Biashara ya kulaza magari(Parking) Dar

bukoba boy

JF-Expert Member
Jan 15, 2015
5,370
3,956
Hivi hii kitu imekaaje?

Ninaona zipo viwanja wanafanya hii biashara lakini bado hawapo kisasa zaidi na bado hawaaminiki sababu ya wizi wa magari au vipuri vyake.

Sehemu nyingi gharama ni 1000 kwa siku ila sidhani kama ukalaza gari hapo likaibiwa au kuhujumiwa kama wataweza kufidia sababu wengi ni wajanja wajanja tu.

Sasa ukapata eneo kubwa maeneo yasio na parking ukaweka utaratibu mzuri ,ulinzi masaa 24 kuna mfanyakazi/wafanyakazi wapo kuhudumia wateja.

Hili sio wazo zuri? Au kama wapo wanaotekeleza vp utekelezaji wake umekaaje?
 
Hili wazo zuri lakini lilikosa uchangiaji, vipi ulifanikiwa kuanzisha hii biashara?
Mimi nilikuwa kwenye kutafuta info kuhusu hii biashara ndiyo nikaja kuta hii nyuzi ya kitambo.
 
Kuna maeneo ya serikali ambayo yamegeuzwa sehemu za kupaki magari binafsi kwa faida ya maofisa binafsi. Mfano pale uwanja wa Arnatoglou na shule ya sekondari ya Gerezani. Kuna magari mamia kwa mamia yanawekwa hapo kwa malipo. Sina hakika fedha zinakwenda wapi lakini kuna harufu ya ulaji. Je TAKUKURU inalielewa hilo?
 
Back
Top Bottom