Biashara ya Duka la Rejareja: Ushauri, Mchanganuo, Changamoto na Namna ya Kutunza Kumbukumbu

Sijui mie nimezowea kununua maduka ya wapemba
Na yana wateja
Prestige ni nzuri kuliko blueband

Wanapima kwenye kilo, unanunua ile ndoo unapima ina kilo ngapi unaangalia bei uliyonunulia kisha utaangalia utauzaje upate faida
Asante sana
Hapo kwenye blue band sijakuelewa, make kule umetaja unga wa prestige.
Mi najua kweli ile prestige ambayo tunapikia na nyingine tunapaka kwenye mikate.

Huo 'unga' unatumika kwa mapishi ya nini?
 
Asante sana
Hapo kwenye blue band sijakuelewa, make kule umetaja unga wa prestige.
Mi najua kweli ile prestige ambayo tunapikia na nyingine tunapaka kwenye mikate.

Huo 'unga@ unatumika kwa mapishi ya nini?

Mmmh aisee wewe, Sijui wapi nimesema unga wa prestige

Prestige ya kwenye kindoo cha lita kumi, wenye maduka huwa wanauza kwa kupima kwa kilo ama nusu ama robo kulingana na mahitaji ya mteja.

Maziwa ya unga ya cowboy, unanunua mfuko ule nadhani ni kg 25 unakuta unauza kwa kupima kwa kilo

Mimi Hornet nauza unga wa lishe tu, ndiyo bidhaa niliyoomba nimpelekee jamaa dukani kwake.
 
Mkuu Ibravo,
Kwanza kabisa nikukaribishe humu maana unaonekana umejiunga humu this month hivyo you are still junior member, kwa kifupi humu kuna changamoto nyingi na shauri nyingi ambazo hata nyingine zinaweza kukukatisha tamaa kabisa au hata kujuta kuwa hivi nani alikushauri kuingia humu na ku-post threads za hovyo hovyo (wachangiaji wengine wanaweza kuziona hivyo), leo nikupe changamoto moja juu ya hii thread uloleta hapa:

Ibravo, sina nia ya kukukatisha tamaa juu ya mpango wako wa kuanzisha biashara ya duka hilo kwa capital hiyo ambayo umebahatika kuipata, ila to be honest nimeshangazwa na kusikitishwa na wazo hili kutoka kwako (msomi/graduate mtarajiwa). Naomba niseme wazi kuwa elimu unayosoma haijakusaidia chochote na nadhani ulikuwa unapoteza muda huko au labda ulikosea fani ulokuwa unasomea, wapo vijana wengi wanaenda vyuoni kusoma kwa mkumbo tu bila kujua anakwenda kusomea nini hasa. Lakini nadhani hapa ni uelewa wako tu ndo maana una wazo la kujiajiri, vinginevyo ningekulaumu kwa namna tofauti.
Nina imani watajitokeza wana JF wengi ambao wakisoma mchango wangu huu hawatanielewa, ila acha tu niseme ulonilazimisha kusema hasa baada ya kusoma uzi wako Ibravo.
Hata kama tunasema UJASIRIAMALI, inawezekanaje MSOMI/GRADUATE mtarajiwa unatoka chuoni unapewa mtaji wa mil 1, then unakurupuka na wazo la kufungua duka la kuuza UNGA, MCHELE n.k (UCHUUZI)? hivi hapa tutasema shule/elimu imekusaidia??? Na hapa niseme kuwa kama vijana wengi mnaenda vyuoni mnalipa fees huko miaka 2,3-4 nakuendelea, mnamaliza mnakuja na mawazo ya namna hii huku mitaji ya kiasi hiki mnabahatika kupata then niseme wazi kuwa elimu itakuwa haijawasaidia. Haya ni mawazo MGANDO, mtu unataka kufanya kitu kwa mazoea tu kwa kuwa watu wanafanya, huu si UJASIRIAMALI, ujasiriamali ni uwezo wa kubaini fursa kulingana na mtaji ulionao.
Nafurahia sana na watu wanaokuja humu kuuliza ili wapate mawazo kutoka kwa wachangiaji wanaJF great thinkers, wengine wanaenda mbali zaidi kwa kutamka kiasi (initial capital) alichonacho na anaomba ashauriwe afanye shughuli gani, watu wanatoa ushauri ktk shauri hizo wanasema AKILI YA KUAMBIWA, CHANGANYA NA ZAKO, then unapata shughuli ya kufanya. Ibravo nimesema sina lengo la kukukatisha tamaa ila nakueleza tu ya moyoni, wewe umeleta hapa wazo ambalo tayari unalo kichwani ndo maana watu wameshindwa kukushauri ila nina imani wengi wamekushangaa GRADUATE mtarajiwa unaleta wazo la namna hii hapa. Shughuli unayotaka kufanya hata ambaye hajasoma anafanya tu, ni UCHUUZI huo. Nilitegemea msomo uje na wazo tofauti kabisa kwa mtaji huohuo kwa kuwa kwa mjasiriamali wa kweli mil. 1 ni mtaji tosha tu.
Baada ya kukueleza haya sasa nakupa wazo, unaweza kulichukua au ukaliacha integemea kama umenielewa au utaniona nimeku-dis sana;
Kwanza kabisa kwa kuwa umesoma inabidi uwe na mawazo mchemko si mgando, inabidi uwe tayari kutoka mjini kwa kuwa kwa wazo lako ulilo nalo unaonekana unaishi ama unataka kuishi mjini tu, kwa mjasiriamali hili halimfungi kwa namna yoyote.
Pili inabidi uondokane na mawazo ya biashara hizi za UCHUUZI, jaribu kufikiria mawazo ya ki-uzalishaji zaidi, (kilimo, ufugaji, viwanda n.k) na siyo duka, kwa mtazamo wangu miye kuwa na duka la kununua na kuuza (UCHUUZI) ni uvivu wa kufikiri tu, hivi uliona wapi Mzungu anauza duka bwn? Hizi ni kazi za Wahindi, ni wavivu wa kufikiri tu. Sisemi Wazungu ndo bora sana ila walio wengi wana mawazo bora, yeye anafikiria akutengenezee SIMU, uwasiliane na jamaa zako, ukishaona umuhimu wake utamtafuta tu ununue kwake na hapo utaona WAVIVU WA KUFIKIRI aka WACHUUZI wanapanga foreni kiwandani kwa Mzalishaji kuweka order ya handsets za simu, JAMAA ANAPIGA HELA. MZALISHAJI anatengeneza kitu BORA kwa kuwa anajua WAVIVU WA KUFIKIRI/WACHUUZI watamsaidia (bila wao kujua) kuuza bidhaa zake.
Ibravo nimesema sikukatishi tamaa ila ningekukubali kama ungekuja hapa na wazo kuwa kwa kuwa umeenda shule basi ungeuliza humu kuwa una mtaji wa hela hiyo (1mil) then unataka kulima Mahindi, Mpunga n.k (kwa kuwa unaonekana una interest na vitu hivyo) then upate sasa mawazo ya GREAT THINKERS. Asikwambie mtu, KILIMO ni moja ya UZALISHAJI na si UCHUUZI, wewe lima tu kitaalamu, vuna mazao yako, utaona WACHUUZI wanakuja wenyewe kutaka kuuza bidhaa zako, we unapiga hela tu unakuna kitambi (unajua tena wabongo kwa vitambi) na nikupe siri, Tsh. 1,000,000/= kuwekeza kwenye kilimo ni mtaji mkubwa mno (kama upo tayari kuondokana na mawazo ya kukaa mjini).
Huku kwetu kukodi heka moja ni Tsh. 30,000 hadi 45,000 kwa mwaka na huku kwetu kwa mwaka tunalima mara mbili (mvua za vuli na masika), kwa hela ulonayo utakuwa na heka za kutosha, sema anza na heka 5 ambayo itakugharimu Tsh. 225,000/= kukodi tu mashamba. kulima kwa tractor kila heka moja ni tsh. 40,000 x 5= 200,000/= zinazobaki fanya matumizi mengine kama palizi, mbolea na matumizi mengine kama hayo, hapa bro unazungumzia miezi mitatu tu kama ume time mvua za vuli tayari utakuwa na magunia yako 5x15= 75 ya mahindi, huku kwetu wakati wa msimu wa mavuno gunia la mahindi linauzwa Tsh. 45,000/= x 75= 3,375,000/=, kumbuka hapa umelima mvua za vuli tu, utaingia tena shambani mwezi Feb ili u-tme mvua za masika, na hakuna tena gharama ya kukodi maana ni ileile ulolipa awali, mwezi wa sita tena unavuna mazao yako unasubiria WACHUUZI tu, unapiga hela. Mkuu ukikomaa ki-jasiriamali baada ya miaka michache nina uhakika mashamba hutakodi tena, utakuwa na ya kwako, utaanza ufugaji, maana kuna uzi wa MALAFYALE Jukwaa la Ujasiriamali unasema 'Kilimo na Ufugaji kwa pamoja vinalipa' nenda kasome pale uone GREAT THINKER wanavyokuwa na mawazo ya ki-GT.
Kwa leo mkuu.
Naomba kufahamishwa kwa mwenye kujua duka la rejareja la kuuza mchele, juice na kadhalika linaweza kuitaji mtaji kiasi gani

Ibravo post:
Habari zenu Wana Jamii Forum,

Mimi ni mwanafunzi wa chuo mwaka wa tatu,katika harakati za kujiandaa na kupambana na maisha pindi nitakapohitimu elimu yangu na kurudi mtaani,nimetafuta pesa ikiwa kama mtaji wa biashara milioni moja (1,000,000)hasa ya duka la bidhaa za vyakula.

Tatizo ni kwamba si mzoefu ktk biashara na ni mara ya kwanza kutaka kuifanya hii biashara kwan matarajio yangu ni kujiajiri mwenyewe.

Naomba ushauri kwa yeyote mwenye uelewa kuhusu hili kunipa mchanganuo wa bidhaa muhimu zinazotakiwa kuwepo dukani kama vile unga kiasi gani,mchele n.k kulingana na mtaji huo wa Milioni Moja.

Natanguliza Shukrani zangu.


================================================
MAJIBU KUHUSU BIASHARA HII
================================================
asante
 
Nilifanikiwa mkuu naendelea mdogo mdogo. Kifupi bidhaa huwa nanunulia maduka ya jumla pale Manzese Tip top na darajani na ndo nilienda kuna wauzaji waungwana sana wakanipa list zote na utaratibu wa kupanga bei.

Kuna jamaa walijitokeza humu kunisaidia ambao nilitaka niwape elfu 40,000 ila nikaona wazugaji tu. Mara tuma kwanza pesa mara njoo tuonane hii kasi sio rahisi kama unavyofikiri na wakati mimi nilitaka mtu aniandalie excel file yenye bidhaa zote na bei ya kununulia na kuuzia na wapi nikanunue alafu nampa hiyo 40,000 simple tu. Watu wagumu kweli. Baada ya kuona longo longo hizi na mimi ni mtu aisiyetaka complication na mtu wa kuyaona mambo hata magumu kuwa ni marahisi nikaachana nao nikaingia mwenyewe chimbo madukani na kwenye maduka ya akina mangi na kuulizia. Wengine walinifukuza na wengine walikataa kata kata hata kwa kuwalipa. Ila kwa vile penye nia pana njia nilifanikiwa. Na kwa vile sina hiyana na tamani watanzania wenzangu watamanio kuifanya hii biashara waifanye bila longo longo nyingi nimeweka hapa baadhi ya bidhaa ambazo nimezidowload kwenye accounting software ninayotumia dukani. So far so good nilianza na mauzo ya siku ya kwanza ya shilingi 10,200 nikala faida ya buku mbili kwa siku na kwa sasa in average mauzo ni 70,000 kwa siku with average profit ya 30% ambayo ni 21,000 kwa siku.

Nenda kafungue mkuu na niulize nikwambie ninayoyajua so far kwa hii experience ya miezi mitatu.

Karibu sana

Mkomamazu
Mkuu, naomba unitumie hii kwa email yangu..
Email nakutumia PM
 
Mleta mada umenikosha na mm nimefungua duka leo nina siku ya 7 na siku ya kwanza niliiza laki na Arobaini(140000) Ilinipa moyo sana ila kesho yake ikashuka mpk 50 trend inayoenda toka siku ya tatu na nne ni hyo 50,60 na 70 I hope mambo yatakua mazuri tuu bidhaa ulizoweka Almost nimeweka zote kasoro mafuta ya kupima pima. Nimekuzidi hapo gas nina gas za aina tatu mihan, oryx na O ga.

Kwa mitaa yetu Mihan inatoka vzr daily toka nifungue ninauza mtungi 1 hadi 2. Namshukuru Mungu aisee. Kwa sasa nashughulikia Line ya tigo na Mpesa. Jamani mm nimeona watu wamekua matajiri kwa biashara hii na tena wanakwambia uanze kwa mtaji mdogo uwe una ongeza bidhaa kadri ya mahitaji ya watu. So mtu akitaka kufanya kitu just mpe moyo na sio kuleta theories ambazo hata hujawai kufanyia practicals. Asante tena mleta mada umenipa moyo zaidi wa kupambana
 
Mleta mada umenikosha na mm nimefungua duka leo nina siku ya 7 na siku ya kwanza niliiza laki na Arobaini(140000) Ilinipa moyo sana ila kesho yake ikashuka mpk 50 trend inayoenda toka siku ya tatu na nne ni hyo 50,60 na 70 I hope mambo yatakua mazuri tuu bidhaa ulizoweka Almost nimeweka zote kasoro mafuta ya kupima pima. Nimekuzidi hapo gas nina gas za aina tatu mihan, oryx na O ga.

Kwa mitaa yetu Mihan inatoka vizuri daily toka nifungue ninauza mtungi 1 hadi 2. Namshukuru Mungu aisee. Kwa sasa nashughulikia Line ya tigo na Mpesa. Jamani mm nimeona watu wamekua matajiri kwa biashara hii na tena wanakwambia uanze kwa mtaji mdogo uwe una ongeza bidhaa kadri ya mahitaji ya watu. So mtu akitaka kufanya kitu just mpe moyo na sio kuleta theories ambazo hata hujawai kufanyia practicals. Asante tena mleta mada umenipa moyo zaidi wa kupambana

Mrejesho mzuri huo...
 
Mimi nauza vifuatavyo ambavyo vinatoka haraka;

mafuta ya kula,
sukari,
unga ngano(mara nyingi naisambaza kwa mama ntilie ili iuzike haraka),
sabuni ya kufulia(ya mche na unga),
pipi na jojo,
maharage,
majani chai,
mifuko ya kubebea,
viberiti,

angalau hivyo vina cash flow nzuri kwa upande wangu.
bila shaka mkuu unatokea #KIGOMA hapo kwenye jojo umenikosha sana
 
Back
Top Bottom