Biashara ya Duka Mwanza ni mzigo

Biashara ya Duka Mwanza ni mzigo

Super H

JF-Expert Member
Joined
Oct 6, 2012
Posts
1,070
Reaction score
405
wakuu salaam sana .
mimi ni mfanyabiashara hapa mwanza ila hizi biashara za duka sio dili tena kwani serekali yetu sikivu imeitolea macho na huwezi pata faida.
Tra mashine ni 800,000
jiji leseni 200,000 na kuendelea hadi 1m
kodi ya pango ndio balaa hadi 8m kwa mwaka,mapato Tra kwa mwaka 1M na zaidi .
.kodi ya usafi kila mwezi 8000
_ni afadhali uwe machinga kuliko kuwa na duka hapa mwanza !
tufanye shughuli gani wakuu kwani hata bidhaa kuingiza nchini bandarini tra wanacharge bei juu sana na hivyo walaji wanashundwa kumudu.
 
Pole mkuu ndio Serikali yetu sikivu, lakini mwisho wa siku anaeumia ni mtumiaji wa mwisho ambae ni mwananchi wa kawaida.!!
 
wakuu salaam sana .
mimi ni mfanyabiashara hapa mwanza ila hizi biashara za duka sio dili tena kwani serekali yetu sikivu imeitolea macho na huwezi pata faida.
Tra mashine ni 800,000
jiji leseni 200,000 na kuendelea hadi 1m
kodi ya pango ndio balaa hadi 8m kwa mwaka,mapato Tra kwa mwaka 1M na zaidi .
.kodi ya usafi kila mwezi 8000
_ni afadhali uwe machinga kuliko kuwa na duka hapa mwanza !
tufanye shughuli gani wakuu kwani hata bidhaa kuingiza nchini bandarini tra wanacharge bei juu sana na hivyo walaji wanashundwa kumudu.

mkuu una duka gani??la spare??la vifaa vya ujenzi??la nguo??
 
upo sahihi kwa wale wafanyabiashara tumekuelewa. TRA wanachojua kukamua tu wengi wanafunga biashara.
unatumia million 1 kwa mwezi wakat faida laki 3.hali si nzuri kwa wengi si wewe tu.
 
Tatizo wafanyabiashara hatuna jukwaa PLATFORM ya kutusemea/ kututetea Mbona hali hii imeanza karibia miaka mitatu sasa. labda tuwaombe wanasiasa na sisi wafanyabiashara tuwe na wawakilishi bungeni, tuombe katiba mpya itutambue , pili labda tuandamane, Vilevile TRA ndio lengo lao kuu KUFILISI WAFANYA BIASHARA WAZAWA wanasema wazi kuwa sisi ni wasumbufu mfano mapato yako kwa mwaka ni sh 8 million, mtaji 50 million wanafanya AUDIT baada ya miaka 3 wanakudai sh million 300 (mia tatu) ,, VAT, SDL, PAYEE, Income Tax, na kila kimoja wanaweka ma penalty, pia hakuna hesabu yeyote yako wanayoitambua bali ya kwao tu ya kutoka formula za mitaani, na vitisho kibao... TRA ni JAMBAZI aliyehalalishwa na serikali na naamini watu wengi sana wanafilisiwa na TRA na hata KUUWAWA na pressure za hawa MAJAMBAZI....
 
nina duka makoroboi la nguo na mlangoni machinga wanauza nguo hizohizo sasa embu nishaurini nifunge duka niwe machinga kwani wao hawana garama yeyote
 
nina duka makoroboi la nguo na mlangoni machinga wanauza nguo hizohizo sasa embu nishaurini nifunge duka niwe machinga kwani wao hawana garama yeyote

Pole sana, hii naona kote gharama za uendeshaji ni kubwa sana, hapo Mwanza maduka naona yamewazidi wateja, na kazi imekuwa ngumu.
 
wakuu salaam sana .
mimi ni mfanyabiashara hapa mwanza ila hizi biashara za duka sio dili tena kwani serekali yetu sikivu imeitolea macho na huwezi pata faida.
Tra mashine ni 800,000
jiji leseni 200,000 na kuendelea hadi 1m
kodi ya pango ndio balaa hadi 8m kwa mwaka,mapato Tra kwa mwaka 1M na zaidi .
.kodi ya usafi kila mwezi 8000
_ni afadhali uwe machinga kuliko kuwa na duka hapa mwanza !
tufanye shughuli gani wakuu kwani hata bidhaa kuingiza nchini bandarini tra wanacharge bei juu sana na hivyo walaji wanashundwa kumudu.

Mkuu pole sana ndugu yangu kwa mashambulizi hayo makali! Kwenye kilimo hivyo vinyonya faida tunaviita PESTs ni wadudu, magugu na magonjwa, na yako manyonyaji mengine makubwa yanaitwa VERMINES ni nguruwe, nyani, ngedere na wezi (watu)!! Umemalizia vizuri sana post yako kwa kuuliza vizuri sana hapo kwenye RED!!

Ni kwamba dunia ndivyo ilivyo, kila unakogeukia kwenye kutafuta riziki huwa kunachangamoto zake, kila alie kwenye shughuri yake akichanganywa na changamoto huanza kuhisi labda shughuri zingine zinanafuu! Ukienda kwenye shughuri nyingine unakuta nako watu wanalizwa na yaliyoko huko.

Mkuu nakualika jaribu na kilimo cha mazao ya chakula! Mkuu afadhari ya Pests wa Kilimo kuliko pest wa biashara rasmi! Kama unaweza kumudu kilimo cha umwagiliaji, kilimo bado ni eneo halijaingiliwa sana na Human PESTs (watoza kodi, ushuru, n.k), kwa wanaofanya kilimo kwa kutumia utaalamu na technolojia kilimo hakifanyiwi fujo sana kama ilivyo kwa yule anayeanzisha biashara ya mtaani! Ukianzisha biashara ya mtaani inakuwa kama umeleta mzoga kwenye Fisi wengi. Ni unagombaniwa kama mpira wa kona!! Msiogope Kilimo hasa cha mazao ya chakula, mkitumia utaalamu na kwa kilimo cha umwagiliaji mtaweza kuepukana na hao wanyonya damu, ila tatizo na nyinyi mmezoea kukaa mijini mno hapo basi ndiyo ugumu ulipokalia! Angalizo* (Usiguse mazao ya biashara kama pamba, kahawa, tumbaku, huko hayo mazao wakulima wanafanyiwa mizengwe sana kwenye bei na wanafanyiwa dhuluma sana kweye malipo, fuatilia kasheshe za wakulima wa korosho ni vilio tu)
 
nimekukubali mkuu Kubota sina shamba hapa town japo natamani sana kulima
 
Last edited by a moderator:
Na ni afadhali hayo mapato wanayokusanya wananchi wafaidike bali wao wanazidi kunenepa vitambi
 
Hata mm nilitaka kufungua duka,lakin kama mchezo ndio huu,ngoja niwazue tena.
 
Mwanza ipi kama ni hii niliyopo sidhani,,kwanza kuwa mbunifu,pili biashara fanya kwa ujanja na ubabe,,tatu kiroho/kiimani uwe juu,wa mwanza wanalijua hili,,mwanza pesa ipo mingi tena sana,,,
 
wakuu salaam sana .
mimi ni mfanyabiashara hapa mwanza ila hizi biashara za duka sio dili tena kwani serekali yetu sikivu imeitolea macho na huwezi pata faida.
Tra mashine ni 800,000
jiji leseni 200,000 na kuendelea hadi 1m
kodi ya pango ndio balaa hadi 8m kwa mwaka,mapato Tra kwa mwaka 1M na zaidi .
.kodi ya usafi kila mwezi 8000
_ni afadhali uwe machinga kuliko kuwa na duka hapa mwanza !
tufanye shughuli gani wakuu kwani hata bidhaa kuingiza nchini bandarini tra wanacharge bei juu sana na hivyo walaji wanashundwa kumudu.

Mkuu, hiii Tanzania ukijifanya mlokole unakufa na njaa, BIASHARA YAKO ITAKUFA! Leseni zamani ilkuwa bure, sasa wanachaji pesa lukuki, tena ni kila mwaka, TRA wanakukadiria wanavyopenda wao, tena hiyo KODI unailipa KABLA haujafanya biashara (malipo kabla), yaani kiujumla TRA hawako kuona unakua kibiashara, ukiwaeleza halihalisi ya biashara yako ilivyo ngumu wanakuambia FUNGA BIASHARA!!!!!....yaani siyo wawe friendly mjadiliane namna gani inakuwa wao wanakuwa wakali na roho mbaya na kuomba rushwa, wao wanajua mfanyabiashara mara zote anatengeneza faida. USHAURI WANGU MKUU NAKUSHAURI FANYA LOLOTE LIWEZEKANALO KPUNGUZA GHARAMA KWA JINSI YOYOTE, KAMA WAO WALIVYO MAFISADI NAWE KUWA FISADI, UJASIRIAMALI UMENIFUNZA MAMBO MENGI SANA!
 
mlangoni machinga wanauza nguo hizohizo sasa embu nishaurini nifunge duka niwe machinga kwani wao hawana garama yeyote
Super H

Mmachinga yeye ameingizaje huo mzigo bandarini, au kokote alikoupata, bila kulipia kodi?
 
Super H

Mmachinga yeye ameingizaje huo mzigo bandarini, au kokote alikoupata, bila kulipia kodi?

Mmachinga halipii leseni, kiwango cha chini leseni duka la nguo kwa sasa ni 150,000/= kwa mwaka
Mmachinga halipi mapato, kiwango cha chini mapato duka la nguo lenye umri wa miaka mitatu ni zaidi ya 400,000/=
Mmachinga halipi pango, makoroboi pango chumba cha ukubw wa kawaida inweza kuwa laki 500,000/= Kwa mwezi
Mmachinga halipi bili ya umeme
Mmachinga halipi ada ya usafi
Mmachinga halipi mfanyakazi

Kwa ujumla kama umefanya biashara hata kidogo utaelewa nini namaanisha, mfanyabiashara wa kati ndiyo mlipaji mkubwa wa kodi hapa Tanzania, mapato mengi ya TRA yanatoka huko, hawana ubavu wa kuwafuata wafanyabiashara wakubwa, wanawahonga na wanakwepa kodi mpaka utashangaa, ndiyo maana watu wanakimbilia kufanya biashara haram kwa sababu ZINALIPA, hazina mikodi ya ajabu! Biashara nyingine inayolipa na haina usumbufu ni KILIMO, twendeni tukalime wakuu. Sijui Kahtan Ahmed ataweza?
 
Last edited by a moderator:
Mmachinga halipii leseni....
Nimekuelewa vizuri kabisa..

Lakini siko huko kwenye leseni na pango na kadhalika, nataka ku focus kwenye jambo lifuatalo, awali ya yote.

Nauliza hivii, competitor wako Mmachinga, ambae mmesema anauza bidhaa hizo hizo, yeye analipaje kodi ya kuingiza bidhaa nchini au anaikwepaje? Maana mmesema Mmachinga hana gharama yeyote.
 
Mmachinga halipii leseni, kiwango cha chini leseni duka la nguo kwa sasa ni 150,000/= kwa mwaka
Mmachinga halipi mapato, kiwango cha chini mapato duka la nguo lenye umri wa miaka mitatu ni zaidi ya 400,000/=
Mmachinga halipi pango, makoroboi pango chumba cha ukubw wa kawaida inweza kuwa laki 500,000/= Kwa mwezi
Mmachinga halipi bili ya umeme
Mmachinga halipi ada ya usafi
Mmachinga halipi mfanyakazi

Kwa ujumla kama umefanya biashara hata kidogo utaelewa nini namaanisha, mfanyabiashara wa kati ndiyo mlipaji mkubwa wa kodi hapa Tanzania, mapato mengi ya TRA yanatoka huko, hawana ubavu wa kuwafuata wafanyabiashara wakubwa, wanawahonga na wanakwepa kodi mpaka utashangaa, ndiyo maana watu wanakimbilia kufanya biashara haram kwa sababu ZINALIPA, hazina mikodi ya ajabu! Biashara nyingine inayolipa na haina usumbufu ni KILIMO, twendeni tukalime wakuu. Sijui Kahtan Ahmed ataweza?

Naona machinga mambo yao mengi chee kabisa, mi nakushauri uwe machinga. Tatizo hoja yako kuu hapa si gharama za uendeshaji, ni machinga. Unatamani hata mgambo washushwe sasa hivi. Una chuki na machinga, sasa ukiwakataa wao wakale wapi? Kumbuka wana familia Kama wewe, wanataka kutoka kama wewe. Cha msingi walalamikie magamba make sera zote za uendeshaji wa Serikali zipo chini Yao.
 
Last edited by a moderator:
Back
Top Bottom