Biashara inauzwa m35 | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Biashara inauzwa m35

Discussion in 'Biashara, Uchumi na Ujasiriamali' started by chash, Jun 11, 2012.

 1. chash

  chash JF-Expert Member

  #1
  Jun 11, 2012
  Joined: Jun 5, 2012
  Messages: 553
  Likes Received: 27
  Trophy Points: 45
  Ni ya m-pesa, tigo na airtel money. Ina matawi (maduka) kumi. Nane yanafanya kazi. Ina faida ya million tano na zaidi kwa mwezi. Faida inaweza kuongezeka zaidi ya hapo.Kwa mawasiliano: 0755442766, 0712926433
   
 2. CHASHA FARMING

  CHASHA FARMING Verified User

  #2
  Jun 11, 2012
  Joined: Jun 4, 2011
  Messages: 6,133
  Likes Received: 2,129
  Trophy Points: 280
  Mkuu unacho uza nini hapo? lazima unyumbue hiyo milioni 35 inakuja vipi, make suzani ni kutamka tu milioni 35,
  Je hiyo milioni 35 inajumuisha

  1. Nyumba/offisi za kufanyia kazi

  2, Vitendea kazi

  3, Wafanyakazi

  4. Na hiyo milioni 5 faida,

  Au wewe unazua n ini hasa, Je ni jina la kusajiliwa na Vodacom kuwa wakala?
   
 3. chash

  chash JF-Expert Member

  #3
  Jun 11, 2012
  Joined: Jun 5, 2012
  Messages: 553
  Likes Received: 27
  Trophy Points: 45
  Mkuu, nashukuru kwa interest na maswali yako. Itakuwa vizuri kama upo serious tuwasiliane uje kwenye biashara ukagueKila kitu na upate maelezo yote. Kwa kweli hiyo m35 nimekisiakwa kujiuliza hii biashara inayo niingizia kipato cha m5 kwa mwezinikiwa nimeweka float ya m12 inafaa niiuze bei gani? basi kama utanipasababu za kutosha nitapunguza bei. Asante
   
 4. georgeallen

  georgeallen JF-Expert Member

  #4
  Jun 11, 2012
  Joined: Jun 3, 2011
  Messages: 3,758
  Likes Received: 57
  Trophy Points: 145
  Acha longo longo. Tafadhali jibu swali.
   
 5. CHASHA FARMING

  CHASHA FARMING Verified User

  #5
  Jun 11, 2012
  Joined: Jun 4, 2011
  Messages: 6,133
  Likes Received: 2,129
  Trophy Points: 280
  Mkuu tatizo si kuwa na nia, na hata siku moja huwezi uza biashara kwa kukadria kama vile watu wanavyo uza Bamia, Mkuu Biashara yoyte kabla ya kuiuza lazima uandae ripoti za kufa mtu ili kuwavutia wazwekezaji, HII FOLUM INASOMWA NA WATU WENGI SANA UNAWEZA KUTA KUNA MTU YUKO SOUTH AFRICA ANATAKA ANUNUE AU YUKO KENYA ANATAKA ANUNUE, sasa ukija na story kwamba umekadria, watakushangaa sana kuwa siriasi mkuu

  Nimekuuliza hiyo Milioni 35 inakuja vipi hujajibu, na usiseme umekadria tu, na umesema una offisi 6 je nazo zinauzwa? je wafanyakazi?

  MKUU TAFUTA WASHAURI WA BIASHARA WAKUSAIDIE KUNADAA TARIFA ZA FEDHA ZENU ULETE HAPA JAMVINI, VINGINEVYO MKUU HAKUNA ATAKAYE KUELEWA
   
 6. Jestina

  Jestina JF-Expert Member

  #6
  Jun 11, 2012
  Joined: Jan 6, 2011
  Messages: 4,807
  Likes Received: 120
  Trophy Points: 160
  kama unaweza jibu hapa hapa...maswali ya komandoo kwa faida ya wengi...
   
 7. wehoodie

  wehoodie JF-Expert Member

  #7
  Jun 12, 2012
  Joined: Nov 20, 2011
  Messages: 784
  Likes Received: 361
  Trophy Points: 80
  Hapo unauza goodwill/brand au inventory? maana wafanya kazi sio asset hawathaminishwi na pia kama ofisi zipo kwenye majengo ya kupanga sijui ni vifaa assets zepi zinavyofikia hiyo bei ya TZS 35M?? Fafanua.
   
 8. Globu

  Globu JF-Expert Member

  #8
  Jun 12, 2012
  Joined: Jan 12, 2011
  Messages: 7,975
  Likes Received: 176
  Trophy Points: 160
  Biashara ya kiswahili hiyo.
   
 9. Shark

  Shark JF-Expert Member

  #9
  Jun 12, 2012
  Joined: Jan 25, 2010
  Messages: 20,136
  Likes Received: 7,389
  Trophy Points: 280
  Hayo maduka 10 yapo kwenye kiwanja chako au cha kukodi??

  Kama ni kukodi/kupanga, Tshs ngapi kwa kila moja/yote?

  Yamelipiwa kodi mpaka lini??
   
 10. MamaEE

  MamaEE Senior Member

  #10
  Jun 12, 2012
  Joined: Jun 2, 2011
  Messages: 103
  Likes Received: 5
  Trophy Points: 0
  Naona ameshasepa... hizi biashara za kuamka na kutamka bei bila vigezo, tabu tupu.
   
 11. chash

  chash JF-Expert Member

  #11
  Jun 12, 2012
  Joined: Jun 5, 2012
  Messages: 553
  Likes Received: 27
  Trophy Points: 45
  Mkuu, najaribu tena nikujibu.Naona unataka gumzo yote ifanyike kwenye forum. Ok.

  Kwanza nikutaarifu, biashara ni willing buyer and willing seller kwa hiyo nnaweza kutaja bei yeyote ambayo naona inafaa.
  Hii m35 ni goodwill kama @weehodie alivyo sema. kama ipo juu basi nikipewa sababu ya kupunguza kidogo nipo
  tayari.
  Pili. Biashara ina ofisi nane. zote za kukodisha. Kwa m35 utapata na mikataba ya kodi ya mwaka mmoja.
  Kila ofisi ina kaunta na viti. ofisi mbili ni kaunta zenye madirisha ya vioo ya kutolea huduma, mbili ni nondo na grill, zingine ni open kaunta lakini muhudumu anakuwa mbali na mteja. kodi zote pamoja ni 360,000 kwa mwezi.
  computer ni moja, laptop yenye mtandao wa mpesa kukuwezesha kuangalia kazi zinavyo enda.
  Simu za kazi ni 19 ikiwa ni pamoja na head offfice na management till ya kukuwezesha kuhamisha hela kutoka ofisi moja hadi nyingine, kupokea commission n.k

  Wafanyakazi ni 11. mishahara yao wote kwa mwezi ni 820,000. wafanya kazi 9 wapo tayari kuendelea na boss mpya.
  Kuna taratibu tunazo zitumia ili kuwa na uhakika kwamba kwa sehemu kubwa wanakuwa waaminifu.

  Maduka mawili yapo dsm mengine yote ni mikoani. hii ni muhimu kwa sababu hutapata tatizo la float kama inavyo kuwa kwenye maduka mengi. Mikoani wanatoa hela sana na hapo unapata float. Mjini wana deposit sana hivyo una pata cash ya kuzungusha mkoani.

  Biashara inauzwa as a going concern. yaani jinsi inavyo endelea, owners wanabadilika na mwingine anaingia nakuendelea au kufanya mabadiliko yanayo mpendezeni yeye.

  Hatuuzi vocha, simu, betri, au makasha ya simu. Hizi ni biashara unaweza kufanya kwenye hayo maduka ukaongeza faida
  kwa kiwango kizuri. Maduka manne yanafaa sana kwa kuweka pia mtandao wa internet, yote yanafaa kuweka photocopy, typing, printing n.k Kama ukiamua kuweka float m20 na zaidi na uongeze biashara ya simu na vocha nina uhakika faida kwa mwezi haita pungua m10 kwa mwezi. Hii biashara ina kuwezesha kupata mikopo mikubwa benki mfano m100 na zaidi kwa ajili ya mzunguko wake wa hela. Hivyo tusema future yake ni nzuri sana.

  Mapungufu ya biashara.
  Kazi ni kubwa kwa sababu lazima u balance hela kila siku ku hakikisha hamna short. Hiyo lazima uwe mtu makini kwenye
  hesabu. Hata wafanya kazi wakiwa wazuri kama haupo makini unawapa nafasi kudokoa. Kila baada ya mda usio mrefu zunguka maduka yote. Hii inachosha. Unapo weka stock na kupanua biashara itabidi kuweka walinzi na kuongeza wahudumu. Ni vizuri uwe na system ya kuweka fedha kiasi kisicho kikubwa kwa wakati mmoja na pia uendelee kuboresha maduka kwa ajili ya security ya fedha jinsi kazi zinavyo endelea.

  Sababu ya kuuza hii biashara. Wenyewe wanasafiri kwenda nje ya nchi. kwa mda wa mwezi mmoja watakusaidia ku-take over na kuelewa kazi.
   
 12. chash

  chash JF-Expert Member

  #12
  Jun 12, 2012
  Joined: Jun 5, 2012
  Messages: 553
  Likes Received: 27
  Trophy Points: 45
  nimesha jibu siwezi kusepa kwenye ukweli.
   
 13. Safari_ni_Safari

  Safari_ni_Safari JF-Expert Member

  #13
  Jun 12, 2012
  Joined: Oct 5, 2007
  Messages: 22,481
  Likes Received: 5,861
  Trophy Points: 280
  Kwa risks ulizoorodhesha biashara haina bima mkuu?
   
 14. chash

  chash JF-Expert Member

  #14
  Jun 12, 2012
  Joined: Jun 5, 2012
  Messages: 553
  Likes Received: 27
  Trophy Points: 45
  sikuweka bima.
   
 15. Nivea

  Nivea JF-Expert Member

  #15
  Jun 12, 2012
  Joined: May 21, 2012
  Messages: 7,449
  Likes Received: 71
  Trophy Points: 145
  SASA UM EFUNGUKA KIDOGO JAPO KWA JEURI MKUU ,INABIDI UWE MPOLE UNATEGEMEA KWA MAELEZO ya awali mtu atatoa hela kweli labda ukaongee na MAIGE hela ndogo sanakwake. bali kama walengwa ni watu wakawaida funguka zaidi kwenye hili
  1, hayo maduka yapo wapi, mkoa gani nakama ni dsm maeneo gani ili mtu ajipange atayatembeleaje/
   
 16. chash

  chash JF-Expert Member

  #16
  Jun 12, 2012
  Joined: Jun 5, 2012
  Messages: 553
  Likes Received: 27
  Trophy Points: 45
  kwa kuona maduka na maelezo zaidi piga simu 0755442766 au 0712926433 asante
   
 17. Jestina

  Jestina JF-Expert Member

  #17
  Jun 13, 2012
  Joined: Jan 6, 2011
  Messages: 4,807
  Likes Received: 120
  Trophy Points: 160
  mkuu kwa nini usingesplit hio millioni 35 ni nyingi mno kuitoa kwa mkupuo/kwa mtu mmoja.....lakini ungezigawanya at least maduka matatu matatu,au mawili mawili....ili iwe affordable,au haiwezekani????nenda taratibu na mie maana kilaza atii lol:glasses-nerdy:
   
 18. chash

  chash JF-Expert Member

  #18
  Jun 14, 2012
  Joined: Jun 5, 2012
  Messages: 553
  Likes Received: 27
  Trophy Points: 45
  niki split maduka faida na operations sitabadilika sana kiasi mengine yatakuwa hayana faida. It will be a different thing. Ukitaka duka mbili au tatu fuatilia utaratibu wa kupanga frame mbili au tatu alafu uombe simu za kufanyia kazi kutoka vodacom, tigo nk. Hivyo haitakubidi kulipa hela kwa mtu na hela yako utaiweka directly kwenye flot. Asante
   
 19. TIQO

  TIQO JF-Expert Member

  #19
  Jun 14, 2012
  Joined: Jan 8, 2011
  Messages: 13,832
  Likes Received: 46
  Trophy Points: 0
  Ok umetiririka mkuu
   
 20. Ghost

  Ghost JF-Expert Member

  #20
  Jun 15, 2012
  Joined: Apr 20, 2010
  Messages: 429
  Likes Received: 2
  Trophy Points: 0
  Ni operation nzuri ila inachosha...it needs full time supervision. C unajua cc watz ni wavivu:lock1:
   
Loading...