Biashara mpaka barabarani, Mamlaka ziangalie madhara

Biashara mpaka barabarani, Mamlaka ziangalie madhara

Ni kero sana hawa machinga

Sent using Jamii Forums mobile app
Kituo chetu cha Daladala asubuhi huwezi kusimama au Kukaa kusubiri Usafiri. Moshi mzito wa kuni zinazopika vtafunwa na Supu ni Kero. Hivi hawa Health Officers haya Matatizo ya Watu kupikia Barabarani wanashindwa kuzibiti? Unataka kupanda Gari unanuka Moshi. Mnapishana na kukimbizana kugombeavUsafiri kando ya Moto!!!
 
Kwa nini mtu ujenge kibanda cha nguo katikati ya lami hivi hawa watu wako Sawa boda boda nao kila sehemu kwao ni kituo cha kusubiri abiria.
 
Halafu eti kuna pedestrian, walkways sijui service roads???? Barabara chache bongo zinapo jengwa hawatengi maeneo hayo kwa watu kupanga vitu njiani. Nooop!

NI KERO KERO KERO TUPU. Siku nitakapo kanyaga mali ya mtu akalalamika ndipo nitakapo foka kama kichaa...
 
Kwa hili JPM kachemka mbayaa, hata kama ni wapiga kura, kufuata utaratibu sio dhambi hata siku moja. Kuna kipindi hapa nyuma(nadhani 2018) kariakoo palipendeza, watu walikuwa wanaingia madukani kununua bidhaa, jamaa kaenda Mbezi-Kimara kaanza kuwaambia watu waachwe wafanye biashara wanavyotaka, eti ni wapigakura wa mzee baba.

Ndio maana nashangaa hii kitu mnaita 'political science', sijui huko mnafundishana nini hakyanani...
[emoji23] [emoji23] [emoji23] [emoji23]
 
Bora ingetokea tu.
Wakuu acheni kuwaombea watu mabaya bwana
Hata hivyo hawatahama Ng'oo kisa ajali

Ni kweli ina KERA SANA sio kidgo Mji Mzima huu kero Tupu Hakuna Sehem ya afadhali
Bora kidogo kituo cha MAWASILIANO Mule Ndani Pako Shwari Sana


Na hili Swala Factor kubwa ni Mfumo wetu wa Maisha Tanzania
Yani tunaeep kuzalisha Wamachinga hawapungui
 
Wawamhie kitu cha kwanza asubuhi kila mtu afagie eneo lake kabla ya kuanza bisshara.
 
Back
Top Bottom