Hii kitu nilishajiuliza.
Nikagundua kuwa kwa Bongo humu humu ndani huwezi kupata faida.
Nikaona eti labda kama unaenda kuuza dollar (USD) nchi za nje (mfano South Africa) unapata Rands (ZAR) halafu unazileta Tz kuziuza.
Niligundua hivyo baada ya kuona nikibadili USD zangu hapa Tz na kuwa ktk Rands napata Rands chache ukilonganisha na nikizibadili USD kiasi kilikile huko bondeni (South Africa).
Mfano:
Exchange rate kwa Tz (TZS) ikiwa:
USD - BUY 1,600: SELL 1,625
RAND - BUY 1,85: SELL 200
Kwa South Africa (ZAR) ikiwa:
USD - BUY 9: SELL 11
Fastjet (go & return): Dar - Jo'burg: Takribani 500,000 Tshs
Reference: (
https://www.jamiiforums.com/habari-...-mpya-ya-fastjet-from-tz-to-south-africa.html)
Kwa hiyo ukiwa na 48,750,000 Tsh unaweza kununua 30,000 USD (kwa bei ya 1,625 Tshs kwa kila 1 USD).
Unaenda kuziuza hizo 30,000 USD huko South Africa kwa Rands 270,000 (kwa bei ya 9 Rands kwa kila 1 USD)
Unarudi Tz ukiwa na hizo Rands 270,000 halafu unaziuza kwa 185 Tshs kila Rand, unapata 49,950,000 Tshs.
Ukitoa mtaji na gharama ya usafiri kwenda na kurudi unabaki na faida.
Faida ni: 49,950,000 - (48,750,000 + 500,000) = 700,000 kwa siku = 21,000,000 kwa mwezi.
Hata ukisafiri kwa nusu ya siku zote kwa mwezi, tuseme upate faida ya 10,000,000 Tshs kwa mwezi.
Lakini kumbuka:
(1)Kuna sheria na taratibu za kimataifa za kusafirisha pesa. Hapa nd'o palinichanganya kidogo, lkn ninaamini HAPA ND'O UFUNGUO WA HIYO BIASHARA ULIPOKAA (This may be the place where the right key for this business is hidden).
Reference: IATA - International Air Transport Association
(
IATA - South Africa Customs, Currency & Airport Tax regulations details)
(2)Kuna madhara ya mionzi kwa wale wanasafiri kwa ndege mara kwa mara (Ionising radiation).
Reference: (
ARPANSA - Cosmic radiation exposure when flying)