Biashara ya Dagaa: Mjadala wa Uendeshaji, Masoko, Faida, Hasara na Changamoto zake

MzungukoMnangani

JF-Expert Member
Jan 7, 2012
303
81


Poleni na majukumu wadau, me naomba kwa yeyote mwenye uzoefu wa biashara ya dagaa (wakavu) wa mwanza kupeleka Dar, naomba kujua gharama za kununulia kwa wavuvi, gharama za kuwakausha pamoja na usafirishaji, soko lake na mtaji wa kuanzia na yote yanayohusu biashara hii.

Natanguliza shukrani.

WADAU WENGINE WANAOHITAJI KUFAHAMU KUHUSU BIASHARA HII

MAJIBU/MICHANGO YA WADAU KUHUSU BIASHARA
 
Ha ha ha haa, kaka hilo jina lako, ngoja na mimi nijiite MZUNGUKOLUCHELELE
 
Kaka dagaa ukitaka kumpata nenda ktk visiwa vya ukerewe au sengerema hata bukoba na musoma pia utakuta wavuvi wanavua wakitoka huko huwaanika juani wakikauka majira ya mchana huwauza kwa wafanyabiashara kwa gunia ni sh,40000- 60000 au pungufu ya hapo na baada ya kutimiza mzigo wako husafirishwa kwa meli au mashua mpaka mwana na bei ya kusafirisha gunia ni sh, 2000 hadi mwanza na baada ya kufika mwanza ndo unafanya utaratibu wa'kusafirisha kuwapeleka dare es salaam umenipata.
 
Kusafirisha ni 1Mil/1.5 Mil kwa tani 10/15, kifupi ni rahisi sna kwa kuwa mwanza magari mengi yanarudi tuou hakuna mizigo wala mazao huko ya kuja jijini.
 

Shukrani ndugu ngoja kesho nitembelee maeneo ya Sengerema
 
Wakuu nimesikia watu wanatengeneza hela kwa kufanya hii biashara, so nadhani na mimi nilikua nataka kujua deep zaidi inakuwaje hasa advantages and Disadvantages?? kwanza kabisa najuwa humu ndani wazoefu na kuna watu wa kila aina so sidhani kama itakuwa vibaya tukishauriana wakuu.

1)Kwanza kabisa kiasi ambacho unaweza kuanzia kwa biashara kama hii kuanzia milioni ngapi ambapo utanunua mzigo wa kutosha??

2)Sehemu ya kuuzia zikitoka Mwanza na kufika Dar, Je sehemu zipo ambapo zinaweza kuuzikana kwa ujumla I mean Soko???

3)Je kuna faida gani na hasara gani katika kuzisafirisha na njia ipi ya usafiri ni njia nzuri zaidi

Wakuu kwa haraka haraka nadhani hayo ni ya muhimu kwa sasa nadhani itakuwa vizuri zaidi wengine kama watakuja na idea au maswali mengine na tukapata majibu zaidi.

Nawakilisha
 
Biashara ya dagaa inahitaji umakini mkubwa sana. Usipokuwa mwangalifu, kuna uwezekano mkubwa sana wa pesa zako (mtaji) kuuacha Mwanza! Madalali wa kuuza dagaa Mwanza sio waaminifu. Kwanza wanachakachua uzito wa kilo za dagaa kwa kuchanganya michanga.

Vilevile soko lake huku Dar lina-fluctuate sana. Bei ya kilo ya dagaa inabadilika mara mbili au tatu ndani ya wiki moja. Hivyo ushauri wangu wa bure: tafuta biashara nyingine ya kufanya kuliko kuingia hasara kwenye dagaa.

Unaweza kuni-inbox if u need more clarification
  • Dagaa mza zinanuliwa SOKO LA MWALONI, KIRUMBA
  • Dagaa dar zinauzwa K'koo na ktk masoko mengineyo jijini japo madalali ndio wamekamata soko

- Endapo ni dagaa kwa ajili ya chakula cha kuku, wasiliana na FALCON, maeneo ya Tegeta; falcon ndio wasindikaji wakuu wa chakula cha kuku hapa Dar.

Goodluck!
 

Nashukuru sana mkuu wangu kwa msaada wako na mawazo yako mazuri na ya maana, yeah nitakucheck tuongee vizuri zaidi kaka wala hamna tatizo kabisaa.
 
Kama uko na mawazo ya kufanya biashara ni bora ukaifanya wala mtu asikuogopeshe na ww ukaacha kufanya mjasiliamali hatakiwi kuogopa kufanya kitu cha kufanya ni kuangalia hizo risks alizozisema mdau hapo juu kuna kipindi kama mwezi umepita, nilitembelea Kilosa nikataka kwenda porini hivyo ikanipasa kununua baadhi ya vyakula pale mjin,nilistaajabu kukuta bei ya kilo moja ya dagaa iko sawa na kilo moja ya nyama kwa Dar.

Kwa huko nyama iko chini kidogo zaidi ya dagaa hao wa Mwz hivyo inaonekana soko lake ni zuri sehemu hizo ingawa sikufanya utafiti wa kutosha sana ila nilizunguka sokoni na nikakuta bei iko juu zaidi ya nyama hivyo kama kweli uko tayari unaweza ukafanya utafiti wako katika hiyo biashara ikiwa ni pamoja na kutafuta masoko maeneo hayo sio kila bidhaa lazima iende k/koo mdau hata maeneo mengine kuna masoko mazuri tu cha msingi ni ujasiri na kutokata tamaa.
 

Asante sana mkuu wangu na nashukuru sana kwa mawazo yako na kuwa open zaidi, yeah ni kweli kabisa na wala hujakosea biashara ni ujasiri na kuwaa na nia na kiu ambacho unataka kufanya ndio muhimu zaidi, so yes nitafatilia zaidi hizo sehemu, je una hint ya sehemu zingine uziweke hapa wazi mkuu?

Pamoja sana.
 
Saluti kwenu wanajamvi,

Mimi nipo Mwanza na ninafanya biashara ila ndo nimeanza na huwa nasafirisha kupeleka Dar na kwa sasa nataka kujipanua, natafuta soko Singida, Dodoma au Tunduma.

Kwa yeyote anayehitaji nipo tayari kufanya nae kazi au hata kunisaidia kupata soko hayo maeneo niliyoainisha! Yeyote ambaye yupo tayari ani PM! Pia ushauri na nk unakaribishwa.

Naomba kuwasilisha
 
mpambanaji1

Mkuu habar za majukumu,
Heri ya mwaka mpya..

Nilikuwa nafikiria kufanya biashara ya dagaa yaaniniwatoe wanapopatikana niwapeleke mtwara au niletewe huko japo mwenyewe naishi dar es salaam.

OMBI:
Naomba maelekezo,
1: Nahitaji mtaji kiasi gani ili kuanza biashara hiyo?
2: Vipi kuhusu faida katika biashara hiyo.
3: Kuhusu usimamizi wake (vikwazo vipi nitakumbana navyo)
 
Last edited by a moderator:

Mkuu za majukumu ni njema tu na heri ya mwaka mpya pia mkuu! Tena mkuu huko Mtwara ndo kwenyewe kabisa kama unauhakika wa soko na unamtaji wa kutosha embu tuwasiliane ili tuongee kwa undani zaidi naona ndo itakua njia rahisi ili uweze kupata maelezo ya kutosha!
 

Mkuu ungetumwagia hapa tukafahamu hasa hasa maswali aliyokuuliza mkuu isack, otherwise kila mtu atakuwa akikupigia simu unatoa maelezo upya.
 
Ndugu weka mambo hadharani kila mtu ajue tuweze kufanya biashara, mimi nipo Mbeya
 
hiv mkuu je wale wakukaanga naweza kuwapa?

Hawa unaweza kuwapata lakini ni lazima uweke order sio kwamba unawakuta! kama vipi nipe order na offer yako ya kilo moja iliyokaangwa tuanze mwaka!
 

Similar Discussions

Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…