Mvua zinaharibu mishe

Mohamedex121

JF-Expert Member
Jan 27, 2022
1,688
3,142
Salamu wakuu naimani kuna wenzangu na mimi wale wahanga wa mvua za siku mbili hizi. Nawapa pole sana tuendelea kuchukua tahadhari kutoka kwa mamlaka husika

Mvua zinaponyesha tunaoteseka ni sisi wamachinga tusiokuwa na sehemu rasmi ya kufanyia biashara maana asilimia kubwa biashara zetu ni kusimama na meza barabarani wengine hutumia mwamvuli lakini kama mnavyojua mvua mara nyingi huwa zinaharibu mishe

Kipindi cha mvua wateja hupungua sana sijui Kwanini. Any way nina siku mbili nimeshinda nyumbani bila kwenda kwenye mihangaiko. Naombeni mnisaidie hela ya kula wakuu pesa ya akiba nimelipia kodi jana tarehe 1.

Hivyo hadi sasa sina hata mia na sijui napataje hela ya kula jioni hii maana mpaka sasa bado sijala chochote toka asubuhi.

Natanguliza shukurani wakuu
 
Back
Top Bottom