Kama unataka kufungua internet cafe lazima ujifikirie mara mbili.
Kutokana na ongezeko la simu za kisasa zenye uwezo wa internet na makampuni kupunguza bei za internet imechochea biashara ya internet cafe kudorola.
Zamani internet cafe ata za uswahilini zilipata wateja.
Ukifungua internet cafe kwa sasa ili ufanikiwe inabidi ufungue sehemu zenye wanafunz au mzunguko wa watu wengi na uweke vitu vingi.
Gharama za uendeshaji internet cafe zimekuwa kubwa kuliko kipato.
mfano wa gharama hizo kama za kodi ya chumba, internet service provider, umeme, TRA,kulipia bango au maandishi, matengenezo ya computer, mshahara wa mfanyakazi.
umeme kukatika hovyo hovyo kunadumaza na kuleta hasara
Hivo kabla ujafungua internet cafe fikiria mara mbili mbili