Biashara gani Pasua kichwa....!!!!?

=======================
Mkuu unasema kweli au unatani?
maana mimi nikotayari kuianzisha hiya project kama utaniunganisha nahuyo mchad
Naona LAT amekukatisha tamaa kama ungekuwa tayari kwa hiyo project tungewasiliana na Mchad ufanyanae kazi
 
Biashara kichaa duniani ni biashara ya pilipili

1. Unayeuza huonji
2. Unaowauzia hawaonji
3. Haina nyongeza
4. Ukiuza ni chafya na kukohoa
5. Hata ukiacha bila kufunika asubuhi unaikuta kaka ulivyoacha
6. Zikikaribia kuharibika huwezi kusema utazipeleka nyumbani kwa matumizi
7.
8.
9.
 
Daladala na Taxi hii ni balaa niliishawahi kuona jamaa hesabu ya teksi analetewa 10,000 kwa siku na daladala analetewa 25,000 kwa siku nyingine unaambiwa walikamatwa na trafiki kwahiyo wakapigwa faini 40,000 huku bado gari haijaenda service mafuta yenyewe wanaweza kuweka yaliochanganywa na mafuta ya taa, kuna jamaa alikuwa na daladala tano akajikuta amebakiwa na mbili tu, mchezo wa kupokezana madereva kwenye daladala ndio unaua gari lako maana gari lako anapewa teja aendeshe yeye wala hajali litapigiza kwenye mashimo kila mwezi unanunua spring mpya
 
  • Thanks
Reactions: LAT
Wakuu ili tuweze kuwa makini na aina za biashara pale tunapotaka kuwekeza na kufanya biashara ninaomba angalau tujuzane biashara gani ni pasua kichwa (biashara kichaa) yaani katika makundi haya: hutumia muda mwingi, usumbufu mkubwa, risk kubwa na pia faida hupatikana kidogo .... hii ni katika level ya ujasiriamali .... assuming that unaifanya kwa ufanisi wote na discipline ya biashara

hapa tunaweza kupata na ufumbuzi wa mojawapo ya biashara pasua kichwa

  • yaweza kuwa biashara ya kuleta magari toka nje yasiyo na brand za kijapani .... kama vile volkswagon, hammer, Peugeot, Renault, BMW, range rover n.k ?
  • Biashara ya kuleta mkaa kama agent wa wachoma mikaa na kuwauzia retailers ?
  • biashara ya maji ya kunywa retail ?
  • biashara ya kuuza vocha za simu ?
  • biashara ya daladala ?
  • biashara ya bodaboda ?
  • biashara ya taxi ?
  • gutter politics (siasa uchwara) ...?
  • biashara ya udalali kishoka

na nyinginezo nyingi twaweza endelea kuzitaja na kuelezea

hakuna anayetaka kupasua kichwa kwa kufanya bishara kichaa ..... i stand to be corrected
Watu wanaofanya biashara za haya magari sijui aisee maana kuna jamaa aliyaagiza kilichotokea yote yako yard yanapigwa kutu watu hawana mpango nayo wateja wake ni wachache sana
 
biashara inayoniogopesha ni ya madini ..... yaani ukizubaa kidogo tuu ujanja unaingia
 
Biashara ya kuuza vocha (Superdealer) kuna ndugu anafanya hii biashara kila leo huwa haishi vituo vya polisi maana jamaa wanamuibia sana mtu anauza vocha za milioni 5 au 7 anatokomea na hela.
 
Binafsi nadhani hakuna biashara mbaya kama unajua tricks za hio biashara (kitu ambacho kina-kuset apart from the rest)...

Biashara ikiwa rahisi kufanyika basi kila mtu atafanya na demand itapungua..., kwahiyo hata hizo perishable goods ukihakikisha kwamba margin yako ni kubwa na una soko la kutosha basi hata ukiuza nusu tu ya bidhaa pesa yako imerudi

Biashara ya magari wajanja huwa wanahakikisha kuna management nzuri na gari likisharudisha pesa tu anauza na kununua jipya...

Kwahiyo kila biashara ikifanywa kwa utaratibu wake ina faida; cha kufanya ni kuhakikisha unafanya homework na kujua A, B, na C za hiyo biashara. Margin kama ni ndogo basi inabidi uuze volume kama margin ni kubwa unaweza ukaleta gari moja tu lakini ukiliuza hata kama limechukua mwaka mzima faida yake huenda ikawa ni sawasawa na faida ya mtu alieuza kitu kwa miaka miwili... Kwahiyo kinachomata ni research inaweza ikawa ni uchizi kuuza ICE North Pole lakini ikawa ni goldmine kuuza ice jangwani au kuuza kiti moto Zanzibar huenda usipate kitu lakini Tanzania bara ikawa ni deal
 
Halafu kama ni dala x 2 liwe la kwenda Mbagala,utajuta kuzaliwa,maana kule hamna cha mzazi,babu,mtoto rtc wote wanakulia timing kukukopa,halafu konda lazima avute kwanza maana hawezi kuongea na abiria wa kule bila hivyo-duuuh mm sithubutu!

biashara ya usafiri ni kichaa in TZ
-TRA
-Trafiki
-Sumatra
-Majembe-yono
-Mateja,wapiga debe ,dereva unproffesional

hapo ndio utaona ukichaa wa biashara hii ya usafiri in TanzaGIza
 
Biashara isiyo pasua kichwa ninayoiona kwa TZ ni ya wasichana wa kazi kwenda Muscat na Saudia,nilikutana na jamaa anao wa 5,nikamuuliza sasa unawauza moja kwa moja au?Akasema la,kila kichwa akiwafikisha ni USD 2,000 halafu salary yao kwa mwezi ni 700USD yy anakula hapo 200 per head kwa 2 yrs, kama unajua kiarabu sawa la maana usiwe na yellow fever,malaria na HIV , kula kulala bure,ukijua kiarabu added advantage,nisichojua kwanini macho madogo ndio wengi kuliko ss muscat wakati sisi na e.g wa Myscat tunaelewana kiswahli>

Mkuu, unakumbuka bei kwenye miaka ya 1970 ilikuwa sh ngapi?
 
Duniani kuna biashara za kila aina! South Korea kuna wa Bangladeshi kazi yao kutoa watu Bangladeshi kuwaingiza South Korea!

Wanawapeleka kufanya kazi viwandani kila kichwa dola 10,000 miezi kumi jamaa wanafanya kazi ili walipe dola 10,000 unakuta mtu moja ana vichwa 10 mpaka 20
 
Wakuu ili tuweze kuwa makini na aina za biashara pale tunapotaka kuwekeza na kufanya biashara ninaomba angalau tujuzane biashara gani ni pasua kichwa (biashara kichaa) yaani katika makundi haya: hutumia muda mwingi, usumbufu mkubwa, risk kubwa na pia faida hupatikana kidogo .... hii ni katika level ya ujasiriamali .... assuming that unaifanya kwa ufanisi wote na discipline ya biashara

hapa tunaweza kupata na ufumbuzi wa mojawapo ya biashara pasua kichwa

  • yaweza kuwa biashara ya kuleta magari toka nje yasiyo na brand za kijapani .... kama vile volkswagon, hammer, Peugeot, Renault, BMW, range rover n.k ?
  • Biashara ya kuleta mkaa kama agent wa wachoma mikaa na kuwauzia retailers ?
  • biashara ya maji ya kunywa retail ?
  • biashara ya kuuza vocha za simu ?
  • biashara ya daladala ?
  • biashara ya bodaboda ?
  • biashara ya taxi ?
  • gutter politics (siasa uchwara) ...?
  • biashara ya udalali kishoka

na nyinginezo nyingi twaweza endelea kuzitaja na kuelezea

hakuna anayetaka kupasua kichwa kwa kufanya bishara kichaa ..... i stand to be corrected

Mimi naona LAT unawakilisha taswira za Watanzania/Waafrika wengi..... kuwa biashara ni kuweka mguu juu na kungojea faida tu! Huu ni uvivu na ndio maana Waafrika wengi hawainukii kuwa wafanyanyabiashara wakubwa. Watu wanachimba maelfu ya futi ardhini ili kupata bidhaa ije kuwa ki-deal na vitu ambavyo viko juu ya ardhi?
 

Similar Discussions

Back
Top Bottom