Biashara ya simu na vifaa vyake kutoka China

Betterhalf

JF-Expert Member
Dec 20, 2016
2,879
2,554
Hello, habari wana jamvi.

Nina ndoto ya kufanya biashara ya kuagiza ama kwenda kununua mzigo China hususan simu na vifaa vya simu.

Naomba kujua na kupata ushauri wenu, nahitaji;
1. Mtaji kiasi gani?
2. Gharama za safari (kama itanilazimu kusafiri)
3. Itanichukua muda gani aidha nikisafiri ama nikiagizia kufanikiwa kurudi ama kupokea mzigo Tanzania
4. Mambo mengine muhimu ninayotakiwa kuwa nayo ukiondoa hoja kama leseni, fremu n.k.

Naomba kuwasilisha.

Ahsante sana.
 
Ngoja tuone...hii iwe sababu ya wenye ndoto ya biashara hii tuweze kupata fursa ya kuifanya hii biashara.
 
kaka mshana alikuwa anawaunga watu wajasiriamali kwenda china sasa jaribu kuonana nae kama wameshasafiri au la au ujue utaratibu wao
 
Hello, habari wana jamvi.

Nina ndoto ya kufanya biashara ya kuagiza ama kwenda kununua mzigo China hususan simu na vifaa vya simu.

Naomba kujua na kupata ushauri wenu, nahitaji;
1. Mtaji kiasi gani?
2. Gharama za safari (kama itanilazimu kusafiri)
3. Itanichukua muda gani aidha nikisafiri ama nikiagizia kufanikiwa kurudi ama kupokea mzigo Tanzania
4. Mambo mengine muhimu ninayotakiwa kuwa nayo ukiondoa hoja kama leseni, fremu n.k.

Naomba kuwasilisha.

Ahsante sana.
Mkuu vip ulifanikiwa?
 
Nimesoma huu uzi nikasikitika.Kuagiza Mzigo china siku hizi unaweza kufanya online.Ila inategemea na Thamani ya Mzigo na aina ya Bidhaa.Kama Ndio Unaanza kuna majukwaa kama Aliexpress,Alibaba,Made in China.com na Mengine mengi.Unachotakiwa kufanya kwanza ni kuamua aina ya bidhaa kisha tembelea hayo majukwa ufanye window shoping na kuanzisha mawasiliano na watu walioko China ambao wanauza bidhaa kwenye hayo majukwaa.

Pili utahitaji kuwa na mawasiliano ya watu wa usafirishaji.Hapo inabidi uwafahamu.Baadhi ya Kampuni za usafirishaji zina mawakala wao Kule China ambao unaweza kuwatumia kwenda kukagua mzigo wako kabla ya kulipa,kuonana na wako n.k.Unapoagiza kwa mara ya kwanza usiagize mzigo mkubwa.Agiza kama Samples Tu.Hii itakusaidia kuona ubora wa bidhaa,kufahamu gharama za usafirishaji,muda wa mzigo kukufikia,gharama za kodi na tozo.

Zingatia kwamba Mitandaoni kuna matapeli lakini pia kuna wafanyabiashara ambao ni genuine.Epuka sana vitu ambavyo ni nafuu sana kuliko uhalisia wake.Epuka Kununua bidhaa kwa muuzaji ambaye rating zakesi nzuri.Epuka kununua bidhaa ambazo huelewi mteja wake atakuwa nani.
 
Back
Top Bottom