Kumachawa ww biashara utaifanya bila mtaji unadhan wote wanaolalamika ajira hawana mawazo ya kufanya biashara kama mtu hana hata hela ya vocha jero na anaish kwao hiyo biashara anaifanyaje au ndo utaleta porojo za kuwa winga au siyo.
Watanzania wengi tunafeli kwa sababu ya mawazo kama haya.
Unamdharau winga wakati akikusanya hela kwa siku ukazidisha mara mwezi ni zaidi ya mshahara wa muhasibu au daktari wa Hamashauri.
Eti utamkuta mtu kazi yake ni kula,kulala,akiamka anakaa kwenye sofa kashika remote ya Tv kwenye sebule ya shemeji yake ukimuuliza wewe unafanya biashara gani?anakujibu sina mtaji,sasa unataka huo mtaji uanguke kutoka mbinguni?
Kama ni kijana wa kiume nenda kajichanganye kwa wahindi upige vibarua umake pesa kwa miezi kadhaa upate mtaji ufanikishe lengo lako na kama ni kijana wa kike nenda katafute vibarua hata kwenye migahawa au saloon umake pesa upate mtaji utimize lengo lako badala ya kupoteza muda kulalamika kila wakati huku umri unaenda muda haurudi nyuma.
Mimi nimeishi na vijana wa kutoka nchi mbalimbali wa kutoka Kenya,Uganda,Sudan,Ghana,Nigeria,Sierraleone,Gambia sasa kila nikiwacheki hawa vijana ujanja wao wa kujiongeza nikilinganisha na kwetu TZ najiona tuko nyuma mno yaani wametuacha mbali.
Wenyewe unakuta kijana ana miaka 19 tayari ameshajiongeza anachekecha haraka haraka mazingira ya nyumbani anagundua hapaliki anapanda anasafiri kwenda ughaibuni anatua kiwanjani kugombania ajira tena hawa ni form 4 tu ila wana confidence hatari ukiingia kichwakichwa kwenye interview na degree yako wanakuaibisha wanachukua ajira.