Kwangu mimi nilitaka tu kukupa ushahuri kuwa utakapokuwa umekamilisha ujenzi wa majengo ya mitambo na store basi nitafute nikupe ushahuri wa mashine, katika dunia ya leo hatutumii tena roller machine kwa kukoboa kwani inakuwa na wastage kubwa ya mahindi, wastani wa gunia la kilo 108 kgs kwa roller machine utajikuta unapata kg 75 au 78 za mahindi, lakini kuna mashine za kisasa output baada ya kukoboa inakuwa kg 92 hadi 95 ktk gunia la kg 108 hii inakupa faida kubwa na tija zaidi, ukiamua kutegeneza unga wa dona machine hii ndo yenyewe, capacity yake ipo ya ton 20 kwa siku, 30tons kwa siku hadi 50tons inategemea utaaamua kutumia hammer mill au vip, hata hivyo ktka kusaga kama utaamua kutumia hammer mill ni wakati mzuli kupata vinu vizuli vya kisasa kabisa vinavyotumia motor ya HP50 vinu 3 stainless steel unga unakuwa bora sana na sio carbon steel mill,
Haya bwana kazi ni kwako, thanks
OkNenda Mombasa mbele ya Magereza Ukonga sehemu inaitwa Madafu. Kuna Mhindi ana design Log na kuprint mifuko
Ndio kwa baadae !! Kwa sasa nilitaka nianze kidogo kwa kusambaza madukani kwanza kabla cjafanya kitu kikubwa Sijui kama hata hicho kitahitaj hizo process zote Mkuu??Soko ni nzuri sana ila jiandae kupata vibali vyote husika..TFDA, TBS, Business Licensing Authoriesties etc
Sawa sawa Mkuu!!Hapo kwenye sembe ongeza DONA ni muhimu kwa shughuli za wanaume na ikiwezekana familia nzima watumie dona kuepuka magonjwa ya utapiamlo
By experience!
Nenda mikoa ya Iringa au Mbeya, nunua mahindi moja kwa moja kwa wakulima, sogeza mahindi kwenye mashine ya kusaga iliyo karibu ili kupunguza carriage cost!
NB: hapa uwe umeshaongea na watu wa mashine, ikiwezekana uwe unawaachia pumba ili gharama ya usagishaji iwe chini zaidi (chini ya 5000/= kwa gunia)
Mahindi yakifika kiasi unachotaka, anza kusaga na kupaki(kwa kuanza unaweza kuwa unatumia mashine ya kushonea ya kukodi na mifuko yenye nembo ya mtu mwingine (mtafute)!
Gharama ya mfuko tupu usio na nembo ni around 200-350 bei ya jumla na 400-600 wenye nembo)
Kipimo kiwe kilo 5, 10, 25 na 50 (gharama ya upakiaji kwa makuli ni around 700 kwa kila kilo 50!
Tafuta magari yanayosafirisha mizigo mikubwa, ongea nao wakuunganishie mzigo wako kwa wasafirishaji wengine (madalali are so good in this)!
Mzigo ukifika mkoa wako wa soko waombe wakushushie sehemu ambayo ni rahisi kwako!
Zambaza mzigo kwa wateja wako!