Biashara mpaka barabarani, Mamlaka ziangalie madhara

fyddell

JF-Expert Member
Dec 19, 2011
11,109
19,987
Hii ni barabara ya Uhuru soko la Karume, wafanyabiashara wanaotandaza bidhaa zao chini wamesogea mpaka usawa wa barabara na kusababisha usumbufu na foleni zisizotarajiwa kwa watumiaji wa njia hiyo kuelekea au kutoka katika ya jiji la Dar es Salaam.

Hakuna mamlaka ya kuzuia hili kwa usalama wa wafanyabiashara na magari yatumiayo barabara hiyo?
Au vitambilisho vya mjasiliamali vinawapa kinga wafanyabiashara kufanya biashara mahali popote pale?
Huko mjini maeneo ya Kisutu barabara ndogo zitokazo na ziingiazo zote zimejaa mama ntilie na wauza matunda. Tunaomba mamlaka husika irudie ule utaratibu wa zamani wakutenga maeneo maalumu ya biashara.

Tutajua kuwa hili lilipangwa kimkakati ili kuongeza mapato serikalini. Sasa tunaomba mamlaka iangalie madhara yanayosababishwa na ufanyaji biashara holela.

IMG_20200124_110343.jpeg
IMG_20200124_110233.jpeg
IMG_20200124_110217.jpeg

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Acha watu watafute riziki ya halali ukiwatoa hapo utawapeleka wapi?
Ikitokea basi ajali kazini Mzee!!!
 
Hii ni barabara ya Uhuru soko la Karume, wafanyabiashara wanaotandaza bidhaa zao chini wamesogea mpaka usawa wa barabara na kusababisha usumbufu na foleni zisizotarajiwa kwa watumiaji wa njia hiyo kuelekea au kutoka katika ya jiji la Dar es Salaam.

Hakuna mamlaka ya kuzuia hili kwa usalama wa wafanyabiashara na magari yatumiayo barabara hiyo?
Au vitambilisho vya mjasiliamali vinawapa kinga wafanyabiashara kufanya biashara mahali popote pale?
Huko mjini maeneo ya Kisutu barabara ndogo zitokazo na ziingiazo zote zimejaa mama ntilie na wauza matunda. Tunaomba mamlaka husika irudie ule utaratibu wa zamani wakutenga maeneo maalumu ya biashara.

Tutajua kuwa hili lilipangwa kimkakati ili kuongeza mapato serikalini. Sasa tunaomba mamlaka iangalie madhara yanayosababishwa na ufanyaji biashara holela.

View attachment 1332807View attachment 1332808View attachment 1332810

Sent using Jamii Forums mobile app

Rais alisema wapange sehemu yheyote watakayoona inafaa, na akasema akisikia kiongozi yeyote aliyemteua anawanyanyasa hao wapiga kura wake, atamtumbua.

Waache tu ajali zikiongezeka na watu kupoteza maisha wataondoka wenyewe.
 
Hii ni sababu nyingine ya kuthibitisha kuwa we're doomed, bidhaa zipo katikati ya barabara, bodaboda zimepaki katikati ya barabara, watembeza matunda wapo njiani kabisa. Why?

Kweli kuzaliwa taifa masikini ni mzigo mzito.
 
Halafu huyo huyo anawaambia watu wazaliane kwa fujo..hawa wa sasa kuwa control ni shida, halafu bado dah..!

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Back
Top Bottom