Biashara ya Dagaa: Mjadala wa Uendeshaji, Masoko, Faida, Hasara na Changamoto zake

Mkuu mbona swali langu umepiga kimya kunijibu kuhusu Uduvi nikiwa Tanga maeneo gani nitapata Uduvi na kwa bei nafuu maana nashinda kwaajili ya mifugo yangu.
Mkuu bado unahitaji uduvi? Je unapatikana wapi?
 
Habari zenu wadau... Leo nataka niwaletee biashara ya kuanza na mtaji mdogo... Biashara ambayo kama wewe Ni mwanafunzi wa chuo au mama wa nyumbani au hata mfanyakazi unaetaka kujipatia kipato Cha ziada itakufaa Sana.. biashara hii usipokua na aibu itakutoa vizuri tuu...

Hii biashara unaweza kuanza na mtaji wa 55,000... Ni biashara ya dagaa...
Kwenye hii ela utapata dagaa ndoo kubwa ambao wanafika kilo kumi...
KWENYE JINSI YA KUWA PACK SASA..
Unaweza ukafunga
gram 100 ukauza TSH 1,000
gram 50 ukuaza TSH 500.....
Sasa kwenye kila kilo moja utapata utapata packet 10 za elfu Moja au packets 20 za 500... Kwenye kila kilo moja utapata faida ya tsh 4500 ambapo kwenye kilo kumi utapata faida ya tsh 45,000 Kama kila week ukiweza kuuza Hadi kilo kumi natano hadi ishirini utajikuta mwisho wa mwezi umesave hela nzuri sanaaa...
Natamani maswali na maoni yote niyajibie humu humu ili hata ambao watakua sio wateja wapate kitu Cha kujifunza..
Msimu wa dagaa upoje Tanga?
 
Nilipomaliza form six wakati Niko home nliwahi kufuatana na mshkaji wangu ambae yeye alikuwa anaanika kasera kule sahare. Tulifika mpaka Magoma huko.

Juzi amenipigia simu kuhusu hiyo biashara yake, alinikumbusha mbali sana na imebidi nimfae na ameanza tena kuanika
Magoma ndio nimeishi mkuu senta yetu makangara.
Dah nimeikumbuka Korogwe.
 
Jamani poleni na kazi, baada ya kufanya biashara ya dagaa kwa muda fulani kutoka Mwanza kwenda Dar es Salaam nataka nipanue wigo wa kupeleka mkoani Songwe mpakani mwa Tanzania na Zambia (Tunduma)

Lakini kabla sijapata kwanza nilitaka nipate mawasiliano ya watu au wanunuzi wa dagaa kwa bei ya jumla.

Kama upo au unamfahamu INBOX MESSAGE
 
Jamani poleni na kazi, baada ya kufanya biashara ya dagaa kwa muda fulani kutoka Mwanza kwenda Dar es Salaam nataka nipanue wigo wa kupeleka mkoani Songwe mpakani mwa Tanzania na Zambia (Tunduma) lakini kabla sijapata kwanza nilitaka nipate mawasiliano ya watu au wanunuzi wa dagaa kwa bei ya jumla.

Kama upo au unamfahamu INBOX MESSAGE
Nipo Mbeya nitume nikakutafutie soko ntakupa majibu.
 
Jamani poleni na kazi, baada ya kufanya biashara ya dagaa kwa muda fulani kutoka Mwanza kwenda Dar es Salaam nataka nipanue wigo wa kupeleka mkoani Songwe mpakani mwa Tanzania na Zambia (Tunduma)

Lakini kabla sijapata kwanza nilitaka nipate mawasiliano ya watu au wanunuzi wa dagaa kwa bei ya jumla.

Kama upo au unamfahamu INBOX MESSAGE
Wa mikoa mingine tukitaka inakuwaje
 
Nitarudi kuelezea vizuri kuhusu hii biashara kesho ngoja nilale kwanza, nimepita huku mida mibaya.
 
Karibu mkuu, leo ndio hii.

UZOEFU WANGU

Wazo lako la kupanua wigo wa kibiashara ni zuri

Nimewahi kuifanya hii biashara miaka 5 iliyopita kwa Dar, haikunipa matunda sana nikaamua kuacha.

Sababu kubwa ilikuwa udalali kama kawaida zilivyobiashara nyingi za Dar.

Sababu ya pili ni soko jinsi unavyonunua na kuuza ni tofauti.

Mwanza utanunua kwa debe ila Dar utauza kwa kilo soko halitambui kipimo cha debe.

Changamoto inakuja kwenye aina ya dagaa na uzito utakaotoa, kuna uwezekano mkubwa sana wakukupoteza mtaji.

Unakonunua unakutana na madalali lazima wakupige unakoenda kuuza pia unakutana na madalali lazima ule nao, hapo unategemea utapata nini? mbaya zaidi uwe mgeni kabisa katika hii biashara na dagaa hauwajui vizuri.

Kwa upande wa Tunduma ndipo ninapopatikana ila sijawahi kuifanya huku, lakini nimewahi kufatilia jinsi soko lilivyo ikohivi;

Tunduma wananunua na kuuza kwa debe kama ilivyo Mza, bei ya sasa sifahamu mpaka niulizie.

Unatafuta mtu wa kufanya nae biashara unamtumia mzigo anauza kisha anakutumia pesa kulingana na makubaliano yenu

Wafanyabiashara wengi huku wanamiliki stoo ila mtaji wa mzigo hawana, wenye mitaji mikubwa wanafata wenyewe na kuwasambazia wenye stoo wasiyokuwa na mtaji kwa mali kauli.

Kwahiyo usiwe na matumaini makubwa sana kwamba utapiga hela kwa muda mfupi sababu tayari kuna watu wameshatengeneza falme zao katika biashara hii, labda uje na mbinu na mawazo mapya.

Biashara ya dagaa hapa haijachangamka sana na wanunuzi wakubwa wa hii bidhaa ni jirani zetu Wazambia na Wakongo, lakini kwa upande wa Wazambia wanapendelea zaidi furu wale samaki wadogo wadogo wanaochambuliwa toka kwenye dagaa nafikiri unawafahamu.

Hivyo kama utakuja angalia soko la furu huko Mwanza na huku Tunduma, lakini ukiweza angalia pia soko la vibambara vya sangara havipo huku.

Aina ya dagaa wenye bei huku ni wale wa nyasi wanatoka Bukoba na wale wa mafuta waliyokaangwa

Kuhusu usafirishaji mwaka 2017 kwa gunia moja la dagaa toka Mwanza mpaka Tunduma ilikuwa 7000 kwasasa sifahamu, Utauliza huko Mwaloni(soko la dagaa) Mwanza.

Mwisho japo siyo kwa umuhimu;

Karibu Tunduma border ya wajanja lango kuu la nchi 8 za SADEC Tanzania.
 
Asante kwa mchango mzuri.

Naomba kujua bei ya furu kwa Tunduma.
yaani debe moja la furu linanunuliwaje kwa jumla?
 
Similar Discussions

Back
Top Bottom