji 50,000 inawezekana lakini swali ni kwamba upo serious
na hiyo biashara? Kama jibu ni "ndio" basi huwezi anza biashara ya mali kuoza na mtaji wa kusua sua.
SIO kila anaeanza biashara na mtaji mdogo ni kweli "kakosa mtaji mkubwa au hana" kuna watu biashara ipo damuni (hata mimi siingiii),wanapenda anzia chini chini chini,hawa raia ndio hata mimi nawaogopa,hawa sio watu nawafananishaga na marobotHaoa
Hapa umeandika kama anayeanza na 50K anapenda kumbe ndipo muscle yake ilipoishia.
Ni kweli asee,, ht mi nimefuatilia madam nyingi nimeiona hili jangaNilichogundua Watanzania kuja kuondokana na adha ya Umasikini sio leo. Mtu hata atoe ushauri mzuri namna gani lkn bado atatukanwa au kupewa kejeri. Any way hii labda inatokana na stress ambazo tuko nazo asee....!!!
Kwanza kabisa hii biashara inagusa hitaji la msingi la mwanadam ambalo ni chakula, ni lazima ule ili uweze kuishi na kila siku mahitaji yetu tunayapata sokoni, dukani au gengeni kwahiyo ni uhakika kabisa kuwa na wateja tena kila siku asubuhi mchana na usiku
Kingine nina rafiki yangu mimi ana hii biashara ndo inamuweka mjini anatengeneza faida nzuri sana na wateja wanamiminika kwa wingi sana na tips anazotumia ndo hizo hizo nilizoelezea hapo juu!!!!
Genge nyumbani kwako wakazi wa Dar tunakufikishia bidhaa zote za gengeni kwa Bei nafuuSwali 1:
Mimi ni mkazi wa Dar es Salaam, ningependa kufanya biashara ya kuuza genge, naomba msaada wenumwenye kujua naweza nunua wapi vitu vya sokoni kwa bei nzuri, na nikimuajiri mtu aniuzie inabidi nimlipaje?
Natanguliza shukurani..
Swali 2:
Pinkshlady
habari wana jf, nawazo lakuanzisha biashara ya genge, lakini la kitofauti kidogo na haya tuliyozoea, nikiwa na imani nitawateka watu wengi, sababu itakuwa karibu na barara kuu na paking ipo ya kutosha,
nikitarajia kuuza matunda ya aina zote, vitu vya sokoni, mayai, ikiwezekana na kuku.
Naomba ushauri wenu niwe na mtaji kiasi gani wa kuanzia? ni soko gani naweza kupata vitu kwa bei ya chini?
na kuna ulazima wa kuwa na leseni ya biashara?
Ushauri:
Hongera sana kiongozi kwa mawazo yako mazuri,ila biashara hii haiko hivyo unavyozani,kiufupi ni biaharayenye changamoto nyingi sana na imejaa fitina/ushirikina wa kila aina,ukiweza kujipanga(kwa Mungu/miungu) hapo sawa.Miongoni mwa biashara zenye hela nzuri ni biashara ya genge. Genge linataka mtaji mdogo lakini faida yake ni nzuri sana na kwa mtu anayetaka afanye hii biashara ni nzuri sana
Pia, ni biashara nzuri ambayo hautapata usumbufu wa TRA na pia hutowaza sana kuhusu wezi tofauti na biashara yengine
Cha kuzingatia ili biashara yako hii ya genge ifanikiwe:-
Kwanza unatakiwa uwe mtu social sana uwe unaongea na wateja vizuri pia uwe ni mtu wa tabasamu mteja akija wakati mwingine mfano kitunguu ni 200 yeye kaja na mia basi usisite kumpa kwa mia hii itamsogeza kwako
Kingine ni ubora wa bidhaa, chagua bidhaa zenye ubora na zenye mvuto mfano ukichagua nyanya bamia au nyanyachungu ziwe ni zenye ubora na mvuto hata mtu akipita akiziona azisiache .
Usiuze vitu ghali sana uza walau bei ya sokoni au inayokaribiana na sokoni ili hata mtu akiwaza unavyouza aone ni sawa tu na sokoni aone kwenda buguruni sokoni kununua nyanya ni sawa tu na kununua kwako maana unauza sawa tu na sokoni
Kingine ni kiwango cha bidhaa uzingatie usipunje wateja uza kama kiwango cha vipimo vya sokoni ili kumfanya mtu awe mtejawako wa kila siku aachane na mpango wa kwenda sokoni
Kwa mbinu hizi utapata wateja na utauza sana
Kila la kheri!
Mtaji wa laki sita vp mkuuHii biashara ukipata eneo zuri lenye watu inalipa.
Pia haihitaji mtaji mkubwa kama biashara nyingine.
Sent from my SM-A105F using JamiiForums mobile app
Kweli kabisaBiashara nzuri sana mbali na location na mtaji, pia kama unaajiri mtu usimueke kijana wa kiume....
Mana kuna wanawake wanakuja na mia tano but watataka warudi na vitu vya buku...
Nimepata eneo la uswahilini movement ya watu ipo i think wateja nao watakuwepoNi baishara nzuri ila tu upate eneo zuri kwasababu bidhaa zake zinatakiwa kutoka haraka sana ukizichelewesha zinakudodea.
Sent using Jamii Forums mobile app