'Biashara inapotoka sana ni kipindi cha hatari sana'.

Crispin Nyoni

JF-Expert Member
Dec 11, 2012
413
90
Wakuu!Nilikuwa napita mahali nikakuta mwanababa mmoja kwenye simu akiongea maneno hayo.Naomba mnisaidie yana maana gani?
 
Kibiashara kipindi hiki kibaya kwani juhudi za kusaka wateja zaidi zinapungua kwa kujivunia wateja wanaopita kama upepo.
 
Watu wakiona unapata mafanikio basi na wenyewe wataanzisha hiyo biashara kwa kasi sana na utakuwa na competitor wengi,thats why unaona matajiri huwa hawa invest sehemu moja mf, azam hajakaa na unga pekee yake ameenda ktk vinywaji,recycling etc
 
unapofungua biashara ikafikia hatua ya kuwa inatoka sana new rivals wanaingia sokoni na kusababisha competition ambao unakuwa mkali maana ajaye nyuma yako tayari kashaisoma product yako na kuja na yake ambayo ni modified. So customer watapungua kwako na kwenda kwenye modified products, pia hata bei ya bidhaa yako yaweza kushuka na kusababisha hasara.
 
Wakuu!Nilikuwa napita mahali nikakuta mwanababa mmoja kwenye simu akiongea maneno hayo.Naomba mnisaidie yana maana gani?

Biashara inapotoka sana ni alama ya mafanikio, hiyo huvuta competitors wengi baada ya kuona ni biashara inayotoka na pia kutoka sana kwa biashara yako ni chukizo kwa maadui zako ambao daima hawavutiwi na mafanikio hayo! Sasa hao wote kwa pamoja yaani washindani na maadui huanza kuweka mazingira ya kuweka vikwazo, kuchafua biashara yako, kuhujumu, kukuzushia hili na lile, kuwa hulipii hili na lile, yaani hapo mapambano mengine huwa yameshaanza! Ni kweli 'Biashara inapotoka sana ni kipindi hatari sana'!
 
Mimi nadhani hii tahadhari ni kwa wafanyabiashara wapya,hapa namaanisha kwa mfano ukiona biashara ya kuku wa nyama inatoka sana usijidanganye kwenda kufungua banda la kufugia kuku kwa 7bu tu wanalipa kwa kipindi hicho,kumbuka kipindi hicho utapata vifaranga kwa bei ya juu sana, hii haimaanisha kuwa kwa mfanyabiashara wa bidhaa husika aachane na biashara hiyo,ni tahadhari tu kwa wale watakaotamani kuingia kichwakichwa kwenye biashara husika maana biashara ikiwa nzuri inamaanisha kwa mtu atakayetamani kuanza kufanya biashara kipindi hcho hata bidhaa za kuanzia atazipata kwa bei ghari sana,mwisho wa siku muda wa biashara yako kuchanganya utakuta ndo muda ambao hyo biashara imedoda and u knw what gonna happen! Kikubwa sio kuangalia bidhaa flani inatoka sana na kuingia kichwakichwa..ni tahadhari tu kwa wale watakaokuwa nje ya 'game' kutoingia kwenye game husika kwa tamaa,pia walioko ndani ya game hakika watameki sana kipindi hicho na hiyo kauli haiwa-affect kama wengi wanavydhani..
 
Back
Top Bottom