Biashara mpaka barabarani, Mamlaka ziangalie madhara

Biashara mpaka barabarani, Mamlaka ziangalie madhara

Acha watu watafute riziki ya halali ukiwatoa hapo utawapeleka wapi?
Ikitokea basi ajali kazini Mzee!!!
Nafikiri serikali ilitakiwa kuwa na mbinu muafaka juu ya hili swala la kuwakamua kodi wajasiliamali wenye mtaji chini ya mil 4 na si kwakuwaruhusu wafanye biashara mahali popote pale.

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Kuna kipindi pale Gerezani, palipendeza kweli kweli(mwaka juzi), machinga wote waliondolewa. Nenda sasa hivi.

By the way, mwanzisha mada, unafikiri nini kifanyike kumaliza tatizo hilo? Namaanisha, wakiondolewa hapo, waende wapi?
 
Hapo ukute utaratibu upo ila hawaufatu Au
Mamlaka hawaja fany chochote Wapo tuu

Yani ilimradi ni Africa Hakuna tuliwezalo

Kaliakoo kwanzia kamata Kwenye kituo cha reli Mpaka msimbazi wamejaa wamachinga pembeni kwa watembea kwa miguu
Kaz ni kupishana na Magari kama vile na Sisi ni Magari
 
Hapo bado bodaboda wapaki mbele wanajali biashara zao kuliko roho za watu.Mbagala nikipita huwa najiuliza maalaka hazioni.
Inasikitisha Sana. Ila watanzania hatujihadhali na matukio ambayo yalishatokea kipindi cha nyumba. Nashangaa kwanini mpaka madhala yatokee ndio tuchukue hatua wakati maisha ya ndugu zetu yameshakatishwa?
Tujifunze na tuelimike kutibu jeraha kabla ya kidonda.

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Tatizo ni wanunuaji. Watu wakikataa nunua wataondoka tu. Watu waende madukani

Sent using Jamii Forums mobile app
Kwahili Mkuu ni ngumu amini nakwambia. Hawezi kumzuia mwenye hitaji wakati anahitaji, atafuata kile akitakacho kilipo kwasababu anahitaji. Chamsingi nikuwa na utaratibu maalumu kwa wafanyabiashara nasi tutawafuata popote walipo.

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Hii ni barabara ya Uhuru soko la Karume, wafanyabiashara wanaotandaza bidhaa zao chini wamesogea mpaka usawa wa barabara na kusababisha usumbufu na foleni zisizotarajiwa kwa watumiaji wa njia hiyo kuelekea au kutoka katika ya jiji la Dar es Salaam.

Hakuna mamlaka ya kuzuia hili kwa usalama wa wafanyabiashara na magari yatumiayo barabara hiyo?
Au vitambilisho vya mjasiliamali vinawapa kinga wafanyabiashara kufanya biashara mahali popote pale?
Huko mjini maeneo ya Kisutu barabara ndogo zitokazo na ziingiazo zote zimejaa mama ntilie na wauza matunda. Tunaomba mamlaka husika irudie ule utaratibu wa zamani wakutenga maeneo maalumu ya biashara.

Tutajua kuwa hili lilipangwa kimkakati ili kuongeza mapato serikalini. Sasa tunaomba mamlaka iangalie madhara yanayosababishwa na ufanyaji biashara holela.

View attachment 1332807View attachment 1332808View attachment 1332810

Sent using Jamii Forums mobile app
Mamlaka ya huu kanisa nchini iliruhusu hivyo hakuna mwingine anayeweza kuthubutu kuingilia, waliambiwa barabara zimejengwa ili wafanyie biashara na wakiweza wakapange biashara zao kwenye ofisi za serikali ya mtaa.
 
Rais alisema wapange sehemu yheyote watakayoona inafaa, na akasema akisikia kiongozi yeyote aliyemteua anawanyanyasa hao wapiga kura wake, atamtumbua.

Waache tu ajali zikiongezeka na watu kupoteza maisha wataondoka wenyewe.
Huoni kuna tatizo hapo mkuu katika hilo agizo?

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Tunaanzaje sasa kukataa kuwaunga mkono masikini wenzetu.
Nadhani siku ikitokea kama lile bus lililokuwa linaenda Arusha tokes Dar likakosa break na kuwaparamia watu na magari pembeni, Utakuja hapa na hadithi nyingine.
Sawa ni wenzetu, lakini kwanini tusiepushe majanga mkubwa zaidi yanayoweza kugarimu maisha ya Hao masikini mapema?
The authority is needed to do something about this seriously.

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Kuna kipindi pale Gerezani, palipendeza kweli kweli(mwaka juzi), machinga wote waliondolewa. Nenda sasa hivi.

By the way, mwanzisha mada, unafikiri nini kifanyike kumaliza tatizo hilo? Namaanisha, wakiondolewa hapo, waende wapi?
Nilishasema tangia mwanzo Mkuu, kuwa ingepaswa watulie maeneo ambayo yalikuwa yameshatayarishwa tangia awamu iliyopita kama kwenye masoko yaliyojengwa kila kata nchi nzima, kwa Dar kuna Machinga Complex, Kariakoo, Karume, Mbagara market n.k
Tatizo ni urahisishaji ili kitu flani kipatikane kwa njia yoyote ile.

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Kwa hili JPM kachemka mbayaa, hata kama ni wapiga kura, kufuata utaratibu sio dhambi hata siku moja. Kuna kipindi hapa nyuma(nadhani 2018) kariakoo palipendeza, watu walikuwa wanaingia madukani kununua bidhaa, jamaa kaenda Mbezi-Kimara kaanza kuwaambia watu waachwe wafanye biashara wanavyotaka, eti ni wapigakura wa mzee baba.

Ndio maana nashangaa hii kitu mnaita 'political science', sijui huko mnafundishana nini hakyanani...
 
Hili jambo la kupanga miji yetu naona tumeahindwa Kabisa...Wizara ya Ardhi nyumba na maendeleo ya Makazi wanatakiwa kuwahi kabla ili tusiwe na miji mingi isiyopimwa iliyojaa uchafu kama hivi.

Ni jambo la aibu sana...
 
Back
Top Bottom