BIASHARA YA COASTER ZA KUKODI SPECIAL HIRE

BIASHARA YA COASTER ZA KUKODI SPECIAL HIRE

Pharm D

JF-Expert Member
Joined
Feb 17, 2017
Posts
1,238
Reaction score
3,016
Wakuu habari ya Jumapili;
Nina mategemeo ya kupata kiasi fulani hivi cha pesa kinachoweza kununua basi dogo kama coaster/civilian/Rosa, naomba ushauri kwa wenye uzoefu wa hii biashara kuanzia soko, usimamizi, gharama za uendeshaji n.k nione ni jinsi gani ntaweza kujipanga na changamoto ntakazokutana nazo mapema kabla mradi haujaanza
Nb; nategemea kuanza na gari moja

** Natanguliza shukrani**
 
Nimekua mvivu kuandika ...ila ni business nzuri nmewahi fanya ila niliacha kwa sababu zangu binafsi.
 
Mimi naomba kuuliza business ya garden park inalipa...yani natafuta eneo naweka garden watu waje kula, kukaa, kupiga picha mfano ni kama pale mtaa wa magari 7, mbezi mwisho
 
Mimi naomba kuuliza business ya garden park inalipa...yani natafuta eneo naweka garden watu waje kula, kukaa, kupiga picha mfano ni kama pale mtaa wa magari 7, mbezi mwisho
Kama una mtaji kwa dar au dodoma fanya hii....
 
Mkuu Sina idea kuhusiana na hiyo biashara lkn naweza kukusaidia katika ununuaji wa gari Toka nje ya nchi na pia kuhusiana na mkopo wa kununua gari iwe mean vya nchi au nje ya nchi
0686153806
 
Mimi naomba kuuliza business ya garden park inalipa...yani natafuta eneo naweka garden watu waje kula, kukaa, kupiga picha mfano ni kama pale mtaa wa magari 7, mbezi mwisho
Hii inalipa na ndo watu kama wamesanuka... nina marafiki wawili wamefungua hizo na tayari harusi kadhaa zimefanyikia hapo.
 
Hi biashara, dereva ni WA Muhimu kuliko mtaji, Kuna biashara ambazo hakikisha una rasilimali watu kabla ya chochote

Pia Kama upo Dar, gari yenye picha hapo chini ni Marketable sana kwa Dar es salaam na Miko ya karibu ( ukiwa na connection )
 
Ni kweli kabisa akitulia mishe inalipa sana
 
Nikushike mkono, nunua special hire yako. Tafuta ofisi ya watumishi, kiwanda, taasisi binafsi, mashirika, migodi nk. Ongea na hao watu utawachukua asubui majumbani mwao na kuwarudisha, patana nao malipo mwisho wa wiki au itakavyokupendeza kwenye makubaliano yenu. Gari iwe safi gari kipupwe kipulize vizuri.
 
Kwanza inatakiwa ujue wateja wako ni watu wa aina gani, kubeba staff au kusafirisha maiti mikoani.
Kwa Mimi kuliko kutoa milioni 80 kununua coaster bora ninunue mchina howo tipper nisake tenda za kutoa mchanga shamba kuleta mjini kwenye ujenzi.
Au hio amount nichukue mchina fupi youtong ya siti 45 nipige ruti za sh elf 20 au 15 asubuhi moja jioni moja gari inarudi kulala sebuleni kwangu naiona.
 
Back
Top Bottom