Biashara ya gym, vifaa vyake na changamoto zake

kj75

JF-Expert Member
Feb 17, 2019
491
590
Habari wanaJF.

Ni matumaini yangu kuwa hamjambo wote na mnaendelea vizuri na shughuli zenu za kila siku naomba kupata wenye uzoefu na hii biashara ya gym iko je, nataka nifungue sehemu fulani hivi.

Jamani msaada wenu asante.

1623995126254.png

1623995491483.png

Sijamuona mtu ametoboa kwa biashara ya gym, labda ufanye kama passion/hobby.
 
Me mtu wa mazoezi, ila inalipa Sanaa mkuu, japo Ni ghalama mwanzoni , Fungulia uswahilini ndio utapiga pesa
 
Sijamuona mtu ametoboa kwa biz ya gym, labda ufanye kama passion/hobby.
We nadhani ujawaia kufanya hata ayo mazoezi yenyewe,, gym zinalipa, ila Gym fungulia uswazi fulani, sio hizi ambazo babkubwa sana ,, fungulia uswahilini ndio unapiga pesa
 
We nadhani ujawaia kufanya hata ayo mazoezi yenyewe,, gym zinalipa, ila Gym fungulia uswazi fulani, sio hizi ambazo babkubwa sana ,, fungulia uswahilini ndio unapiga pesa
Sawa mfanya mazoezi wa uswazi.
 
Sawa mfanya mazoezi wa uswazi.
Me nna gym mbili maeneo Kama ayo dada, nna experience na nnachokisema, na nikisema uswazi simaanishi uswazi unayoijua wewe, yaani watu wa mazoezi wanaziitaga local gym, kiingilio elfu 3,na kwa kulipia mwezi 70,000, kwa siku huwa hawakosekani watu 20 mpk 30 wastani, wale wa ingia toka, umeme kwa mwezi elfu kumi tu, Kuna siku idadi inazidi zaidi,
 
Tengeneza gym classis,watakuja watu wa maana na ndiyo wenye uwezo wa kulipa,katika magym kuna biashara nyinhine binafsi nyingi tu hufanywa,ikiwa location nzuri, na gym nzuri utapata wateja sana maana zitakuja piss kali na magentlemen pia,si unajua kuku habanfuki penye mchele.
 
Me nna gym mbili maeneo Kama ayo dada, nna experience na nnachokisema, na nikisema uswazi simaanishi uswazi unayoijua wewe, yaani watu wa mazoezi wanaziitaga local gym, kiingilio elfu 3,na kwa kulipia mwezi 70,000, kwa siku huwa hawakosekani watu 20 mpk 30 wastani,wale wa ingia toka, umeme kwa mwezi elfu kumi tu, Kuna siku idadi inazidi zaidi,
Sawasawa mke wangu.
 
Naomba kujua vifaa vyake vinapatikana wapi Na Bei zake zikoje???
 
Ikwa na vifaa vya kutosha kama vile dumbbells uzito tofauti hata seti 5 , bench 2 za chest, za triceps, z bar za biceps...

Zingatia na watu wa aerobics hasa wakina dada jkiweza kuwateka itapendeza zaidi...
Maana hawa hufanya mazoez siku mbili tatu na kupotea wakipata maumivu😂😂 inabidi uwape elimu kadri wanavyofanya ndio mwili huzoea!

Bjnafsi iwe local gym , au ya kisasa zowte zinalipa kila moja kutokana na uwekezaji wake.

Za kisasa bei kiwango cha chini ni kati ya Tshs 10,000 /siku , 150,000/mwezi.

Local gym bei kiwango cha chini ni kati ya Tshs 2,000 /siku , 30,000/mwezi.

Ni biashara inayolipa sana, ukisimamia vizuri
Vifaa vya kutosha , marketing nzuri, mazingira mazuri ya kufanyia mazoezi.

Inalipa kuliko hata mtu aliyejenga vyumba vitano uswazi akodishe kwa Tshs 50,000/=

Maintenance yake ni ndogo , local gym utahitaji si chini ya 3mil+ kwa kuanzia
 
Me nna gym mbili maeneo Kama ayo dada, nna experience na nnachokisema, na nikisema uswazi simaanishi uswazi unayoijua wewe, yaani watu wa mazoezi wanaziitaga local gym, kiingilio elfu 3,na kwa kulipia mwezi 70,000, kwa siku huwa hawakosekani watu 20 mpk 30 wastani,wale wa ingia toka, umeme kwa mwezi elfu kumi tu, Kuna siku idadi inazidi zaidi,
Kiasi gani unatengeneza kwenye gym moja?
Faida ioo kwa wateja wa siku au mwezi?
 
Kwanza mkuu inategemea na eneo lenyewe lina ukubwa kiasi gani na kama ni kubwa basi ni vyema ukaweka complete gym set up
kama ni la size unaweza weka incomplete lakini basic equipment kama zifuatazo lazima ziwepo

1: Full dumbell set(in libs, 5lb-50lb) hii utapata na rack yake

2: barbell rack complete set (30lbs-110lbs)

3: Cardio machine kama aina nne i.e trademills, bicycles,na nyingine na brand nzuri ni lifefitness au startrac

4: Bench press na mawe yake hii inakuwa na accurate weight 5kg-105kg unaweza pata ya zaidi ya hapo i recommend smith machine

5; Machine nyingine kama za miguu,tumbo, hizo unaongeza moja baada ya nyingine kutokana na mwamko wa biashara hiyo. Na uzuri mashine nyingi za sasa hivi zinakuwa multifunctional

6: Ruberized floor muhimu carpet lile mpira

Kingine unatakiwa kuangalia ni mazingira ya goli lenyewe gym lazima iwe kaeneo ka town town kidogo hasa penye makazi yaliyochangamka in short mahali panaingia ingia ugeni

Markerting/ advertising hasa ki digital inaweza kukuza biashara ya gym hasa eneo likiwa salama na accessible. Sale inaweza kuwa ya kwa siku.kwa mwezi, miezi 3,6 hata mwaka ukipenda ni wewe na bei utakayopanga. unaweza kaba kuanzia single membship, couple/double/family.

Kila kitu kikisimama ni bora zaidi ukasimamia mwenyewe mpaka utakapopata mtu unaemwamini
Wasalam hiyo ndo maarifa kidogo niliyo nayo juu ya gym
 
Back
Top Bottom